Sakata la Dowans: Balozi Paul Ndobho amemtaka Rais Kikwete kuvunja baraza la mawaziri!

ASKOFU MSAIDIZI

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
209
23
Kufuatia mgongano wa mawaziri kuhusu sakata la malipo ya Dowans, Balozi Paul Ndobho ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Musoma Vijijini mkoani Mara amemtaka Rais Kikwete kuvunja baraza la Mawaziri!!
Pia alimupongeza Samweili Sitta kwa kuwa mzalendo na shujaa

Augustino Mrema yeye amemtaka Rais Kikwete kutolea ufafanuzi juu ya mgongano wa mawaziri kutokana na sakata la malipo ya Dowans.

Mrema amewataka mawaziri wote wanao pinga malipo hao wajiuzuri na kupinga uamuzi huo wakiwa nje ya serikali.

Chanzo: Nipashe
 
Claire Short alifanya hivyo (kujiuzuru) ....alipokuwa anapinga mauzo ya Rada kwa Tanzania by BAE systems ambapo waziri mkuu Tony Blair alikuwa akiunga mkono.

Mkuu,
Sahihisho:
Clair Short hakujiuzulu kwasababu ya kupinga mambo ya rada. Alijiuzulu kwasababu ya mambo ya Iraq
 
Sitta na mwakyembe hawapaswi kujiuzuru bali wanatakiwa kuimarisha upinzani ndani ya ccm kwa maslahi ya taifa.



Tunataka kuona wahalifu wana anikwa ndani ya ccm ili wakose kukimbilia upinzani!


Huwezi ukakimia shamba na kumwacha nguruwe anakura!!!!
 
Mrema amewataka mawaziri wote wanao pinga malipo hao wajiuzuri na kupinga uamuzi huo wakiwa nje ya serikali.
Source : Nipanshe ya leo
Kwani serikali ipo upande gani, wa mawaziri wanaopinga ulipaji au wanaounga mkono ulipaji?
 
Back
Top Bottom