Balozi Ombeni Sefue amrithi Luhanjo

Kuna uwezekano mkubwa kuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Bw. Ombeni Sefue ndiye atakayerithi mikoba ya Katibu Mkuu Kiongozi aliyejikuta kwenye malumbano na wabunge mwaka huu pamoja na kygubijwa na lawama nyingi Bw. Luhanjo a.k.a "Chifu". Hizo ndizo tetesi tulizozisikia leo.
Kweli ka inzi kako mkuu ni noma!!!!!!!!!
 
kumbukumbu hazionyeshi kama Luhanjo ambaye ni CS alipata kuwa miongoni mwa UWT
 
Acha majungu, mbunge gani anastahili nafasi hii, hii ni nafasi ya serikali kama mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa, hii ni mihimili miwili tofauti..

Wakenya hamstahili kuingilie kwenye maswala yetu ya ndani mkuu, ka mbali na hili jukwaa.

Mbunge anaweza kuwa mkuu wa wilaya/mkoa muda wowote kwa matakwa ya mkuu wa nchi, lakini hii position ni tofauti.
 
Anatakiwa ajue sana medani ya siasa na utawala wa hapa nyumbani kuwa ubinafsi kwanza.....na ufisadi kwanza!!hongera sana Balozi Sefue!!
 
Kwenye red. Mkuu Chif Secretary sie Katibu wa Baraza la Mawaziri cheo hicho kinaitwa Karani wa Baraza la Mawaziri (Clerk to the Cabinet). Wa mwisho kumfahamu alikuwa somebody Mkwizu. Nafasi hiyo hata Pinda aliwahi shika 1996 mpaka alipopata Ubunge 2000. Kimsingi post hizi za CS na Karani BLM ni reserved (sijui kama ni sahihi) kwa watu wa system masenior waliokaa Ikulu mda mrefu.
Mkuu labda unaongelea secretariat. Katibu MKuu Kiongozi ndiye Katibu wa Baraza la mawaziri. Sasa huo ukarani mimi sijui. Clerk to the Parliament ni karani wa bunge au katibu wa bunge au anaitwa Secretary to the Parliament? Hivi vyeo vya Westminster mzee siyo vya Tanzania! Usijaribu kufanya direct translation utapotosha umma!
 
Kuna uwezekano mkubwa kuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Bw. Ombeni Sefue ndiye atakayerithi mikoba ya Katibu Mkuu Kiongozi aliyejikuta kwenye malumbano na wabunge mwaka huu pamoja na kygubijwa na lawama nyingi Bw. Luhanjo a.k.a "Chifu". Hizo ndizo tetesi tulizozisikia leo.

Yamkini waliopo pale New York United Nation wameshaona mtu anafungasha virago, maana siku hizi secret services zimepanuka na siri zinamwagwa nje nje, anapotangwazwa tayari watu walishajua kinachoendela.

Iweje Vatican inapotangaza uteuzi wa askofu bongo wameshajua nani na muda atatangazwa, iweje bongo yetu?
 
Anatakiwa ajue sana medani ya siasa na utawala wa hapa nyumbani kuwa ubinafsi kwanza.....na ufisadi kwanza!!hongera sana Balozi Sefue!!
Naona profile yake inaonyesha amekaa nje kwa muda. Kuna faida zake kama kuleta utendaji wa kimagharibi hapa Tz lakini pia kuna shida zake hasa zinapokuja siasa za ndani. Inabidi azisome siasa za ndani na ku cope nazo kwa mwendo kasi wa mwanga!
 
Mpui Lyazumbi,

..Joseph Butiku alikuwa Private Secretary[Katibu] wa Raisi, na baadaye akateuliwa Mkuu wa mkoa wa Mara mpaka alipostaafu.

..David Jairo naye alikuwa Private Secretary wa Raisi kabla hajateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Nishati na Madini.

..hiyo ni nafasi nzito na nyeti ambapo uteuzi wake hufanywa na Raisi mwenyewe.

kumbe ndo maana Jairo kiburi,yawezekana anajua mengi ya Mkulu na anaogopwa,duhhhh
 
Hakuna kisichowezekana katika awamu hii. MM tusaidie profile ya huyu Mhe. Balozi.

