Balozi Uingereza amfunda JK

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,004
Balozi Uingereza amfunda JK
Mwandishi Wetu
Daily News; Monday,June 09, 2008 @08:33

BALOZI wa Uingereza nchini Philip Parham, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kutoogopa kuchunguza na kuwashitaki viongozi waovu bila kujali umaarufu wao.

Parham alisema kitu cha msingi ni kuangalia endapo ushahidi na maslahi ya umma yanahitaji afanye hivyo; bila kujali kuwa watuhumiwa ni watu mashuhuri kiasi gani.

“Usiogope kuchukua uamuzi unaoweza uonekane wa hatari wakati tayari maamuzi hayo yamekwisha kuhalalishwa na viashiria vya faida yake,” alisema Parham katika maadhimisho ya miaka 82 ya kuzaliwa Malkia Elizabeth II, yaliyofanyika Dar es Salaam juzi.

Lakini pia amemtaka asiogope kuung’oa uzembe na udanganyifu. “Lakini pia usiogope kuwaamini marafiki zao kama wanastahili uwapo uaminifu huo...usiogope kuendeleza na kuhamasisha ufanisi pamoja na uadilifu,” alisema katika hotuba yake.

Balozi huyo alitaka pia Rais asiogope kukabiliana na watu wenye maslahi binafsi ambao wanajaribu kuzuia maendeleo kwa sababu zao za kichoyo.

Pia amewataka viongozi kutoogopa kuachia ngazi au wadhifa pale ambapo kazi fulani yaweza kufanywa vizuri na wengine.

Akizungumzia uchumi wa Tanzania, balozi huyo alisema bajeti ya mwaka uliopita ilikuwa takriban dola bilioni 5, kiasi ambacho Waingereza wanakitumia katika kununua mikanda ya DVD kwa mwaka.

“Hii pia ni sawa na asilimia 2.5 tu ya bajeti ya Afya ya Uingereza kiasi hicho ni sawa kabisa na robo ya fedha ambayo wacheza kamari Uingereza wanakipoteza kwa mwaka na kwamba kiasi hicho ni sawa na thamani ya chakula kinachotupwa kama mbaki nchini mwake.

“Hiki kiwango halisi cha fedha ambacho Serikali ya Tanzania inacho ili kuweza kuwapatia wananchi wake huduma ya elimu, afya, miundombinu pamoja na ulinzi kwa wananchi milioni 40 waishio nchini ambayo ni kubwa zaidi ya mara nne kwa Uingereza,” alisema.

Alisema kuna nuru katika hali ya baadaye ya Tanzania. “Ikiwa katika hali ya utulivu, mshikamano wa jamii, demokrasia hai, uchumi mzuri, fursa kubwa ya kiuchumi ambazo hazijatumika kikamilifu, Rais mwenye uwezo na utashi kutoka Jumuiya ya Kimataifa ina nafasi kubwa ya kubadilika,” alisema.

Balozi alisisitiza kuwa Tanzania si nchi masikini na wananchi wake hawapaswi kuwa masikini.

Alisema matumaini ambayo ameyaona katika baadhi ya mikoa bila kusahau katika macho ya watoto wa Kituo cha Dogodogo cha Dar es Salaam na hakika matumaini hayo yasivunjwe moyo na akasisitiza kuwa yanawezekana tu iwapo kila mtu atatimiza wajibu wake.

Balozi huyo aliwataka Watanzania wasiogope kusema ukweli juu ya dola hasa pale dola inapotishia ustawi wa heshima ya binadamu na utulivu katika ukanda huu.

Lakini pia alitaka Watanzania wasiogope kubadili fikra zao pamoja na sera endapo itajidhihirisha wazi kwamba uelekeo mpya ni sahihi. Pia wasiogope kuipatia sekta binafsi fursa, uhuru pamoja na kujiamini katika kuongeza nafasi ajira, tija na ukuaji wa uchumi.
 
