Balozi wa Tanzania Nchini Malaysia kujitetea Baraza la Maadili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balozi wa Tanzania Nchini Malaysia kujitetea Baraza la Maadili

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by nngu007, Jun 21, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Tuesday, 21 June 2011 19:41 newsroom


  NA HAMIS SHIMYE
  BALOZI wa Tanzania nchini Malaysia, Abdul Sisco Mtiro, leo atahojiwa na Baraza la Maadili, kutokana na kutowasilisha tamko la mali na madeni kwa Tume Maadili ya Viongozi wa Umma.

  Tangazo lililotolewa jana na tume, lilisema balozi huyo ataanza kujitetea leo asubuhi katika ukumbi wa Karimjee, mjini Dar es Salaam. Sisco atatoa utetezi mbele ya jopo la majaji wa baraza hilo, linaloongozwa na Mwenyekiti Jaji mstaafu, Damian Lubuva.

  Baraza hilo jana lilimhoji Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rorya, Charles Ochere, kutokana na kushindwa kuwasilisha tamko la mali na madeni kwa tume ya maadili.

  Akitoa utetezi, Ochere alisema alishindwa kujaza fomu hizo kutokana na kuchaguliwa kuwemo katika tume ya kuchunguza upotevu wa sh. milioni 500 uliotokea ndani ya halmashauri hiyo. “

  Nimekuwa nikijaza fomu vizuri tangu mwaka 2005 hadi 2008, lakini 2009 nilishindwa kujaza kutokana na kuwepo ndani ya tume,’’ alisema. Kutokana na hilo, Mwanasheria wa tume, Hassan Mayunga, alidai hoja za mwenyekiti huyo hazina mantiki kwa kuwa ni za hisia.

  Jaji Lubuva alisema baraza litatoa uamuzi baada ya kupitia utetezi huo.
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Jeuri na kiburi anajuaa kuitwa kwake kuja tz watamlipa atatoa pumba watampa onyo aatarudi zake Malaysia hana shida hy tume haina meno ni mkwara mbuzi tu!
   
 3. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 1,813
  Trophy Points: 280
  hivi kwa nini wa malysia wasitumie ubalozi wa beijing! .. Malysia as i know sio mbali na china..! kwa sasa ubalozi wa beijing unahudumia veitam na mongolia nadhani ... nakumbuka kipindi cha zamani bongo kulikuwa hakuna ubalozi wa Greece tulikuwa tunatumia wa Nairobi
   
 4. mchakachuaji192

  mchakachuaji192 JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Ni kweli kabisa Malaysia na China sio mbali, mie nimekaa hapa Malaysia mwaka wa tatu huu sasa sioni faida ya kuwepo huu ubalozi wetu huku zaidi ya hawa walioko ubalozini kuandaa vipati vya kijinga kuwaalika wanafunzi nyumbani kwa balozi na mwisho wa siku dada zetu wanaangukia pabaya (kuna katabia kapo ka hawa watu kutembea na wanafunzi wakienda huko kwenye sherehe zao) pia hakuna ushirikiano kabisa huku kama walivyo wenzetu wa UK na USA na kwingineko, hapa hakuna association yeyote ile ya watanzania kama ilivo India, yaani tupo tupo , na huo ubalozi wenyewe uki-google hauonekani unapewa majibu ya ubalozi wa Singapore, nilichokiona mie unaendeshwa kisanii sanii tu

   
Loading...