Kwa uchache

OMBENI Y. SEFUE
Ambassador Ombeni Yohana SEFUE formally began his tour of duty as Permanent Representative of the United Republic of Tanzania to the United Nations in New York on 31st August, 2010. Before that he was Tanzania's Ambassador to the United States of America in Washington D.C. from 15th June, 2007 to 14th August, 2010. Previously, Ambassador Sefue served as his country's High Commissioner (Ambassador) to Canada from October 2005 to June 2007.
A career diplomat, Ambassador Sefue also served as Counselor in the Embassy of Tanzania in Stockholm, Sweden, between 1987 and 1992.
Between 1993 and 2005, he worked as Speechwriter and Personal Assistant to two Presidents of Tanzania- President Ali Hassan Mwinyi (1993-1995) and President Benjamin William Mkapa (1995–2005).
Among other things, Ambassador Sefue assisted President Mkapa when he served on the Commission for Africa (The Blair Commission) that produced its report, Our Common Interest: Report of the Commission for Africa in March 2005, and participated with him at the G8 Summit session that discussed the report at Gleneagles in early July 2005.
He also worked with President Mkapa when the president served as Co-Chair of the ILO World Commission on the Social Dimension of Globalization between 2002 and 2004, participating in the preparation of the Commission's report, A Fair Globalization: Creating Opportunities For All, issued in February 2004.
Ambassador Sefue completed his undergraduate studies in Public Administration in 1977 at what is today Mzumbe University in Morogoro Tanzania. He earned an M.A. in Public Policy and Administration from the Institute of Social Studies (ISS) in The Hague, The Netherlands, (1981). He holds a Post-Graduate Diploma in International Relations and Diplomacy from the Tanzania-Mozambique Center for Foreign Relations in Dar es Salaam, Tanzania (1986).
Ambassador Sefue is married to Mrs. Anita M. Sefue and they have two children.
 
Kuna uwezekano mkubwa kuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Bw. Ombeni Sefue ndiye atakayerithi mikoba ya Katibu Mkuu Kiongozi aliyejikuta kwenye malumbano na wabunge mwaka huu pamoja na kygubijwa na lawama nyingi Bw. Luhanjo a.k.a "Chifu". Hizo ndizo tetesi tulizozisikia leo.
Mkuu Mwanakijiji, nakuvulia kofia!.

Sasa baada ya tetesi hizi kuthibitishwa, ulitakiwa kuiupdate hii thread!
 
Duh naona watu wanapinga uteuzi lakini hawasemi ubaya wa aliyeteuliwa! Labda tu kwa kuwa kateuliwa na JK! Jamani mwenye mamlaka ya kuteua ni JK kwa sasa hakuna mwingine na urais wake hauna ubia. Tuwape nafasi walioteuliwa wafanye kazi tutawapima tu baada ya muda mfupi katika majukumu yao hayo mapya. Haya mambo ya watu walewale bila kusema kwa mfano angemteua fulani kwa kuwa ana.sifa zifuatazo ambazo huyu aliyeteuliwa hana afadhali. Pia tukumbuke mtu anayeteua na kuthibitisha uteuzi ni mmoja hivyo si rahisi kuridhisha kila mtu!
 
viongoziikulu.JPG

Mkuu wanatumia pencil ila sema tu alisahau kulipiga kifuto na kulirekebisha.
 
Luhanjo ameaidiwa kupewa Ubalozi katika nchi za Africa, stay tune
Huu upuuzi utaisha lini? Hii nchi inaonekana ukitaka kuukwaa uongozi lazima uwe mtuhumiwa hahahhah bongo raha kweli kweli! CCM mbona mnatuchosha hivi lakini huu umangimeza utaisha lini? Kupeana madaraka kama vile watanzania wengine ni mbumbumbu mzungu wa reli. Watu wazee mvi mpaka oops! sorry.
 
Kuna uwezekano mkubwa kuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Bw. Ombeni Sefue ndiye atakayerithi mikoba ya Katibu Mkuu Kiongozi aliyejikuta kwenye malumbano na wabunge mwaka huu pamoja na kygubijwa na lawama nyingi Bw. Luhanjo a.k.a "Chifu". Hizo ndizo tetesi tulizozisikia leo.

vituko,sidhani kama itakuwa hivyo,kk lazima awe amepitia cheo cha uktbmkuu
 
Kuna watu ambao katika serikali ya ccm yatupasa kujua wakati wote wako wapi na wanafanya nini. Ombeni Sefue ni mmoja wa watu hao.
 
Mwkjj, huko mwanzo, ulisema.....Sefue ni mtu wa karibu "sana" na Kikwete. Msisitizo uko kwenye neno "SANA"

then:

Kuna watu ambao katika serikali ya ccm yatupasa kujua wakati wote wako wapi na wanafanya nini. Ombeni Sefue ni mmoja wa watu hao.

Inaelekea Ombeni Sefue unamfahamu vizuri. Inapendeza JF inapokua na watu wanawajua viongozi wetu kwa undani , natumaini uko mbele utafunguka zaidi kuhusu uyu mweshimiwa ukaribu wake na utawala wa sasa wa TZ, na kwa nini inatupasa kujua wakati wote wako wapi na anafanya/wanafanya nini.
 
Back
Top Bottom