Balozi wa Sweden atembelea Ofisi za JamiiForums

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,441
215,219
Hii ndio taarifa mpya inayosambaa mitandaoni kwa sasa na ni Heshima kubwa sana kwa JF na ni recognition ya nguvu sana.

Kutambuliwa huku kwa JF na Jumuiya za Kimataifa kunakuja kutokana na UHURU MKUBWA WA KUTOA MAONI NA JUHUDI ZA MAKUSUDI ZA KULINDA FARAGHA ZA WATEJA WAKE.

Mungu ibariki JF

=========

Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Anders Sjöberg leo Februari 1, 2022 ametembelea ofisi za JamiiForums na kukutana na watendaji na mwakilishi wa Bodi ya Wakurugenzi wa JF.

Pamoja na mambo mengine, ameweza kujua namna Jamii Forums inavyoendesha shughuli zake katika kuhakikisha inafanya uchechemuzi wa Haki za Kidijitali, Uwajibikaji, Demokrasia na Utawala Bora nchini Tanzania.

JF inasimamia mtandao wa JamiiForums.com unaotoa nafasi kwa Watanzania kutumia #UhuruWaKujieleza kwa njia ya mtandao na kujadili masuala anuai, ikisaidia wananchi (Citizen Journalists) kupaza sauti zao


496F01A9-D033-48F8-BD84-804BFA078AF7.jpeg
E87BAF56-F3B0-4EE8-94B4-D018B8123115.jpeg
F5451618-EC27-4469-ACAB-22829153B5DC.jpeg
8B887C7C-35E4-402F-986A-7492EA961B11.jpeg
E303EEE1-2704-4F0F-97BB-D6ADB212DF26.jpeg
 
Hivi Hawa JF wao wananufaikaje kwenye huu mtandao, maana naona tunaingia bure kabisa na kujimwaga tu.

Sitaki muamin et mb ndio faida yao maana hata mb huu mtandao unakula kidogo Sana.

Mwenye uelewa plz anitoe tongotongo hapa
 
Hivi Hawa jf wao wananufaikaje kwenye huu mtandao ,maana naona tunaingia bure kabisa na kujimwaga tu.

Sitak muamin et mb ndio faida yao ,maana hata mb huu mtandao unakula kidogo Sana.

Mwenye uelewa plz anitoe tongotongo hapa
Wewe kuwepo JF tayari inamuongezea kipato kupata watangazaji wa biashara, hakuna mfanya biashara kichaa akatangaze biashara kwenye mazingira yasio na watu..nikuongezee nyingine? Nikikupa faida nyingine JF inapata utajilaumu kwanini hujawa na akili kama Maxence Melo
 
61 Reactions
Reply
Back
Top Bottom