Balozi Sefue: Tumepokea mapendekezo ya bunge, ila tunataka kwenda deep zaidi

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,526
....Katika kile kinachoonekana kama sakata la ESCROW kuanza episode nyingine, katibu mkuu kiongozi Balozi Sefue amekiri kupokea maoni na mapendekezo ya bunge, ila amesema uchunguzi unaendelea kuona kama kweli tuhuma hizo ni za kweli au la!!

My Take:

This is another episode, let us stay tune.

Dar es Salaam. Ikulu imesema pamoja na kuwa Rais Jakaya Kikwete amekwishapokea maazimio ya Bunge kuhusu wanaotuhumiwa kuchota Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow, hawezi kuwachukulia hatua mpaka hapo uchunguzi kuhusu suala hilo utakapokamilika.

"Rais lazima aagize vyombo vya uchunguzi kufanya kazi yake na baada ya hapo ndipo atapata mahali pa kuanzia. Watu wengi walitaka Rais Kikwete achukue hatua baada ya kupewa maazimio ya Bunge. Jambo hilo haliwezekani," Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema jana na kuongeza kuwa hatua zitachukuliwa kwa watakaobainika kuwa na makosa ya kimaadili au jinai baada ya uchunguzi.

Alisema uchunguzi kuhusu uchotwaji wa mabilioni hayo uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) pia utazingatiwa na Rais katika kutoa uamuzi.

"Maazimio ya Bunge ni mazuri ila inatakiwa muda kwanza ili Rais naye apate taarifa za uchunguzi zaidi. Maazimio hayo ni muhimu na si ya kupuuzwa hata kidogo," alisema.

Alisema vyombo vinavyofanya uchunguzi kuhusu suala hilo ni vile ambavyo vilitajwa kufanya hivyo katika maazimio manane ya Bunge.

Bavicha wamtaka Kikwete achukue hatua

Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), limemtaka Rais Kikwete kuacha kuhamisha wakuu wa mikoa na badala yake atoe uamuzi wa kuwashughulisha watuhumiwa wote waliohusika na kashfa ya escrow.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu wa Bavicha, Mwita Julius alisema: "Wakati huu si mzuri wa kuanza kuhamisha wakuu wa mikoa kwa kuwa ni gharama, ni muda wa kuwachukulia hatua wahusika wote waliotajwa bungeni wakihusika na sakata la escrow."

Alisema Rais anatakiwa kuwashughulikia wateule wake wote waliotajwa bungeni kwani wananchi wanasubiri kuona mabadiliko hayo kwa haraka.

Juzi, Rais Kikwete aliteua mkuu mmoja wa mkoa na kuwahamisha wengine sita.

Chanzo:Mwananchi
 
huyu naye ni mbwa tunataka mwenye mbwa aseme haraka sio hawa wafuta miguu yake. AG, PCCB, PAC na BUNGE wamesema tunataka nini tena, mbona madiwani wanakamatwa kwa amri ya DC, mbona watumishi wengine wanafukuzwa kwa rushwa ndogo ndogo tu. KITENDO cha kukaa kimya zaidi ya wiki mbili ni aibu, deep ataenda nani wakati ikulu inahusika pia???
 
Hiyo kauli ndio kauli ya JK mkubwa.
 
....Katika kile kinachoonekana kama sakata la ESCROW kuanza episode nyingine, katibu mkuu kiongozi Balozi Sefue amekiri kupokea maoni na mapendekezo ya bunge, ila amesema uchunguzi unaendelea kuona kama kweli tuhuma hizo ni za kweli au la!!

My Take:

This is another episode, let us stay tune.

Source: ITV Habari

Kuna vyombo vya uchunguzi wa zaidi ya hv vilivyofanya ss?
 
Ikulu imejiridhisha kwamba tuhuma dhidi ya Muhongo ni za UONGO NA UNAFIKI WA HALI YA JUU SANA
 
....Katika kile kinachoonekana kama sakata la ESCROW kuanza episode nyingine, katibu mkuu kiongozi Balozi Sefue amekiri kupokea maoni na mapendekezo ya bunge, ila amesema uchunguzi unaendelea kuona kama kweli tuhuma hizo ni za kweli au la!!

My Take:

This is another episode, let us stay tune.

Source: ITV Habari
Huo mradi wa bwana mkubwa ndio maana hawataki kuwajibishana
 
Ikulu inatajwa tajwa kwenye tuhuma hii, nani sasa afanye uchunguzi! Pccb lipoti yake imefichwa! Sasa nani!?
 
Haya, pale kesi ya mbuzi anapopelekewa fisi unadhani ni nini kitatokea
 
Ondoa%2BCCM%2BCHADEMA%2Bx.png
 
Ikulu, huyu sefue si ndo alisababisha broken zikaongewa ikulu, alinyanyasa housegirl USA wakafukuza akaja kuula hapa kwenye ikulu chafu kuliko zote EAC
Yaani ile shombo ya feri tu yahitaji mapafu ya ziada kuivumilia.
pakitema tu feri hata ukiwa IFM UNASHIKA PUA, sijui ikulu penyewe!! Ndo maana professor dhaifu yuko busy angani anakwepa harufu ya thamaki wa feri!!
 
Blaza ndo umeongea ulabugani hapo?
 
Wakuu Jk anajua anawaongoza wafu so hata asipochukua hatua hakuna lolote linaweza kutokea!!Ss hatujielewi kila mtu yuko kimpango wake na hata hawa viongozi wa upinzani wameishia tu kutoa matamko na hawayatekelezi!!Kwani mara ngapi hata wanasusa vikao vya bunge tena kwa mbwembwe afu baada ya muda yanapita kiubaridi bila kuchukua hatua zozote!Hii nidhamu ya woga tuliojengewa na muasisi wa taifa hili ccm watatumia kutunyonya mpaka makamasi!Naomba prof. Jk asichukue uamuzi wa aina yoyote km hata tutazinduka kutoka usingizini!
 
Back
Top Bottom