Elections 2010 Ban Ki Moon amtakia Kikwete kampeni njema

Kanyafu Nkanwa

JF-Expert Member
Jul 8, 2010
849
103
NA MWANDISHI MAALUM

NEW YORK-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amemtakia kampeni njema , Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Rais Jakaya Mrisho Kikwete, na mafanikio mema katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba.

Ban Ki Moon ametoa salamu hizo wakati wa Mazungumzo yake na Mwakilishi mpya wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ombeni Sefue, mara baada ya Balozi huyo kumkabidhi hati zake za utambulisho katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.

Katibu Mkuu wa UN, pamoja na kumtakia kila la kheri na mafanikio Rais Kikwete, pia amempongeza Rais Kikwete na Tanzania kwa ujumla kwa kuwa nchi kiongozi na ya mfano wa kuigwa Barani Afrika katika kutekeleza na kuendeleza malengo ya Umoja wa Mataifa. Hususani amani na usalama Duniani.

Aidha Ban Ki Moon, ameonyesha imani kubwa kwa mwakilishi huyo wa Tanzania huku akimpongeza kwa nafasi za ubalozi alizoshika nchini Kanada na Marekani kabla ya wadhifa wake huo mpya.

Akamtaka kuendeleza msimamo wa Tanzania wa kuwa nchi kiongozi katika Afrika na ndani ya Umoja wa Mataifa kwa kudumisha na kuendeleza malengo yenye maslahi kwa Serikali ya Tanzania, Bara la Afrika na Umoja wa Mataifa kwa ujumla.

Ban Ki Moon akatumia pia nafasi hiyo kutoa shukrani zake, kwa mtangulizi wa Balozi Sefue, Balozi Augustine Mahinga ambaye katibu Mkuu alimteua kuwa mwakilishi wake maalum huko Somalia.

Katibu Mkuu akabainisha kuwa kutokana na heshima kubwa ambayo Tanzania imejijengea ndani ya Umoja wa Mataifa, anaitegemea Tanzania katika kuwasiliana na mataifa mengine hasa yale yanayoendelea.

"Tanzania mmejijengea heshima kubwa ndani ya Umoja wa Mataifa, kwa hiyo usitegemee kuwa utakuwa unaisemea Tanzania peke yake, bali na mataifa mengine pia, na hilo ndio tegemeo langu kubwa kutoka kwako Mhe. Balozi" akasisitiza Ban Ki Moon.

Katika mazungumzo hayo, Katibu Mkuu amemhakikishia Mwakilishi huyo wa Tanzania ushirikiano kutoka kwake yeye binafsi na sekretariati ya Umoja wa Mataifa.

Kwa upande wake, Balozi Ombeni Sefue amemwahidi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kwamba atafanya juhudi zote kuendeleza maslahi ya Tanzania katika UN, kudumisha ushirikiano mzuri kati ya UN na Tanzania, na kuchangia katika kuendelelezaji wa majukumu na malengo ya Umoja wa Mataifa.

Akatumia nafasi hiyo Kumpongeza Katibu Mkuu kwa kusimamia vema utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia, huku akimwomba aendelee kuzihimiza na kuziomba nchini zenye uwezo mkubwa kiuchumi ziendelee kuzisaidia nchi zisizokuuwa na uwezo ili ziweze kutekeleza Malengo ya Maendeleo ya Millenia.

Source: MICHUZI
 
We nini?
Kwani huyo Ban ndiye anatuchagulia rais wa nchi hii?
Katibu mkuu anayo haki ya kumtakia yeyote uchaguzi mwema lakini wanaochagua ni wananchi wa danganyika. Mpelekee Ban salaamkwamba rais ajaye anaitwa Dr W.P.Slaa
 
Kwa hilo hata Mugabe huwa anatakiwa kampeni njema kwa kutekeleza malengo ya Millenium Dev Goals! Hakuna kipya hapo.
 
wakuu mtoa mada anakanganya kumtakia heri JK hakumaanishi keshaupata urais after all JK ndo kamteua huyo balozi wategemea nn chacha
 
Hivi una akili nzuri wewe na unaelewa unachokisema? UKIWA SHABIKI WA KIKWETE BASI HATA AKILI YAKO INA KUWA KIKWETE KIKWETE HIVI.(Maana ya kikwete, ni mtu mvivu kufikiri)
 
Mkuu wangu Watanzania wengi wapiga kura hawamjui huyo Ban ki Moon wala hawana habari ya sifa alizopewa kwani huyo Moon haweki chakula mezani kwao.

Na hakika mtu wa kusifiwa ni Balozi Ombeni Sefue ambaye ni mchapakazi na kaweza sana kuimarisha zaidi mahusiano yetu na Marekani, binafsi namkubali. Huyu ni mtumishi wa Umma ambaye hata JK akiondoka madarakani bado anaweza kuendelea na wajibu wake kama balozi pasipo kuathirika na mageuzi yeyote ya uchaguzi huu..
 
Nakumbuka NARC ya kenya ilipokuwa pinzani ilishirikiana na wapinzani wa tz. Waliposhika madaraka waliambatana na ccm. Sioni ajabu kwa moon kumtakia kikwete kila la heri maana amezingatia itifaki . Ingekuwa kamaliza miaka 10 halafu moon akamuwish mgombea wa ccm hapo tungemwona juha.
 
"mfano wa kuigwa Barani Afrika katika kutekeleza na kuendeleza malengo ya Umoja wa Mataifa. Hususani amani na usalama Duniani".
Nildhani anampongeza kwa uchumi imara,elimu bora,kilimo cha kisasa,industrialization etc
Kama ni suala la amani indirectly anampongeza hayati Baba wa taifa ambaye aliiweka misingi ya amani kwa kuwaunganisha 120 ethnic groups

 
"mfano wa kuigwa Barani Afrika katika kutekeleza na kuendeleza malengo ya Umoja wa Mataifa. Hususani amani na usalama Duniani".
Nildhani anampongeza kwa uchumi imara,elimu bora,kilimo cha kisasa,industrialization etc
Kama ni suala la amani indirectly anampongeza hayati Baba wa taifa ambaye aliiweka misingi ya amani kwa kuwaunganisha 120 ethnic groups

Kwa kwahiyo Kiwete ametunza na kuimarisha vizuri yale ya baba wa Taifa?
 
Nakumbuka NARC ya kenya ilipokuwa pinzani ilishirikiana na wapinzani wa tz. Waliposhika madaraka waliambatana na ccm. Sioni ajabu kwa moon kumtakia kikwete kila la heri maana amezingatia itifaki . Ingekuwa kamaliza miaka 10 halafu moon akamuwish mgombea wa ccm hapo tungemwona juha.

Bado ni juha....mbona hakumtajia kila lakheri Kagame?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom