Balozi wa Kenya aishambulia Russia kwa kuyatambua kama majimbo huru ya Ukraine

Reports: The Armed Forces of #Ukraine surrendered Starobelsk and Severodonetsk without a fight
 
Upumbavu wa mwafrika(mtanganyika) wa kujidharau na kutojitambua ndio huu hapa, ukijidhihirisha wazi. Uzi ni kuhusu mada nyeti, tena ya kimataifa. Ila umejazwa mipasho chungu nzima, utadhani ni wimbo wa taarabu. Kwamba ukiwa mwafrika huruhusiwi kuwa na maoni, kuhusu suala lolote lile la kimataifa?

Wachechnya na wa-Afghani licha ya kudharauliwa walimshinda kwenye vita Mrusi huyu huyu, mnayemsifia kama James Bond. Jinamizi la mkoloni ambaye alijisifia na kujiita The Great British Empire lilifurushwa nchini Kenya na wapiganaji wa Mau Mau. Wakitumia silaha za kujitengenezea, kwenye maficho yao misituni. Labda hilo ndio chanzo cha tofauti za kimitizamo kati yetu sisi majirani, Kenya na Tz. Kwamba sisi tuna historia ya kumwaga damu, tukipambana kivita dhidi ya 'bullies', kama wanavoitwa kwa kimombo.

Hakuna jambo hata moja ambalo linahalalisha uvamizi wa Mrusi nchini Ukraine na Kenya sasa hivi ndio muakilishi wa bara la Afrika, kwenye kamati ya usalama ya Umoja wa Mataifa. Balozi Martin Kimani yupo sahihi kabisa, kwenye matamshi yake dhidi ya Urusi. Tena amedhihirisha wazi kwamba ana uwezo wa kutekeleza majukumu yake. Ambayo ndio sababu kuu ya uwepo wake jijini New York.
 
Tunaomba balozi kimathi azungumzie suala la Ethiopia , DRC na Somalia kwa waafrika wenzetu tunamuona amefanya poa sana
 
Anatetea maslah ya mabeberu
Jombaa, unaanzisha uzi kiushabik kuhusu hotuba ambayo hujaisikiza? Mbona kwenye hotuba yake hiyo balozi Kimani aliwaponda kweli kweli hao mabeberu kwa ukoloni wao barani Afrika? Tatizo ni nini, lugha gongana au ni uelewa finyu tu kama kawa?
 
Jombaa, unaanzisha uzi kiushabik kuhusu hotuba ambayo hujaisikiza? Mbona kwenye hotuba yake hiyo balozi Kimani amewaponda kweli kweli hao mabeberu kwa ukoloni wao barani Afrika? Tatizo ni nini, lugha gongana au ni uelewa finyu kama kawa?
Weka hiyo hotuba hapa tuione mkuu
 
Back
Top Bottom