BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,820
- 287,887
Balozi Uingereza amfunda JK
Mwandishi Wetu
Daily News; Monday,June 09, 2008 @08:33
BALOZI wa Uingereza nchini Philip Parham, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kutoogopa kuchunguza na kuwashitaki viongozi waovu bila kujali umaarufu wao.
Parham alisema kitu cha msingi ni kuangalia endapo ushahidi na maslahi ya umma yanahitaji afanye hivyo; bila kujali kuwa watuhumiwa ni watu mashuhuri kiasi gani.
Usiogope kuchukua uamuzi unaoweza uonekane wa hatari wakati tayari maamuzi hayo yamekwisha kuhalalishwa na viashiria vya faida yake, alisema Parham katika maadhimisho ya miaka 82 ya kuzaliwa Malkia Elizabeth II, yaliyofanyika Dar es Salaam juzi.
Lakini pia amemtaka asiogope kuungoa uzembe na udanganyifu. Lakini pia usiogope kuwaamini marafiki zao kama wanastahili uwapo uaminifu huo...usiogope kuendeleza na kuhamasisha ufanisi pamoja na uadilifu, alisema katika hotuba yake.
Balozi huyo alitaka pia Rais asiogope kukabiliana na watu wenye maslahi binafsi ambao wanajaribu kuzuia maendeleo kwa sababu zao za kichoyo.
Pia amewataka viongozi kutoogopa kuachia ngazi au wadhifa pale ambapo kazi fulani yaweza kufanywa vizuri na wengine.
Akizungumzia uchumi wa Tanzania, balozi huyo alisema bajeti ya mwaka uliopita ilikuwa takriban dola bilioni 5, kiasi ambacho Waingereza wanakitumia katika kununua mikanda ya DVD kwa mwaka.
Hii pia ni sawa na asilimia 2.5 tu ya bajeti ya Afya ya Uingereza kiasi hicho ni sawa kabisa na robo ya fedha ambayo wacheza kamari Uingereza wanakipoteza kwa mwaka na kwamba kiasi hicho ni sawa na thamani ya chakula kinachotupwa kama mbaki nchini mwake.
Hiki kiwango halisi cha fedha ambacho Serikali ya Tanzania inacho ili kuweza kuwapatia wananchi wake huduma ya elimu, afya, miundombinu pamoja na ulinzi kwa wananchi milioni 40 waishio nchini ambayo ni kubwa zaidi ya mara nne kwa Uingereza, alisema.
Alisema kuna nuru katika hali ya baadaye ya Tanzania. Ikiwa katika hali ya utulivu, mshikamano wa jamii, demokrasia hai, uchumi mzuri, fursa kubwa ya kiuchumi ambazo hazijatumika kikamilifu, Rais mwenye uwezo na utashi kutoka Jumuiya ya Kimataifa ina nafasi kubwa ya kubadilika, alisema.
Balozi alisisitiza kuwa Tanzania si nchi masikini na wananchi wake hawapaswi kuwa masikini.
Alisema matumaini ambayo ameyaona katika baadhi ya mikoa bila kusahau katika macho ya watoto wa Kituo cha Dogodogo cha Dar es Salaam na hakika matumaini hayo yasivunjwe moyo na akasisitiza kuwa yanawezekana tu iwapo kila mtu atatimiza wajibu wake.
Balozi huyo aliwataka Watanzania wasiogope kusema ukweli juu ya dola hasa pale dola inapotishia ustawi wa heshima ya binadamu na utulivu katika ukanda huu.
Lakini pia alitaka Watanzania wasiogope kubadili fikra zao pamoja na sera endapo itajidhihirisha wazi kwamba uelekeo mpya ni sahihi. Pia wasiogope kuipatia sekta binafsi fursa, uhuru pamoja na kujiamini katika kuongeza nafasi ajira, tija na ukuaji wa uchumi.