Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen amesema Tanzania ni kielelezo amani Barani Afrika

Afrika hakuna Uhuru Haki maendeleo wala Democrasia.

Afrika kuna Udikteta.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Siasa Chafu.
Njaa na umasikini Uliotopea.
Lakini hawauawi Watanzania kama ngedere, huko unakosifia wanauawa raia wangapi kwa siku/mwezi?
 
Attachments

  • 2297351_tapatalk_1580646729833.jpeg
    2297351_tapatalk_1580646729833.jpeg
    21.5 KB · Views: 2
Yeyote anayetetea maslahi Tanzania ni mwenzetu kinyume na hapo si mwenzetu
Leo ni mataifa rafiki, ila juzi BBC Swahili aliitwa Beberu. Yani hadi Zuhura Yunus aliitwa Beberu juzi tena na Pascal Mayalla
 
Ndugu zangu,

Tanzania inazidi kupaaa

========

Tanzania imetajwa kama Nchi ya kielelezo cha amani na demokrasia katika Bara la Afrika kutokana na mchakato wa kampeni za uchaguzi mkuu unavyofanyika kwa amani,utulivu na usawa kwa wagombea wa vyama vyote huku wananchi wakijitokeza kwa wingi kusikiliza sera za wagombea.

Balozi wa Norway nchini Tanzania Balozi Elisabeth Jacobsen ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi.

333.JPG

Pamoja na masuala ya kisiasa Balozi huyo amesema katika mazungumzo yao wamegusia pia masuala ya ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi hususani katika suala la elimu,afya,nishati na uwekezaji pamoja na biashara baina ya nchi hizo mbili.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amemuomba Balozi huyo wa Norway kuendelea kushirikiana na Tanzania na kumshukuru kwa Nchi hiyo kukubali kutoa kiasi cha dola za marekani milioni 7 kwa ajili ya mradi wa TASAF jambo litakalosaidia kupunguza umasikini kwa watanzania hususani katika kipindi hiki ambapo nchi nyingi zimeathiriwa na janga la Corona.

Mbali na Balozi huyo wa Norway pia Prof. Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden hapa nchini Balozi Anders Sjöberg ambapo amezungumzia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi,haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari na kuvipongeza vyombo vya habari hapa nchini kwa kuandika habari za wagombea wa vyama vyote bila ya ubaguzi.

111.JPG

Kuhusu suala la haki za binadamu Prof. Kabudi amesema taswira inayotolewa kuhusu suala hilo haiakisi hali halisi iliyopo nchini na kwamba Tanzania inaheshimu na kulinda misingi ya haki za binadamu.

Katika tukio jingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amepokea nakala za hati za utambulisho za Balozi Mteule wa Uswis hapa Nchini Mhe. Didier Chassot.
Tuko vizuriiii mpaka beberu limesifia🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Attachments

  • 2525669_IMG_20200913_220650.jpg
    2525669_IMG_20200913_220650.jpg
    33.2 KB · Views: 2
Mmh hii balozi siielewi, yaani mapema yote hii unatuambia demokrasia ahahahaaa 🤣
Ulitaka aseme uyawazayo moyoni?

Mwaka huu jiandaeni kushuhudia ushindi wa KIHISTORIA JPM atawakalisha wapinzani.

CCM 5 Tenaa
 
😅😅Leo ni mataifa rafiki, ila juzi BBC Swahili aliitwa Beberu. Yani hadi Zuhura Yunus aliitwa Beberu juzi tena na Pascal Mayalla
Kama Zitto kabwe ambaye wakati mwengine huonekana ni msaliti tu na hata hicho cha chake kipo ili kuvuruga upinzani ila wakati mwengine akiongea yale ambayo watu hupenda kuyasikia basi haonekani tena kuwa msaliti.
 
Hizi ndo zile habari ambazo mwandishi anakufuata anakuuliza vip Mr Livingstone unaonaje siasa na demokrasia nchini Tanzania? Unadhani mr Livingstone ataanza kusema "kuna siasa chafu sana na ubinywaji wa demokrasia nchini na hivi vitendo tunavilaani sana". Hahaha, mataga na vijarida vyao kazi ipo.
 
