Ban Ki Moon amteua Mkapa kuongoza kura za maoni Sudan Kusini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ban Ki Moon amteua Mkapa kuongoza kura za maoni Sudan Kusini

Discussion in 'International Forum' started by MziziMkavu, Sep 25, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais Mstaafu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amemteua Rais Mstaafu wa Tanzania, Benjamin William Mkapa, kuongoza jopo la tume ya watu watatu itakayoangalia mchakato wa kura za maoni Sudan Kusini na Jimbo la Abyei.
  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa juzi, uteuzi huo unatokana na maombi yaliyotolewa pande mbili zinazounga mkono makubaliano ya amani ya kudumu nchini Sudan.

  Pande hizo ni Serikali ya Sudan na Kikundi cha People’s Liberation Movement.
  Wengine walioteuliwa ni aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ureno, Antonio Moteiro na Bhojraji Pokharel, Mwenyekiti wa zamani wa Tume ya Uchaguzi nchini Nepal.
  Akizungumzia uteuzi huo, Ban Ki Moon amesema, ana imani kwamba tume aliyoiteua itasaidia kufanyika kwa kura hiyo ya maoni itakayozingatia matakwa ya watu wa Sudan Kusini na Jimbo la Abyei.

  Jukumu kubwa la tume hiyo, pamoja na mambo mengine ni kufanya ziara za mara kwa mara nchini Sudani katika kipindi chote cha mchakato wa kuelekea kura za maoni.
  Upigaji wa kura za maoni unatarajiwa kufanyika mwezi Januari 2011, na tume hiyo pia inatarajiwa kukutana na kushirikiana na pande zote zinazohusika katika mkataba wa amani, tume inayoratibu kura ya maoni, jumuia za kiraia na makundi ya waangalizi wa kura hiyo.

  Pamoja na kutoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, tume hiyo itafuatilia kwa karibu mchakao mzima wa kura za maoni na pia masuala ya kisiasa na hali ya usalama.
  Tume itatakiwa pia kufanya kazi ya kuhakikisha inaimarisha imani ya mchako wa kura za maoni, kuhakikisha na kuzitaka pande husika na viongozi kuchukua hatua za pamoja za kutatua matatizo yoyote au migogoro itakayojitokeza.
  Wananchi wa Sudan Kusini, watapiga kura yao ya maoni kuamua iwapo wajitenge na

  Serikali ya Khartoum, wakati wananchi wa Jimbo la Abyei linalogombaniwa na pande zote mbili, wao watapiga kura ya kuamua wajiunge na upande upi iwapo Sudan Kusini itajitenga na Kaskazini.
  Upigaji wa kura ya maoni ni miongoni wa mabadiliko yaliyofikiwa katika Mkataba wa Amani wa mwaka 2005 (CPA), uliomaliza vita vya zaidi ya miongo miwili nchini humo.
  Aidha kura hiyo ni muhimu sana kwa mustakabali wa nchi yote ya Sudan.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. bona

  bona JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  nabii hakubalikagi kwao!
   
 3. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ben Mkapa ni mmoja kati ya viongozi wenye upeo wa juu katika tasnia ya diplomasia kimataifa ambao Tanzania imekuwaa nao..

  Uwezo wake na umahirii wake katika kuelewaa mambo na kuyasimamiaa ni wa kiwango cha juu.

  Congrats Ben for making Tz proud in the international arena.
   
 4. Lucchese DeCavalcante

  Lucchese DeCavalcante JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2010
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 5,473
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kabisa nagalau ana upeo wa juu kumzidi Rais wa sasa ambaye muda wake wa Ikulu ni kwishnei
   
 5. m

  mtukazi Member

  #5
  Sep 27, 2010
  Joined: Jun 8, 2010
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tunamshukuru ban ki mon kwa kuthamini mchango wa mtanzania huyu katika nishani za kimataifa
   
 6. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Vipi mbona JIRANI zetu wa KASKAZINI hawateuliwi kwenye nafasi nyeti za kimataifa kwani wanamatatizo gani?...:confused2:
   
 7. Smatta

  Smatta JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 2,343
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mkapa ako Juu tu sana.
   
 8. RealDeal

  RealDeal JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 297
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo Mkapa anastahili, alikuwa mojawapo ya waliosaidia Kenya wakati wa PEV 2007. Ako juu sana.
   
