Balozi wa Tz amvisha mkewe kimasai ndani ya Buckingham Palace!!

Kwa nini yeye mwenyewe hakuvaa kimasai kama mnasifia yeye? Eti kwa "kumvisha mkewe," hatuwezi kusema "mkewe kavaa"?

Picha yenyewe sioni uhusiano wowote na "baada ya kumwona Malkia," vipi alirudi ubalozini kusoma hotuba za kimasai?

Na mimi kuona picha tu nikaona mfumodume na wanawake kufanywa kama vito na sio watu.

Balozi katinga bonge la suti la kizungu, mkewe katinga kimasai. Waingereza lazima watakuwa wameshangaa sana hili mismatch. Inazidi ku validate notion kwamba Afrika mke ni urembo wa nyumba.

Mimi sina tatizo na Watanzania kuvaa kimasai, kwani hatuna a national dress ambayo ungesema balozi angeivaa, na Wamasai ni moja ya makabila yanayojulikana sana duniani kutoka Tanzania, lakini kama tunaamua kuvaa kama wamasai basi balozi na mkewe wote wangevaa kimasai.
 
Back
Top Bottom