Balozi wa Iran nchini Tanzania amevitaka vyombo ya habari kuacha kutegemea habari za vyombo vya Magharibi

Unawaponda lkn kisiri siri unakwenda kuwapigia magoti wakusaidie ela za kujengea mashule
Sisi waafrika tunapenda sifa za kijinga,ndiyo maana ukisikia Rais sijui wa USA,Russia au kwingineko Kasifia nchi au kiongozi fulani tunashangilia Kama mazuzu.......Western media hazitangazi taarifa nzuri za Africa,zile mbayambaya tu ndiyo utazisikia.

Mfano Hispania kuna ukabila ila watatumia neno zurizuri ila ingekuwa Africa headline ingekuwa tofauti.

In God we Trust
 
Sisi waafrika tunapenda sifa za kijinga,ndiyo maana ukisikia Rais sijui wa USA,Russia au kwingineko Kasifia nchi au kiongozi fulani tunashangilia Kama mazuzu.......Western media hazitangazi taarifa nzuri za Africa,zile mbayambaya tu ndiyo utazisikia.

Mfano Hispania kuna ukabila ila watatumia neno zurizuri ila ingekuwa Africa headline ingekuwa tofauti.
Vyombo vya habari vya Iran havijui hata Tanzania ni mdudu gani? Si bora wanaoandika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mousa Farhang, kwa vyombo vya habari nchini amevitaka kuacha kutegemea habari za vyombo vya magharibi kwa kuwa havina maslahi kwa nchi za Afrika na zile zinazoendelea, vimekuwa vikiandika mambo mabaya kwa nchi hizo kwa maslahi yao binafsi. "Kwa mfano unaweza kuwa humpendi Rais

Magufuli na si nchi kwa ujumla lakini inakuwaje uadui wako na Magufuli ukawa ni uadui wako na Tanzania nzima? Hili si sahihi na vyombo vya habari vinapaswa kuwa makini”.View attachment 1360807



Huyu balozi wa Iran na wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania inayoongozwa na Mh. Palamagamba Kabudi ktk serikali ya CCM Mpya chini ya Mh. Rais John Pombe Joseph Magufuli wasikilize maneno ya Baba wa Taifa aliyoongea miaka hiyo iliyopita juu ya Tanzania iwe nchi isiyofungamana na upande wowote ili isije ingizwa ktk migogoro inayozihusu Mataifa makubwa.

Maana tumeanza kusikia kauli 'wale mabeberu' , ' vita vya kiuchumi'..... Mwalimu Nyerere alisema wanakaribisha 'wadau wa maendeleo ' lakini wasituingize kujenga 'uchama' na mrengo wa kuegamia upande wowote au kutuingiza ktk migogoro isiyotuhusu na mataifa makubwa maana dunia itatuona wendawazimu kujaribu kutunisha misuli kukubaliana na mataifa makubwa kuifurahisha kinchi kitukutu...

Source: AfroMarxtist
 
Rejea pia aliyoyasema balozi wa Iran nchini Tanzania siku ya February 9, 2019

Balozi wa Iran : "waTanzania Msikubali nchi za madola ya nje kuingilia siasa za ndani ya nchi yenu"
.


Hiyo ilikuwa siku ya maadhimisho ya miaka 40 ya Mapinduzi ya Iran, ambapo alitoa muhadhara ktk Chuo cha Diplomasia kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam, Tanzania
Source: Baqir Media
 
February 7, 2019

Balozi Mousa Farhang wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran azungumzia Vinu vya nuklia

Balozi wa Iran azungumzia 'choyo' na 'uzadiki' wa mabeberu kuhusu matumizi ya kiraia ya Vinu vya nuklia nchini Iran. Balozi amesema, Nchi za Magharibi hazitaki kuona Iran iweza kumudu matumizi ya kiatomiki , ikifaidika na utaalamu wa kiNyuklia kiraia na kisha Iran kuifundisha Tanzania namna ya kunufaika na matumizi ya kiraia ya nguvu za atomiki .

 
Back
Top Bottom