Balozi urusi anusurika kuangukiwa na ukuta wa nyumba .

chakubimbi

Member
Nov 25, 2010
21
1
Balozi Jaka Mwambi wa nchini Urusi alinusurika kuangukiwa na paa la nyumba ya ubalozi. Inasikitisha sana ukiona jinsi ubalozi wetu ulivyo kwani umechoka sana na ajabu ripoti ya mkaguzi mkuu (CAG) ilibaini kua kuna ubadhirifu mkubwa kwenye ubalozi huo zaidi ya Tsh 440 milion hazijulikani zilipo. Chakujiuliza ni ubalozi unakosa hata fungu la kufanya matengenezo ?
 
Nchii wajanja wanaila kweli. Wengine wakidai haki zao wanazimwa kama mishumaa. Nafikiri kama wazimaji wangekuwa wanawashughulikia hawa watafuna mali ya umma mbona tungewaelewa na kuwaona mashujaa. Bahati mbaya wao wakila hilo halihatarishi uwepo wa taifa letu ila wengine mkijaribu hata kuuliza ni mabwepande
 
Kumtukana Mzee Mwambi hapa kutokana na Ubovu na Uchakafu wa Ubalozi wetu Moscow (Pyatnyinskaya) ni uonevu.Ubalozi huo ni Mchakavu na unahitaji matengenezo ya kudumu toka enzi za Mzee Tibaijuka (Marehemu ) akiwa Balozi.Sina uhakika kama Ubalozi huo ni Jengo letu au bado tumepangisha kama ilivyokuwa awali.Ubalozi hauna hadhi,na upo mtaani kabisa,wala sidhani kama kuna Ubalozi mwingine wowote eneo hilo.
 
samahani, unamaaanisha nyumba ipi? ya urusi alipo au anayoishi hapa tz?
 
Kumtukana Mzee Mwambi hapa kutokana na Ubovu na Uchakafu wa Ubalozi wetu Moscow (Pyatnyinskaya) ni uonevu.Ubalozi huo ni Mchakavu na unahitaji matengenezo ya kudumu toka enzi za Mzee Tibaijuka (Marehemu ) akiwa Balozi.Sina uhakika kama Ubalozi huo ni Jengo letu au bado tumepangisha kama ilivyokuwa awali.Ubalozi hauna hadhi,na upo mtaani kabisa,wala sidhani kama kuna Ubalozi mwingine wowote eneo hilo.

Mwizi yeyote hawezi kupewa heshima ya "UZEE". Taarifa ya CAG inaweka wazi kuwa Millioni 440 zimepotea kule ubalozini Moscow na hakuna maelezo!! Sasa kwanini huyu mwambi asifunguliwe mashtaka kama Mahalu? Nyumba ya ubalozi inaporomoka huku wezi hawa wanakomba fedha za walipa kodi!!
 
Nchii wajanja wanaila kweli. Wengine wakidai haki zao wanazimwa kama mishumaa. Nafikiri kama wazimaji wangekuwa wanawashughulikia hawa watafuna mali ya umma mbona tungewaelewa na kuwaona mashujaa. Bahati mbaya wao wakila hilo halihatarishi uwepo wa taifa letu ila wengine mkijaribu hata kuuliza ni mabwepande

Hivi na wewe aliyekupa huo u premium member alikufanyia usaili? Tangu lini mwizi akaitwa MJANJA. Acheni upotoshaji bana
 
Kumtukana Mzee Mwambi hapa kutokana na Ubovu na Uchakafu wa Ubalozi wetu Moscow (Pyatnyinskaya) ni uonevu.Ubalozi huo ni Mchakavu na unahitaji matengenezo ya kudumu toka enzi za Mzee Tibaijuka (Marehemu ) akiwa Balozi.Sina uhakika kama Ubalozi huo ni Jengo letu au bado tumepangisha kama ilivyokuwa awali.Ubalozi hauna hadhi,na upo mtaani kabisa,wala sidhani kama kuna Ubalozi mwingine wowote eneo hilo.

Mkuu Pyatnitsakaya street ipo takribani 1.7 Km toka Red square (City Center) na kuna balozi nyingi tu eneo la karibu pale.
 
Nyumba ya ubalozi iliyo urusi ndio ilifumuka paa,yani ilikua kama bahati tulikua tumpoteze, Ilibidi aweke sherehe ndogo ya kumshukuru Mungu kwa kumponya....
 
Aibu sana ila ndio serikali tunayoitaka ya maneno mengi na uongo kibao...kila kitu kudanganya tu!
 
Hivi na wewe aliyekupa huo u premium member alikufanyia usaili? Tangu lini mwizi akaitwa MJANJA. Acheni upotoshaji bana

Wezi wa Tanzania wanajiita wajanja...si mimi nimewapa jina hilo. Kwenye nyimbo za bendi zetu wengine wanapewa beti maalumu. Bahati mbaya sio wewe unayegawa nani apate nini so mimi kuwa premium member is non of your business. Wewe jadili hoja tu.
 
wezi wa tanzania wanajiita wajanja...si mimi nimewapa jina hilo. Kwenye nyimbo za bendi zetu wengine wanapewa beti maalumu. Bahati mbaya sio wewe unayegawa nani apate nini so mimi kuwa premium member is non of your business. Wewe jadili hoja tu.
upotoshaji mkubwa huu wa jamii...msimsingizie mzee wa watu kuwa kajichotoea pesa wakati yeye kapelekwa urusi hizo pesa zishapotea, wakati mwengine mukiandika vitu lazima muwe muna uhakika navyo.
 
Kama walipata fedha wakatumia kwa matumizi mabovu na ukuta wanauona umechakaa walitegemea nini?
 
upotoshaji mkubwa huu wa jamii...msimsingizie mzee wa watu kuwa kajichotoea pesa wakati yeye kapelekwa urusi hizo pesa zishapotea, wakati mwengine mukiandika vitu lazima muwe muna uhakika navyo.

nani kasema mzee wako ndio amekula hizo pesa? Mbona tunapenda kukwepa dhana nzima ya uwajibikaji? hizo hela zinazoibwa anaiba nani maana kila mtu mzee wake hahusiki? Issue sio huyo mzee...issue ni wizi wa mali ya watanzania unaofanywa na watumishi wa umma. Kama yeye kaiba au hajaiba, mi sijui hilo ila yeye sasa hivi ndio balozi na anatakiwa awe na maelezo ya nini hasa kimetokea
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom