Uchaguzi 2020 Balozi wa Marekani nchini Tanzania: Serikali ihakikishe usalama wa Viongozi wa Upinzani, iwaachie waliokamatwa na kurejesha mawasiliano kwa wananchi

Sovereignty means our country is free from outside forces.

Kiukweli siungi mkono mtu wa nje kujihusisha na maswala ya nchi yetu.

Lakini pia siungi mkono injustice.

Yaani wananchi tunawekwa katikati.
 
Wanawajengea mabarabara manyotamba nayo kwenye kampeni, Ukila vya watu ukishikwa tako tulia ukibisha utatemeshwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Huko kula vya kwao si ndiyo sera yenu nyie jamaa wa Chama cha Demoghasia & Maombolezo. Mnataka kuweka rasilimali za nchi rehani ili tuendelee kuwa ombaomba, wakati ambapo tunaweza kujijengea miradi mikubwa kwa ajili ya maendeleo himilivu yatakayotufanya tujiondoe shingo zetu chini ya magoti ya hao mabeberu wanaotamani kuwa viranja wa dunia.
 
Hatuwezi achilia watu wanaotaka kuharibu amani yetu kisa kauli ya balozi.
Inabidi tu wakubali kuwa tayari wameng'olewa kwenye viti vyao
Na kama walivyokjwa walitoka nje bungeni sasa wapo uraiani hatuhitaji tena drama zao acha wapate wanachostahili.
 
Yaani wewe unafahamu kabisa tatizo lililopo ila bado unajitahid kufumbia macho. Tatizo chama tawala kimewekeza kwenye kuua raia wanaodai haki kihalali mana kisera hawana watakachowaambia wapemba wakaelewa.
wewe ulielewaje mbona uko humu badala ya kuwa sehemu husika
jitazame
 
Sovereignty means our country is free from outside forces.

Kiukweli siungi mkono mtu wa nje kujihusisha na maswala ya nchi yetu.

Lakini pia siungi mkono injustice.

Yaani wananchi tunawekwa katikati.
Yaani kuingiliwa ma nchi nyingine kisiasa haina tofauti na kuvamiwa kivita. Aliyeleta wazo la kufungiwa mtandao wakati wa uchaguzi huu aliona mbali sana. Nyerere aliwahi kusema kila hao jamaa wanapoona nchi imeanza kujinasua kwao, na inasonga mbele kimaendeleo, basi ndipo makalele yao yanazidi kuwa mengi sana. Sasa anahitajika kiongozi madhubuti, anayewachora tu, wala hata hawazi KUGEUKA NYUMA! Dkt. JPM ndiye.
 
Balozi huyo ameandika:

Reports of arrests of opposition leaders are extremely concerning. I urge the Government to ensure the safety and security of all opposition leaders, cease these targeted arrests, release detainees, restore telecommunications, and afford due process under the law to all citizens.

View attachment 1617807

Balozi was Marekani Tanzania ana kazi moja tu,kuhakikisha inatengeneza Instability Tanzania ili waweze kuiba rasilimali za Tanzania.Kampuni zao kama Symbion ambazo zilikua zikiuzia umeme Tanesco kwa bei ya juu sasa hivi chali kutokana na mikataba mibovu ya kinyonyaji.

Marekani inaunga mkono chama chochote duniani kinachokubali na kuunga mkono sera za ushoga,hivyo wapo teari kwa namna yeyote kuhakikisha CHADEMA na ACT vinakua na nguvu

Balozi wa Marekani hana hadhi ya kuamuru wahalifu kuachiwa au mitandao ya kijamii kufungwa au kufunguliwa,Vyombo vya ulinzi Tanzania vinajua nini cha muhimu kwa Watanzania.

Balozi wa Marekani ni miongoni mwa wabaguzi wakubwa wa Watu weusi,chuki yake hii haitaicha salama Tanzania,atahakikisha anasababisha maafa na madhara kwa watoto na kina mama
 
Hivi

Huyu baba hanaga kazi zingine? Kwa Kenya huwaga aanaside na serikali kukandamiza wapinzani kwa Tanzania wanaside na wapinzani dhidi ya serikali. Wamerekani wanafiki sana jamani
Ameketi tu huko anapost habari za nchi nyingine
 
una muda mrefu sana jf lakini una fikra finyu sana !

Kabisa. Absolutely. Ndio maana nasema kuna keyboard warriors. Tunadanyana sana. Muda ni mwalimu mzuri.
CDM, nani kawadanganya mabadiliko yataletwa na hao wazungu mnafikiri wako kwenye perfect world?
Why don't you work on something that is local, and yet address true needs of people? Mkishaanzq kubebana nao, hapo hapo mshapoteza. Baadae mnaona mmedhuliumiwa
 
Hivi

Huyu baba hanaga kazi zingine? Kwa Kenya huwaga aanaside na serikali kukandamiza wapinzani kwa Tanzania wanaside na wapinzani dhidi ya serikali. Wamerekani wanafiki sana jamani
kwao kwenyewe wanaua watu kama sisi kama kuku alafu anakuja kuongea urojo huo
 
Tuseme ukweli tu SERIKALI YA TANZANIA awamu ya tano ni Serikali dhalimu sana. Yani huwezi kutofautisha Tanzania na Burundi au Rwanda kwa sasa. Tanzania ni nchi iliyojijengea heshima kubwa kidemokrasia Leo hii tumekuwa kituko.

Swali unalotakiwa kujiuliza, je wanayoyasema marekani ni ya kweli au wanamsingizia MAGUFULI???

Mitandao imezimwa au haijazimwa??? Kura zimeibiwa au hazijaibiwa??

UCHAGUZI ulikuwa huru au uhuni tu??

Je magufuli asingefanya dhulma ya yote haya Marekani wangemsema vibaya? ?

Tatizo ni MAGUFULI...ni MAGUFULI tu
Ungekuwa US ukaona madudu yao, kamwe usingesema lolote. Hao jamaa wana "double-standard" asikwambie mtu. Urafiki wao hudumu kwa yule anayekubali kukamuliwa huku akiwachekea. JPM kwao ni never. Nampenda Rais asiyekubali kukoromewa na kupangiwa la kufanya na watu kama hao ambao Rais wao mwenyewe alishapa kwamba Afrika tungepaswa kuendelea kuwa makoloni kwa kipindi kingine cha miaka 100.
 
Back
Top Bottom