Balozi wa Redds arudisha taji

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Balozi wa Redds arudisha taji

ANGELA.JPG

Angela Luballa

Angela Luballa leo aliwashangaza watu alipoamua kurejesha taji hilo wiki moja tangu avalishwe.
Luballa ambaye pia alishika nafasi ya tatu katika shindano la kumsaka Miss Tanzania, amesema kuwa imani yake haimruhusu kuwa Balozi wa REDDS.
“Imani yangu kwa Yesu ni kubwa mno na hainiruhusu mimi kuwakilisha REDDS, hivyo nimeamua kurejesha taji na zawadi za fedha nilizopewa,” alisema Luballa.
“ Nimerudisha taji hili si kwa shinikizo la mtu yeyote bali ni imani yangu, siwezi kuwa balozi wa REDDS.”
Luballa ambaye inaaminika ni mtoto wa mchungaji ana imani ya kanisa lao ambalo haliruhusu kujihusisha na kitu chochote kinachohusu pombe.
Luballa anasali katika Kanisa la World Alive International Outreach lililopo Sinza.
Mrembo huyo alisema kuwa tayari ameshaiarifu Kamati ya Miss Tanzania na kurudisha taji na fedha Sh milioni 2.5 alizopewa kwa kutwaa taji hilo.
Tangu mwaka 2006, REDDS imekuwa na utaratibu wa kumtangaza balozi wa bidhaa hiyo ambaye anapewa majukumu ya kufanya shunguli za kijamii kupitia kinywaji hicho.
Kwa ushindi huo, Luballa alitakiwa kupewa Sh milioni 2.5 na posho ya Sh 250,000 kwa mwezi kazi ambayo angeifanya kwa mwaka mzima.
Taji la Miss REDDS mwaka jana alikuwa ni Victoria Martin.
Alipoulizwa Mratibu wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga alisema kuwa tayari ameshapata taarifa za kurejeshwa kwa taji hilo.
“ Mimi niko nje ya mji, ila nimeshapewa taarifa kuwa mrembo huyo amerudisha zawadi, nitalizungumza kwa kina pindi nitakaporejea,” alisema.
 
Back
Top Bottom