Bamileke: Kabila la Cameroon linalopingwa nakuogopwa na makabila mengine; ndio hao wanataka Cameroon ijitenge

Jon Stephano

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
5,559
2,000
Mzuka wanajamvi!

Hii dhana ya eti Cameroon majimbo mawili yanayoongea kiingereza North West na South West kujitenga kwasababu ya uonevu inasukumwa sana na Bambekee (Bamilekee).

Bambekee ni semi Bantuskabila maarufu sana Cameroon lenye maendeleo na elimu na pesa. Kwa kifupi ni matajari kama wachaga Tanzania na wakikuyu Kenya. Wanachokosa tu ni madaraka.

Cameroon ina makabila 240 yaliyogawanyika katika makundi matatu Bantus, Semi Bantus, Pygmies na Sudanese (Nitaleta uzi wa hizi kabila siku nyingine).

Cha kushangaza hawa Bambekee asili yao ni majimbo ya yanayoongea kifaransa ila walihamia kwa wingi katika majimbo mawili yanayoongea kiingereza ambalo moja limepakana na Nigeria South West lenye utajiri mkubwa wa mafuta.

Lakini makabila madogo asili ya haya majimbo ya Anglo phone yanayoongea kiingereza hawana shida ya kubaki Cameroun. Ila Bambekee wanawasukuma sana.

Bambekee wana nguvu sana na elimu. Wanajipenda sana na niwafanyabiashara. Wanapenda lugha yao sana na wanapenda kuoana wenyewe kwa wenyewe. Makabila mengine yote Cameroon wanawaogopa na wameapa kamwe hawatashikia madaraka.

Bambekee hata masokoni na kwenye maduka yao wako kivyaovyao na mda wote wanaongea lugha yao ambayo wanaipenda na kuithamini sana. Wengi wa Cameroon Diaspora ni Bambekee.

Bambekee wanamchukia sana Paul Biya. Paul Biya ni kabila la Fung jimbo la kusini mwa Cameroon South Province. Cha kushangaza akina Omar na Ally Bongo wa Gabon ni kabila moja na Paul Biya pia cha kushangaza zaidi Rais wa equatorial Guinea Teodoro Obiang ni kabila moja na Paul Biya ni mipaka tu imewatenga ambapo equatorial guinea ilikuwa koloni la Hispania.

Marekani, Uingereza pamoja na Ufaransa (kichinichini) wanawasupport Bambekee kuleta sintofahamu camerroon. Utashangaa kwanini Ufaransa naye kichinichini anawasupport Bambekee ni kwasababu wameshakosana na Paul Biya.

Makabila mengine Cameroon wanakubali ndio Paul Biya ni dikteta lakini wako radhi aendelee kutawala tu kuliko Bambekee washike madaraka.

Kwenye mpira Bambekee hawapo wengi sana ni Jeremy Njitap tu. Kabila la Bassa ndio wachezaji mpira ni wengi kama etoo Rodger milla na Rigobert Song.

Bambekee ndio tatizo kubwa la kutaka anglophone kujitenga wakisaidiwa na Marekani, Uingereza na Ufaransa ambaye anang'ata na kupuliza. Lakini siyo Wenyeji asili wa hayo majimbo yanayoongea kiingereza.

Source wa Cameroon

Senior JF international political correspondent and analysts
 

Jon Stephano

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
5,559
2,000
Sasa hivi Dayaspora Cameroon wengi Bambekee wanakuwa na mikutano yao wakichangishana hela kununua silaha kuingiza Cameroon. Makabila mengine wanahuzunika sana kwa nini wanafanya hivyo.

Kwasababu makabila Cameroon yameingiliana sana kwa kuoana kwa miongo mingi. Bambekee bado wako wengi tu kwenye majimbo yao ya asili yanayoongea kifaransa. Kwanini wawe selfish kwa kuleta umwagaji wa damu? Marekani, Uingereza na ufaransa ni hatari.
 