Balozi wa Norway nchini Tanzania
Elisabeth Jacobsen amesema Tanzania ni kielelezo amani barani Afrika kwa kuwa Kampeni za uchaguzi zinafanyika kwa uhuru,
amani na utulivu. Amesema kutokana na hayo Tanzania ni kinara wa demokrasia katika mchakato wa uchaguzi

Chanzo: Habari Leo
May be the word democracy has lost its meaning.
 
Misimamo ya Norway kuhusu Haki za Binadamu na Utawala Bora ndiyo msingi wa kila kitu na itaendelea kusaidia jambo hilo lifanikiwe mfano mchango wao kwa Asasi ya Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Bindamu ili kusaidia Utawala bora Tanzania :

Anna Henga, Executive Director of LHRC, and ambassador Elisabeth Jabosen after signing the new core support agreement - Photo:LHRC

Anna Henga, Executive Director of LHRC, and ambassador Elisabeth Jabosen after signing the new core support agreement LHRC
Norway signs new core support agreement with LHRC
On Tuesday April 16 2019, Ambassador Elisabeth Jacobsen signed a three-year core support agreement with the Legal and Human Rights Centre (LHRC) worth USD 2.2 million to support LHRC’s Operational Plan 2019-2021, being part of the six-year strategic plan 2019-2024.
23. Apr 2019
Norway is a strong supporter of human rights in Tanzania and is happy to announce our continued partnership with LHRC. LHRC plays an important role in advocating for and defending human rights in Tanzania by working towards more transparency, accountability and freedom of expression. Furthermore, Norway supports LHRC’s continued effort to improve policy and legal frameworks for specific rights for women, children and people with disabilities. Norway has been supporting LHRC core activities for more than fifteen years including a USD 5 million grant to the Centre between 2013 and 2018.

Source : Norway signs new core support agreement with LHRC
 
Ndugu zangu,

Tanzania inazidi kupaaa

========

Tanzania imetajwa kama Nchi ya kielelezo cha amani na demokrasia katika Bara la Afrika kutokana na mchakato wa kampeni za uchaguzi mkuu unavyofanyika kwa amani,utulivu na usawa kwa wagombea wa vyama vyote huku wananchi wakijitokeza kwa wingi kusikiliza sera za wagombea

Balozi wa Norway nchini Tanzania Balozi Elisabeth Jacobsen ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi

333.JPG

Pamoja na masuala ya kisiasa Balozi huyo amesema katika mazungumzo yao wamegusia pia masuala ya ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi hususani katika suala la elimu,afya,nishati na uwekezaji pamoja na biashara baina ya nchi hizo mbili.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amemuomba Balozi huyo wa Norway kuendelea kushirikiana na Tanzania na kumshukuru kwa Nchi hiyo kukubali kutoa kiasi cha dola za marekani milioni 7 kwa ajili ya mradi wa TASAF jambo litakalosaidia kupunguza umasikini kwa watanzania hususani katika kipindi hiki ambapo nchi nyingi zimeathiriwa na janga la Corona.

Mbali na Balozi huyo wa Norway pia Prof. Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden hapa nchini Balozi Anders Sjöberg ambapo amezungumzia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi,haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari na kuvipongeza vyombo vya habari hapa nchini kwa kuandika habari za wagombea wa vyama vyote bila ya ubaguzi.

111.JPG

Kuhusu suala la haki za binadamu Prof. Kabudi amesema taswira inayotolewa kuhusu suala hilo haiakisi hali halisi iliyopo nchini na kwamba Tanzania inaheshimu na kulinda misingi ya haki za binadamu.

Katika tukio jingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amepokea nakala za hati za utambulisho za Balozi Mteule wa Uswis hapa Nchini Mhe. Didier Chassot.
 
Attachments

  • Magufuli overpowerful.docx
    183.2 KB · Views: 4
  • Busu kwa Tundu Lissu.docx
    126 KB · Views: 3
Yani MaCCM nikama wana wagombea wawili wa uraisi kwenye chama chao

Kuna mmoja ana sema maendeleo hayana chama kuwa yeye ni raisi wa woote! na kuna mwingine anasema mkichagua upinzani sahauni, maendeleo hatuleti kama vile MaCCM pekee yao ndio yana lipa kodi.
Mtaumia saana endeleeni kusema tanzania inatazamwa na dunia.
 
Back
Top Bottom