Balozi wa Marekani akwama kwenye lifti - NI KATIKA JENGO LA WIZARA YA NISHATI NA MADINI, WAZIRI AM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balozi wa Marekani akwama kwenye lifti - NI KATIKA JENGO LA WIZARA YA NISHATI NA MADINI, WAZIRI AM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 17, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 16 May 2012 23:10[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][​IMG]

  Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt (nyuma) akiwa amekwama kwenye lifti ya jengo la Wizara ya Nishati na Madini, jijini Dar es Salaam jana, alipokwenda kumtembelea Waziri wa wizara hiyo, Prof Sospeter Muhongo. Picha ndogo watu waliokuwemo kwenye lifti hiyo wakijalibu kufungua kwa mkono baada ya kukwama. Picha na Michael Jamson

  NI KATIKA JENGO LA WIZARA YA NISHATI NA MADINI, WAZIRI AMWOMBA RADHI


  James Magai

  BALOZI wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt jana alikwama ndani ya lifti katika Jengo la Wizara ya Nishati na Madini, Dar es Salaam kwa takriban dakika 20.

  Balozi Lenhardt akiwa na ujumbe wake wa watu wawili, walikumbwa na mkasa huo mchana wakati wakienda kukutana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. Mbali na Balozi Lenhardt na ujumbe wake, pia kulikuwamo na watu wengine wakiwemo maofisa wa wizara hiyo na kufanya jumla ya watu saba kukwama kwenye lifti hiyo.

  Saa 7:58 mchana mwandishi wetu alipofika wizarani hapo, alimkuta balozi huyo na wenzake hao wakiwa wamekwama ndani ya lifti hiyo katika ghorofa ya kwanza huku ofisa wa mapokezi wizarani hapo akihangaika kufanya mawasiliano na mafundi.

  Mmoja wa wafanyakazi wa wizara hiyo alifanikiwa kuifungua na kuacha uwazi wa kama sentimita 10 na kisha kuweka kibao ambacho kiliifanya iwe wazi lakini bila ya kuwawezesha waliokuwamo ndani kutoka.

  Hatua hiyo iliwawezesha Balozi huyo na wenzake walau kupata hewa wakati wakisubiri hatua zaidi za kuwakwamua. walibaki humo hadi ilipotimu saa 8:14 mchana walipokwamuliwa baada ya mafundi waliokuwa wamefika muda mfupi kabla, kufanikiwa kuifungua.

  Kutokana na tukio hilo, mkutano wa Balozi huyo na Waziri Profesa Muhongo uliokuwa umepangwa kuanza saa 8:00 ulichelewa kwa zaidi ya nusu saa kusubiri wageni hao wakwamuliwe. Ingawa hakuna ofisa wa wizara hiyo aliyekuwa tayari kuzungumzia mkasa huo wa kukwama kwa lifti hiyo, ilielezwa kwamba tatizo hilo limetokana na lifti hiyo kuwa mbovu.

  Mmoja wa wafanyakazi wa wizara hiyo ambaye hata hivyo, jina lake halikuweza kupatikana mara moja alisikika akisema kuwa lifti hiyo ina kawaida ya kukwama.

  Baada ya kufanikiwa kutoka, Balozi huyo na maofisa aliokuwa ameambatana nao pamoja na maofisa wengine wa wizara waliingia katika chumba cha mkutano na kuendelea na mazungumzo.
  Hata hivyo, kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo, Waziri Profesa Muhongo alimtaka radhi Balozi Lenhardt na ujumbe wake kwa tukio hilo lakini akamtania kuwa bila shaka amepata uzoefu wa tatizo la nishati nchini, maelezo ambayo Balozi huyo aliyeitikia huku akicheka.

  Ziara ya Balozi Lenhardt na ujumbe wake wizarani hapo ilikuwa na lengo la kumpongeza Profesa Muhongo kwa kuteuliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo na kuangalia jinsi ambavyo Marekani itaendelea kuisaidia Tanzania kuboresha sekta hiyo.

  Katika mazungumzo hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Manaibu Waziri wa wizara hiyo, George Simbachawene na Stephen Maselle na maofisa wengine wa wizara, yalijikita zaidi katika sekta ya Nishati.

  Waziri Profesa Muhongo alimweleza balozi huyo umuhimu wa nishati katika maendeleo ya taifa na changamoto ambazo zinaikabili sekta hiyo, kiasi cha kufanya kutokuwa na uhakika wa upatikanaji wake.

  Pia Profesa Muhongo alimweleza balozi huyo hatua na mikakati ambayo Serikali kupitia wizara yake imekuwa ikiichukua na inayotarajia kuichukua kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa nishati ya kutosha na ya uhakika.

  "Kipaumbele cha wizara kwa sasa ni kupata umeme uhakika wa bei nafuu na unaotabirika. Ni muhimu kuongeza watumiaji wa umeme kwa kuwa kwa sasa kwa takwimu za Tanesco (Shirika la Umeme Tanzania), ni asilimia 18.4 tu ya Watanzania wanaopata huduma ya umeme," alisema.

  Katika kuongeza watumiaji wa umeme, Profesa Muhongo alisisitiza kupunguza gharama za upatikanaji wa umeme majumbani, mashambani na viwandani.

  Alisema lengo la kuweka msisitizo katika nishati ni kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs), ili kufikia mwaka 2025 iwe ni nchi ambayo wananchi wake wanapata kipato cha kati... "Ili kufikia hilo lazima tupate umeme wa kutosha wa uhakika na wa bei rahisi."

