Balozi wa USA anataka maswali yetu

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,546
838
Mindhali humu ndani watu ni mahiri wa kujadili mambo lakini naona its about time kama kweli watu wako serious na kutaka dunia ijue kinachoendelea Tanzania basi hatuna budi kujitahidi kufanya mijadala kwa KIINGEREZA

Serikali yetu haioni umuhimu wa haya mamabo ya Internet au hili lakini sisi hatuwezi kukaa kusubiri serikali.Sidhani kama hao watu wa EU au USA au TRANSPARENCY INTERNATIONAL watakuwa na muda wa kukaa kuanza kutafsiri haya ma dossier ya UFISADI yaliyoandikwa kwa kiingereza

Najua kuna watu watalalamika kuwa wao KISWAHILI ndio rahisi lakini ukweli ni kuwa DUNIA IKO CONNECTED kwa ENGLISH sasa tuache kujiongopea eti tuna impact na hawa wanatupa pesa za kuendesha nchi zetu

hilo ni wazo tuu kati ya mengi ambayo inabidi yafanyike ili JF iwe na impact ya kutosha nje ya nchiBalozi wa Marekani kujibu maswali moja kwa moja kupitia mtandao

Balozi Mark Green atajibu maswali kutoka kwa Watanzania kupitia mjadala wa moja kwa moja, kwa njia ya mtandao wa komputa, ambao umepangwa kufanyika Jumatatu Oktoba 29, 2007 kuanzia saa tisa mchana.
Katika kipindi hicho cha majibu na maswali, Balozi Green atajadili kuhusu msaada wa dola milioni 698 utakaosaidia kupunguza umaskini nchini Tanzania, ambao uliidhinishwa hivi karibuni.

Balozi Green amesema kuwa huenda maneno “MCC” na “sheria ya Millennium Challenge” yakawachanganya baadhi ya watu hapo mwanzoni, lakini baada ya muda kidogo, Watanzania watajifunza jinsi mpango huo unavyoweza kuleta tofauti kubwa kwatika maisha yao. “Pindi mkataba mpya wa MCC utakapotiwa saini na Serikali ya Tanzania, utajenga ushirikiano wa karibu zaidi kati ya mataifa yetu mawili.”

Mpango huo wa MCC uliotolewa na wananchi wa Marekani, ni mpango wa miaka mitano ambao lengo lake ni kupunguza umaskini, kuchochea kukua kwa uchumi, na kuongeza kipato cha wananchi kupitia uwekezaji maalum katika miundombinu ya sekta za usafiri, nishati na maji nchini kote Tanzania.

Ili uweze kujiandikisha kushiriki kwenye mjadala huu wa mtandao, tumia anuani yako ya barua pepe kuingia kwenye ukurasa wa tovuti ya http://webchat.state.gov.
Unaweza pia kuingia kwenye mjadala huo wa mtandao kupitia ukurasa wa tovuti yetu - http://tanzania.usembassy.gov.
 
watahakikisha vipi hizo pesa zinatumika vizuri maana historia inajionyesha pesa kama hizo huwa zinaliwa na wajanja wachache? na jee kuna wataalam wowote kutoka US katika miradi ya pesa hizo na kama wapo watalipwa vipi maana historia inaonyesha wanaotupa misaada wanatuletea na wataalam wao ambao tunaishia kuwalipa zaidi ya nusu walizotupa.
 
Nakubali hoja yako Game Theory! Napendekeza Jambo forums ianzishe special forum ya kiingereza tuwe active na tuanike mikataba na mambo mengine kwa kimombo!
 
GAMETHEORY
Naungana na wewe kwa asilimia zote. Kiingereza sio lugha yetu ya kwanza kwa hiyo hata hao ambao ni lugha yao ya kwanza wanaweza kuelewa hilo, lakini cha muhimu ni kuwa wajue nini watanzania tunafikiri kuna wanajambo wengi sana wanasukuma kiingereza kwa kiwango ha kuweza kufikisha ujumbe vizuri, wazo lako nakubaliana nalo kabisa. Tunaweza kuwa na forum nzuri ambayo hata watu wanaoweza kutusaidia kurekebisha mambo hapa nyumbani wakajua yanayoendelea
 
Haya mambo mgeyaongea leo mgeambiwa nyie sio WAZALENDO. Huu uzi una miaka 12, Britanicca kauchokonoa. Tanzania yetu hii, watasema mbona China wameendelea bila Kiingereza, na Mbona Urusi walifika mwezini bila kiingereza. Urgument zetu utasikia wajifunze wao ndio wanashida, hahahaha.
 
Back
Top Bottom