 9. A

  African Member

  #9
  Sep 27, 2010
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baadhi ya watanzani wamepata nafasi kubwa katika Tasnia ya kidplomasia kwa sababu wana upeo na weledi wa hali ya juu. Mfano Mzuri, Mahiga Augustin juzi kateuliwa kuwa special representative wa UN Secretary General Somalia, Salim Ahmed Salim aliongoza jopo la watazamaji wa uchaguzi huko rwanda. Warioba aliongoza jopo la watazamaji la common wealth huko Nigeria. Tibaijuka, head of UN habitat for quite long. Nadhani Tatizo la jirani zetu wako arrogant and their diplomats can not be trusted at international level?. Nadhani their thinking is highly influenced by their tribal background. To be able to function at international level you need to be independent thinker and someone really above your ethnicity. I dont see why tribal thinker can leas the international community.
   
 10. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2010
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Mkapa yupo juu sawa sawa hakuna wa kumlinganisha nawaambia!! hizo ni products za Mwl.Nyerere
   
 11. kanywaino

  kanywaino Senior Member

  #11
  Sep 27, 2010
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 171
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  napata utata hapo:confused2:
   
 12. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Na Luteni Yusufu Makamba, jakaya Kikwete, Kinana, Rostam ni product za nanni?
   
 13. RealDeal

  RealDeal JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 297
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  You don't have to compare yourself always with Kenya, I mean, this is about Mkapa, as an individual, respectable man he is. Why does it have always to be: we can do this better than them, they can't do this, blah... it's not necessary really.
   
 14. Smatta

  Smatta JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 2,343
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Do we really need this? Do you want to dilute the importance of this thread by debating on matters that dont relate in any way to the intention of the thread? Benjamin Mkapa is a respectable African, and we as Kenyans respect him on a different level because of his effort in the post election crisis. Stop and think before you type anything, the list of Tanzanian UN reps you have listed only confirms the obvious, stop wasting your time and do something constructive with your life.
   
 15. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #15
  Sep 27, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Huko anaweza kufanya kazi nzuri kwa sababu hana maslahi binafsi kama alivyokuwa Rais wa Tanzania!
   
 16. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #16
  Sep 27, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Mkapa is good but well, he allowed himself to conduct some stuffs that have let other people use against his credibility. Kama watu wengine wote waliowahi kukosea, if he had another chance, am sure he would do so differently on handling internal issues.
  Otherwise, I believe he will deliver maana yeye sio mtu wa sound hizi tunazosikia mpaka zinatoboa masikio
   
 17. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,924
  Likes Received: 1,029
  Trophy Points: 280
  Congrats Mkapa.
   
 18. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #18
  Sep 28, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160

  Punguza Jazba!.

  Issue ni kutaka kujua kama kweli hakuna top diplomats kutoka Kenya ambao wangeweza kusimamia migogoro inayotokea kila kukicha kwenye nchi zinazopakana na Kenya!! (mfano S. Sudan na Somalia.)

  Ukiondoa Tom Mboya na Dr. R. Ouko (WOTE MAREHEMU), Kenya ya sasa ina wanadiplomasia wa aina gani??
   
 19. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli argument yako haina mantiki kwenye thread hii. Lengo la thread si kujilinganisha au kutafuta ushindi dhidi ya Kenya.

  Hongera mzee wetu Mkapa.
   
 20. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #20
  Sep 28, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu maswali yanayoulizwa yanahusiana na thread yenyewe, kwani delimitations ni zipi?.

  Mkapa hajalinganishwa na mtu mwingine! (MTANZANIA GANI ASIYEJUA MATATIZO YAKE?) Issue ni kujua Kenya ya sasa ina wanadiplomasia wa aina gani na kwanini hawachaguliwi kusimamia migogoro inayotokea kwenye nchi inazopakana nazo.

  Kumbuka ni ndani ya miezi mitatu (3) tu tayari Ban Ki Moon ameshachagua wanadiplomasia wawili wakubwa (toka TZ) kwenda kusawazisha mambo huko Somalia na S. Sudani nchi ambazo zinapakana na Kenya na zenye umuhimu mkubwa sana kwa Kenya Kiuchumi, Kisiasa, na Kiusalama.

  Je shule/sera ya diplomasia ya Kenya inafuata mrengo wa aina gani? na inaproduce wanadiplomasia wa aina gani?
   
Loading...