Sawa Kabisa Umenena, Nilisema Week Iliyopita, Kwamba, Budget Ya Trillion 7.2 Or Usd7 Billion, Ni Sawa Nusu Na Misharahara Ya Kampuni Kama Walmart/ Ge/ Siemens/ General Motors/ Bp Nk. Hicho Kiasi Ni Sawa Na Budget Ya Chuo Kikuu Cha Harvad Pekee Au Colombia/ Yale/ Texas N.k Ni Sawa Na Faida Ya Vikampuni Vidogo Vidogo Sana Hapa Marekani. Hii Yote Ni Kwa Sababu Ya Upumbavu Wa Viongozi Wetu Wamezoea Omba Omba, Kama Tanzania Wangejenga Kiwanda Cha Kuasemble Tractor Cha Kuzalisha Tractor 500,000 Kwa Mwaka Kiwanda Cha Mbolea Kwa $300,000,000 Cha Kuzalisha Tone Million 500 Kwa Mwaka Ambavyo Vyote Vyaweza Ghalimu $1 Billion Kwa Serikali Uchumui Ungekuwa Sana. Madini/ Samaki/ Maziwa/utalii Na Mambo Mengine: Kweli Viongozi Wetu Are Very Stupid. Balozi Wa Uk Amesema Ukweli Sana.

huyo Mukulo(Waziri wa Fedha) kasoma hapa hapa Marekani kwenye vyuo vya ubabaishaji ( Degree Mill) ndo madhaha yake hayo kama angesoma vyuo ambavyo ni vizuri kama state universities na kufanya kazi kidogo hapa asingetoa budget ya kipumbavu namna hile.
 
At least amesema. Ila tu wasije kumuona anageuka kibaraka. Maana hayo ndiyo mambo ya wanaCCM, hawataki kukosolewa. Keshokesho tu utasikia kisha pigwa chini!!!! Lakini hizo comparison zinanitia wazimu wakati JK atakuambia mambo yako poa na uchumi unakua!!!!!
 
Mkullo pamoja na kutojua anajua fika kwamba bajeti mawaziri wataingia Mikoanio kuiptisha kwa wananchi kwa style yao mpya .So no worries wadanganyika wamelala
 
Hawa ndio kati ya wale mheshimiwa raisi wetu aliowaita "wakubwa". Labda pengine atayazingatia mawaidha ya huyu "mkubwa".
 
Balozi Uingereza amfunda JK
Mwandishi Wetu
Daily News; Monday,June 09, 2008 @08:33


Balozi huyo alitaka pia Rais asiogope kukabiliana na watu wenye maslahi binafsi ambao wanajaribu kuzuia maendeleo kwa sababu zao za kichoyo.

.

Hapo nampigia makofi huyu balozi maana hilo ni tatizo kubwa kwa TZ. Tena sio tu kwa viongozi wa serikali bali kwa middle class nzima ya TZ.

Kuna watu wengi TZ wanafurahia kuishi na maskini jirani, eti raha uwe na pesa kwenye maskini na kuabudiwa kama miungu watu.

Bila kuondoa huo ujuha, itatuchukua miaka mingi sana kupata maendeleo ya kweli kwa wananchi wote.

Binafsi naamini ni bora kuwa mtu wa kawaida kwenye kundi la matajiri, kuliko tajiri kwenye umaskini wa kutisha.
 
maslahi binafsi yapi? yaani kikwete asiogope kumpeleka rostam segerea? kwa nini asiogope? kuna mtu anayeweza kushau mkono wake wa kulia? the very very hand that feed him? acheni muchezooooooo
 
huyo Mukulo(Waziri wa Fedha) kasoma hapa hapa Marekani kwenye vyuo vya ubabaishaji ( Degree Mill) ndo madhaha yake hayo kama angesoma vyuo ambavyo ni vizuri kama state universities na kufanya kazi kidogo hapa asingetoa budget ya kipumbavu namna hile.

Chenge ni product ya Harvard.....Waafrika ndivyo tulivo

Hawa ndio kati ya wale mheshimiwa raisi wetu aliowaita "wakubwa". Labda pengine atayazingatia mawaidha ya huyu "mkubwa".

JK ni HAAMBILIKI...kiti kimemnogea amesahu yote aliyo ahidi

Mkullo pamoja na kutojua anajua fika kwamba bajeti mawaziri wataingia Mikoanio kuiptisha kwa wananchi kwa style yao mpya .So no worries wadanganyika wamelala.

Watu wameaanza kuamka bahati mabaya idadi ni ndogo....lakini soon wote wataamka
 
Back
Top Bottom