  Akizungumzia umuhimu wa nishati katika kutengeneza ajira na kuinua uchumi, Profesa Muhongo alisema ni lazima kuinua na kuboresha sekta ya kilimo kwa kuwa ndiyo itakayoweza kuondoa tatizo hilo."Lakini, inahitaji nishati. Sisi tunatengeneza mambo yetu sawasawa ili kusaidia sekta ya kilimo ikue na itoe ajira na chakula cha kutosha na hivyo kupunguza mfumuko wa bei. Dawa ya mfumuko wa bei ni umeme, kama haupatikani ni vigumu kuupunguza," alisema.

  Balozi Lenhardt kwa upande wake, alisema Marekani iko tayari kushirikiana na Tanzania kutatua tatizo la nishati nchini.Alimkabidhi Profesa Muhongo mpango mkakati wa namna ya kushirikiana katika kukabiliana na tatizo hilo, ambao umeandaliwa na wataalamu wa Tanzania na Marekani.


  Baada ya mazungumzo hayo, Profesa Muhongo alisema wizara kwa upande wake itakaa na kuandaa dokezo ambalo litatumika kuangalia namna ya kuanza na kutekeleza mpango huo.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]  [​IMG]

  New Energy and Minerals Minister, Professor Sospeter Muhongo

  [h=3]

  At least 30 per cent of the country's over 44 million people should access reliable and affordable power supply by 2015, new Energy and Minerals Minister, Professor Sospeter Muhongo has said.
  [/h]
  Prof Muhongo said while meeting United States Ambassador to
  Tanzania and East African Community, Alfonso Lenhardt that according to Tanzania Electric Supply Company Limited, 18.4 per cent of the population has access to electricity. "We are targeting to have 30 per cent of the population getting electricity in the next two years but how will that be done, it remains a miracle," Prof Muhongo said as Ambassador Lenhardt pledged US support to help the country end its energy problems.

  Prof Muhongo who was appointed to the energy and minerals ministry last week, has raised a lot of expectations in the public because of his unique qualifications and experience as geologist who has served African energy and minerals sectors. Defining his strategy in ensuring that his ambition of supplying 30 per cent of the population is realized by 2015, the minister said he will work closely with Tanesco,
  Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) and National Development Corporation (NDC).

  "I want to bring together all the key players under the ministry instead of working as fragmented institutions as is the case now," Prof. Muhongo said. The former Executive Director of the International Council for Science (ICSU)-Africa Region who was based in South Africa, said he has worked with other African experts of how to harness the continent's energy sector and pledged to work closely with the US government to tap natural gas, coal and hydro-electric power sources.

  "We hope to work with you Mr Ambassador in making sure that our goal of enabling more people to access electricity is realized," he stressed noting that through public private partnership, targets are likely to be met. Briefing the minister of progress made so far by the US and Tanzania in joint energy under Millennium Challenge Account (MCA), Ambassador Lenhardt urged the new minister to endorse a Joint Country Action Plan (JCAP).

  "Let's get on now, let's start working. JCAP is a working document," Ambassador Lenhardt argued saying American energy companies and President Barack Obama's administration are ready to start implementing the plan. He said the US is ready to bring technical and financial support to implement the JCAP which is a vital document defining how private companies can work with government in delivering reliable and affordable energy.

  "Let's work together in the interest of Tanzania and do something with JCAP," the US envoy stressed saying
  Dar es Salaam is among four countries which Washington is supporting under Partnership for Growth which also includes Ghana, El Salvador and Philippines.

  By FINNIGAN WA SIMBEYE, Tanzania Daily News
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Aibu, Labda ni Mweusi tunaona Uafadhali? Tunafisadi kila kitu tunasahau kuboresha mbinu zetu za kazi
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,471
  Trophy Points: 280
  ............................................lift mbovu?kwani kununua lift mpya ni kiasi gani?
  View attachment 54115
   
 4. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  nimi nilishagive up na nchi yenyewe zamani gani
   
 5. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,060
  Likes Received: 1,099
  Trophy Points: 280
  Nani kakudangaya kuwa tunafanana eti kwakuwa mweusi, huyu hafanani na sisi hata kidogo sana sana anashangaa jinsi miafrika tulivyo.
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,292
  Likes Received: 22,062
  Trophy Points: 280
  Kwa hali hii kweli tunaweza kuuima ule wimbo "CHAMA CHETU CHA MAPINDUZI CHAJENGA NCHI"?
   
 7. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,358
  Trophy Points: 280
  alikuwa anaenda kumsainisha waziri mpya mkataba wa kimangungo shetani kamuumbua,.
   
 8. k

  kijereshi JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  wamarekani washaingia songea nyumbi hii bombi hii na ardhi wamepewa ya kutosha tayari kuanza kutifua ardhi yetu kuvuna madini ya urania(uranium) na ndio siri ya safari za mkuu wa kaya huko kwa obama kwakweli nchi yetu itaendelea kuliwa vizaz vijavyo vitakuja shangaa sna jinsi ardhi yetu tunavyoimilikisha kwa wageni,kwakweli wazawa wengi wamenyang'anywa ardhi waliyokuwa wakiimiliki kwa minajili ya kupimiwa na kupatiwa sehemu kdgo inasikitisha kwakweli
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  Huyu mwanajeshi lazima ametumwa kwa ajenda maalumu...mtakuja kugundua baada ya miaka mingi inayokuja. Hawalali hawa mpaka watutawale na kuchukua kila tulichonacho
   
 10. b

  bibi.com JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 1,155
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  kama tuna akili basi tukatae akili, tunajitaji wanaume na wanawake wa haja wanaojua kusimamia maamuzi yao na kupigania nchi yao.
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ingekuwa zama zile wazee wangetupa tafsiri apa kwa nini lift imkwamie yeye na wakati huo uku akiwai appointment
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  Akili tunazo. Tatizo njaa imeingia sana mjini
   
Loading...