Balozi zetu bado hazitangazi Utalii na si Msaada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balozi zetu bado hazitangazi Utalii na si Msaada

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Jun 10, 2008.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,828
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  Nimepata habari hizi muda na mtu mmoja kwa kuniandikia mail .Lakini pia huu ni uzoefu wangu wa miaka madhaa niliyo kuwa nakaa Ughabuni kwamba mabalozi wetu watumishi wao wamejaa dharau , majivuno na maneno machafu.Watu wamekuwa wakilalama kila mara na utawaona wanafanya kazi kama watasikia Rais ama Makamo wa rais anapita ama waziri vinginevyo hakuna lolote

  Nimepata habari za watu 3 Watanzania , wazungu kibao wanalalamikia huduma katika balozi zetu .Mtu wa mwisho ameenda Ubalozini kwetu zaidi ya miezi 3 anaomba info za utalii wa Tanzania lakini hadi sasa hajapewa na kakata tamaa .Balozo zinafanya kazi kwa kujisikia na kejeli wakati wanaishi kwa pesa yetu .Balozi hizi sasa zinashindwa hata kumuunga mkono Rais kwa juhudi za kuitangaza Tanzania , Utalii na vivutio vyake .

  JK kwanza anza na Japan ujue kuna shida gani .Ukitaka ushahidi ninao na sasa nitakupe skendo za kila Balozi na hasa kwenye kuitangaza Nchi .Hawakusaidii wewe wala mimi wala Nchi yetu wao wana maringo yako na kujivuta vuta .

  Ni kweli Ubalozi wa Japan hauna posters wala DVD za Utalii hadi Wajapan wanaaanza ku haha kutafuta info kivyao ?
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,828
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  Hakuna watu wenye habari za balozi zetu hapa jamani ? Ama aliye karibu na Membe amweleze ?
   
 3. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2008
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,383
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  nadhani ni muhimu kujua kama balozi zimewasiliana
  na taasisi husika na kuomba machapisho, vipeperushi
  na hata dvd zinazohusu utalii. kama hazijafanya hivyo
  hayo ni mapungufu/uzembe wa balozi zetu. kama
  balozi zimeomba taasisi husika na hizo taasisi hazija
  wajibika basi taasisi huzika zitakuwa hazijatimiza wajibu
  wao na zimefanya uzembe.

  je hizo taasis husika zimefanya juhudi zozote za kuwasiliana
  na kutuma hizo taarifa kwa balozi zetu na kisha balozi
  zetu zikarudisha hizo taarifa au kukataa?

  je wizara ya mambo ya nje inao mfuko wa kutengeneza
  vipeperushi, machapisho, filamu n.k. za kutangaza utalii
  na wameshindwa kutumia huo mfuko/bajeti?

  kweli balozi zetu zinaendeshwa kwa kodi zetu, je kuna mtu
  anayejua kama hizi balozi zinapelekewa hiyo mishahara kila
  mwezi au kuna wakati jamaa wanakaa bila mishahara kwa
  miezi zaidi ya miwili? mimi nafahamu kuna wakati maafisa
  wa ubalozi walikuwa wanakaa bila mishahara hata kwa miezi
  mitatu. sasa pengine huko kuzembea kwa hao maofisa kunatokana
  na mawazo ya kutokuwa na mishahara?

  dharau, kujiona n.k. hizo ni hulka za baadhi ya watu. naamini
  kwenye balozi zetu wapo watu wenye ubinaadamu sana tu.
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,828
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  Machapisho yana kwenda kote ndiyo jambo mojawapo ambalo balozi zinahusika nazo .Kwa taarifa yako ni kwamba kila Ubalozi una mtu wa kushughulila na tourism.Mishahara ni soo hapa naongea nawe kuna balozi hawajapata mishahara na hata mambo yao ya likizo yako on hold .Nimeuliza wanasema hakuna pesa na hata bills kulipa ni shida lakni bado watu wana vijisenti na Serikali na hata watumishi wana njaa .

  Lakini wakiwa ofisini lazima kusimamia kazi zao maana waliweka mkataba na kama wanagoma basi watangaze .Tabia za njoo kesho zinachosha sana kila ni tourism info na wageni wanataka kuja Tanzania .Je hawaoni wanajinyima mishara wenyewe ? maana serikal ikusanye walipwe wao .

  Naomba Ubalozi wa Japan umulikwe sasa .Kuna shida pale kubwa kwenye Dept ya Utalii .
   
Loading...