Balozi wa TZ nchini China yuko kwa maslahi ya nani??.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balozi wa TZ nchini China yuko kwa maslahi ya nani??....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nderingosha, Oct 25, 2012.

 1. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,526
  Likes Received: 1,312
  Trophy Points: 280
  Kuna mengi yamekuwa yanazungumzwa kuhuu teuzi tata za watendaji wa JK...iwe ndani ya nchi au hata nje ya nchi.....mengi yakisemwa kuwa teuzi hizi huusisha kupeana ulaji etc etc....Mojawapo ya teuzi tata alizowahi kufanya JK ni hii ya balozi wa tz nchini China......wengi wakilalamika kuwa huyu balozi Marmo amechoka na uwezo wa kuiwakilisha tz kwenye nchini inayokuwa kiuchumi haraka kama China ni mdogo....Pia malalamiko haya yamekuwa yakiweka shaka juu ya uwezo wa huyu balozi kuwakilisha maslahi ya TZ na watanzania ndani ya China....hasa ukizingatia sharpness ya wachina katika issues zenye maslahi kwa nchi yao.....

  Leo nairudia tena hii mada kumhusu huyu balozi.....nikileta mashaka makubwa juu ya uwezo wa huyu balozi kusimamia haswa maslahi ya watanzania walioko China.....hapa nikiwagusa wanafunzi wakitanzania wasomao China......Katika post yangu iliyopita nilitoa dukuduku zangu dhidi ya huyu balozi...lakini wengi walidhani kuwa ilikuwa mapema mno kumlaumu huyu bwana kwani alikuwa bado hajajitambulisha kwa watawala wa China.....wengi wakisema tumpe muda kwanza aijue China vizuri.....soma hii post...https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/278144-kimeo-kipya-cha-jk-china-balozi-aliyelala-usingizi-mpaka-sasa.html.....

  Leo hii umeshapita almost mwaka tangu balozi awepo kazini... lakini matatizo ya wanafunzi wa kitanzania China yanaongezeka....pamoja na kuletewa balozi mpya.....Leo hii wanafunzi walioko mwaka wa pili...tatu na kuendelea bado wanalia hawajapata pesa yao ya mkopo toka bodi ya mikopo(HESLB)....kisa eti majina ya account zao hayajapelekwa bodi ya mikopo toka Ubalozini China......imebidi wanafunzi waanze kulalalmika mmojmmoja ndipo ubalozi uanze kushughulika.......mbaya zaidi wanafunzi wamekuwa wakijitatulia matatizo yao mmoja mmoja kwa kupitia contacts zao dar...kama vile hakuna ubalozi wa TZ nchini China......(haya yote nimeyapata toka kwa contacts/sources zangu China)...Ukizungumza leo hii na mwanafunzi yoyote anayesoma China atakwambia hali halisi ndio hiyo.....na haya matatizo yamezidi kuwepo tangu awepo huyu mzee marmo.....miaka ya nyuma hakukuwa na haya matatizo kwa kiasi hiki.....

  Watu watasema haya ni matatizo ya mwambata wa elimu lakini yeye mwambata yupo chni ya balozi....Kinachouma sana na kinachoonesha kwamba huyu balozi hayupo serious na issues za wanafunzi ni kitendo cha yeye kutokutafuta audience na wanafunzi wakitanzania wasomao China ili angalau kusikiliza kero zao.....yeye yupo kama hayupo.....Sasa wanafunzi wanauliza yupo kwa maslahi ya nani kule China???..wanafunzi wanaishi kama yatima wasio na baba.....na kinachowasaidia sana ni ile posho kidogo wanayopata toka kwa serikali ya kichina otherwise mambo yangekuwa mabaya sana kwa hawa wanafunzi.....

  Ni wakati sasa kwa JK kuanza kupima utendaji wa mabalozi wake nje ya nchi akiwepo huyu bwana Marmo....vinginevyo....itabaki kujidhihirisha tu kuwa teuzi hizi ni za kupeana ulaji tu.....na labda mbaya watazidi kuitia aibu TZ kwa utendaji dhaifu....na labda tuzidi kusikia scandles tu toka pande za Uchina(e.g fake contracts...au TZ officials in ivory theft..etc etc)...we need serious people out there(China)......a wake up call for JK........
   
Loading...