Uchaguzi 2020 Balozi wa Marekani ahudhuria hafla ya kumuapisha Rais Magufuli Dodoma, asema ni ishara kuwa uhusiano wa muda mrefu kati ya nchi mbili hautetereki

Labda tujipange kudai Tume Huru lakini sio kushiriki chaguzi tena chini ya hii tume.
Kwa haya yaliyoyokea Katika uchunguzi huu,vyama vya siasa vya upinzani visiingie kwenye uchunguzi mpaka ipatikane tume huru ya uchunguzi

Usalama wa Taifa na vyombo vya dola visiingilie uchanguzi, Watanzania wawe huru kuchagua wanae mtaka
 
Bado hauelewi tu? Serikali ya USA haiwezi kuhudhuria kuapishwa kwa Raisi isiyemtambua, ipi ngumu kwako kuelewa? Kitendo cha USA kuhudhuria maana yake Uongozi ulioapishwa una baraka zote za USA, sasa hayo mengine yanajadilika ndiyo maana yake, mnaweza mkajadili kuhusu demokrasia na mengineyo lkn Raisi wa JMTZ kwa sasa anatambulika kama Pombe Magufuli (PhD), ...

Na hapo ndio utaona tofauti kati ya "diplomat" na "kada"! Kama machinery yao haijakamilisha kuichimbua scenario nzima ya uchaguzi Tz kutokushiriki kwake ingeleta tafsiri kuwa tayari wamemaliza uchunguzi wao na tayari wamefikia uamuzi wa kutounga mkono matokea ya uchaguzi. Akijua pia kwamba ushiriki wake ungetafsiriwa na nyie makada kuwa anaunga mkono juhudi ndio maana akaweka hilo short & clear kwenye huo ujumbe wake.
 
CDM bwana mafisadi wakiwa kwao wanawabadilisha jina, anakuwa mbeba-maono (Mr PM Mstaafu), hiki chama kina watu wanaobadilika-badilika sana kuliko kasi ya mmeto wa indiketa. Nani atawaamini basi???
Hicho ndio kilifanya nisimpe kura Lissu sasa aende the Hague alipokuwa anatishia
 
Balozi yuko sahihi asilimia 100,,maana amegundua watanzania ni mandumilakuwili tuliambiwa tuandamane kudai haki hakuna hata mmoja aliyesogeza pua yake barabarani sasa unadhani atafanya nini na kaona sisi majuha.Pia balozi yuko pale kwa maslahi ya nchi yake na sio yetu.
 
CCM wameonesha dharau kubwa sana kwa mabeberu, yaani licha ya matamko na vitisho kabla ya uchaguzi bado ccm walipuuza na kufanya wayatakayo kwenye uchaguzi
 
Labda tujipange kudai Tume Huru lakini sio kushiriki chaguzi tena chini ya hii tume.
Kila mara huwa najiuliza upinzani hasahasa seif ana akili kweli kila mwaka unashindwa hutangazwi na msimu mwingine unadai utashinda na utatangazwa. Kwa katiba na tume ipi?

Guys you should change your way of approaching elections to win credibility
 
Ofcourse anaewaamini CHADEMA and the likes must have undergone mental erosion. Their claims are vested on half truths and lies. I wonder how they have managed to drag the US into their dirty games
Wasiokuwa na hoja zenye ukweli hupenda kuchandanya kiswahili na kiingereza ili waonekane ni wasomi wabobezi, wewe ni mmoja wapo.
 
Kaangalie na comments kwa Hussein Bashe baada ya ku-tweet: "mitano tena kwa Magufuli".

Mkuu kule tweeter wamejaa vibaraka na mabwana zao, hakuna wapiga kura wa Tanzania kule na kama wapi hawafiki 1%
Ukitaka kujua hali ya siasa za nchi hii kupitia tweeter utaishia alipoishia Tundu
 
Watanzania tujue kuwa msimamo wa balozi binafsi si msimamo wa nchi hivyo anawajibika kuiwakilisha nchi mpaka pale itakapotoa msimamo.
 
Kaangalie na comments kwa Hussein Bashe baada ya ku-tweet: "mitano tena kwa Magufuli".
kwani nyie mitandaoni si ndipo kwenye kura zenu huko?
jadili kauli ya balozi aliotoa live,utaona kabisa kwamba kelele zenu ni sawa na kelele za mlango hazituzuii kulala
 
Lazima diplomasia iendelee. Na uhusiano wa Marekani na Tanzania hakuujenga Magufuli. Hivo kwa lugha nyepesi mahisiano na Watanzania yataendelea lakini kina makonda bado hawapati visa na list itaingezeka soon
 
Uchaguzi umeshaisha sasa tujikite kwenye kujenga uchumi wa nchi, baada ya miaka mitano tukutane tena hapa.

Uchaguzi umeisha sasa tuijenge nchi

CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Sasa ukimfutia JPM vibali vya USA utakua umemkomoa au umempa sababu ya kukaa chato kwa amani na furaha
 
Back
Top Bottom