Eng. Zezudu

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
3,957
2,000
Ubinafsi tu, hamna lolote, hata wachaga nao ubinafsi umewajaa Sana, their head is filled with Mimi mchaga, ukabila niwakupigwa vita unavuruga Taifa.
 

tyc

JF-Expert Member
Feb 25, 2014
633
1,000
Kipimo kikuu sahihi cha kusoma ni kuelimika na kutawala mazingira yako, Jamii yako na ikibidi dunia.

Ukiona umesoma na bado huwezi kutawala Jamii yako basi ujue hujaelimika, hujakidhi takwa sahihi la kielimu, unajisifuje umesoma ilhali bado ktk eneo ulilopo unatawaliwa na uliowazidi elimu!?
 

Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
2,428
2,000
Ila mfano wako unachembechembe za ubaguzi na chuki na ukabila kwa baadhi ya watu, zaidi wale usio wapenda.
 

The 13

JF-Expert Member
Oct 14, 2018
1,874
2,000
Umendika kishabiki kinoma afu izo sifa zingine sio za wachaga mkuu.
 

Jon Stephano

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
5,559
2,000
Umendika kishabiki kinoma afu izo sifa zingine sio za wachaga mkuu.
Wachaga ni wafanyabiashara wakubwa na elimu kubwa na maendeleo ndio maana makabila mengine Tanzania wanawaonea wivu. Huoni Mwanaume Mbowe anavyoandamwa kisa mchaga.
 

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
5,302
2,000
Sasa hivi Dayaspora Cameroon wengi Bambekee wanakuwa na mikutano yao wakichangishana hela kununua silaha kuingiza Cameroon. Makabila mengine wanahuzunika sana kwa nini wanafanya hivyo.
Wanaitwa Bamileke siyo Bambekee mkuu. Na maendeleo yao yako sana connected na raisi Paul Biya maana pia anatoea kabila hil hivyo wanapata upendeleo sana kutoka serikalini.
 

Jon Stephano

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
5,559
2,000
Wanaitwa Bamileke siyo Bambekee mkuu. Na maendeleo yao yako sana connected na raisi Paul Biya maana pia anatoea kabila hil hivyo wanapata upendeleo sana kutoka serikalini.
Mkuu umesoma vizuri Uzi wangu. Bamileke/Bambekee. Wa Cameroon wanatamka Bambekee. Source wa Cameroon wenyewe ninaofanya nao kazi. Soma aya ya kwanza
 

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
5,302
2,000
Mkuu umesoma vizuri Uzi wangu. Bamileke/Bambekee. Wa Cameroon wanatamka Bambekee. Source wa Cameroon wenyewe ninaofanya nao kazi. Soma aya ya kwanza
Wanatamka Bamileke na mimi source ni ndugu yangu rafiki yangu Mcameroon ambaye ndiye Mcameroon aliyeongoza chama Wacameroon waishio TZ kwa muda mrefu.
 

Jon Stephano

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
5,559
2,000
Wanaitwa Bamileke siyo Bambekee mkuu. Na maendeleo yao yako sana connected na raisi Paul Biya maana pia anatoea kabila hil hivyo wanapata upendeleo sana kutoka serikalini.
Mkuu Bambekee ndio Adui mkubwa wa Biya. Hawana conbection yoyote na Paul Biya hao ndio wanamtaka Biya atoke
 

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
5,302
2,000
Mkuu Bambekee ndio Adui mkubwa wa Biya. Hawana conbection yoyote na Paul Biya hao ndio wanamtaka Biya hatoke
Paul Biya anatokea katika kabila lao, japo nao kwasasa wamemchoka pia ila aliwapendelea sana, hata baada ya Biya kufanya mapinduzi aliyemkingia kifua na General naye ni Mbamileke pia otherwise angepigwa chini.
 

Jon Stephano

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
5,559
2,000
Wanaitwa Bamileke siyo Bambekee mkuu. Na maendeleo yao yako sana connected na raisi Paul Biya maana pia anatoea kabila hil hivyo wanapata upendeleo sana kutoka serikalini.
Paul Biya anatokea kabila la Fung South Province anashare kabila moja na rais wa Gabon Ali Bongo na rais wa equatorial guinea
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom