Balozi mpya wa China nchini Marekani aonesha tofauti ya uongozi wa busara kati yake na mwenzake wa Marekani

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,006
1,026
VCG111341342553.png

VCG111354742259.jpg
Ushindani mkubwa kati ya Marekani na China umekuwa ukifukuta na kuatiliwa sana katika miaka ya hivi karibuni. Mtazamo hasi wa Marekani dhidi ya China unajidhihirisha wazi zaidi katika kipindi hiki, kwani Marekani bila aibu wala kificho imekuwa ikiishambulia hadharani kwa maneno na kuinyooshea kidole China kwenye masuala mbalimbali, makubwa kwa madogo au hata yale yanayotokana na usimamizi wake mbaya kama vile COVID-19.

Marekani sasa imefanya mchezo na inaona ni jambo la kawaida kwake kuingilia mambo ya ndani ya China, yakiwemo masuala ya eneo lenye utawala maaluma la Hong Kong, ukiukaji wa haki za binadamu za watu wa Xinjiang hata kuunga mkono wafarakanishaji wanaotaka Taiwan kupata uhuru, huku kila siku ikihubiri kinafiki kwamba itaendelea kushikilia sera ya kuwepo kwa China moja, na eti pande hizo mbili zinatakiwa kuendeleza uhusiano wao kwa moyo wa kuheshimiana.

Mfano mzuri unashuhudiwa kwa Balozi wa Marekani nchini China Nicholas Burns, ambaye uteuzi wake umeidhinishwa bungeni hivi karibuni. Balozi Burns hivi majuzi tu alijifanya "mbwa mwitu mkali” na kuishambulia vikali China wakati alipokuwa kwenye kikao cha Seneti. Burns amesahau kwamba atakuja kufanya kazi ya kuiwakilisha nchi yake hapa Beijing, hivyo badala ya kuonesha nia na utayari wake wa kukuza mawasiliano ya kidiplomasia kati ya China na Marekani na mawasiliano ya kirafiki kati ya watu wa nchi mbili, ameamua kuonyesha tabia ya "mbwa mwitu mkali", akifahamu vizuri kwamba kitendo hicho ni sawa na kuitusi maana halisi ya ujumbe wa kidiplomasia na kuonesha mfano mbaya katika duru za kidiplomasia.

China siku zote inatetea ushirikiano wa kirafiki na nchi za nje, na endapo kuna tatizo au mgogoro wowote basi ni lazima kuondolewa kwa njia ya amani. Mabalozi wa China wameonesha kikamilifu falsafa ya kidiplomasia ya China. Balozi mpya wa China nchini Marekani Qin Gang, alionesha tabia iliyo kinyume kabisa na ile iliyooneshwa na balozi wa Marekani, kwamba “unapokwenda ugenini lazima umuheshimu mwenyeji wako”. Badala ya kuishambulia Marekani, balozi Qin aliamua kuitakia ushindi katika vita vyake dhidi ya COVID-19 na kusema fursa kubwa ziko mbele ya uhusiano baina ya nchi hizo mbili, akionesha matumaini wakati alipowasili kubeba wadhifa wake mpya.

Kwenye ujumbe wake alioutoa kupitia tovuti ya ubalozi wa China, Balozi Qin alisema: “Uhusiano kati ya China na Marekani, kwa mara nyingine tena upo kwenye wakati mpya muhimu, ukikabiliwa na sio tu mitihani mingi na changamoto, bali mbele kuna fursa nyingi pia.”

Licha ya shutuma zilizotolewa na mwenzake wa Marekani, Balozi Qin ameonesha matumaini makubwa, na kubainisha fursa zilizopo katika ushirikiano huu mkubwa wa pande mbili katika masuala yakiwemo mabadiliko ya tabia nchi na kudhibiti COVID-19 duniani. Pia aligusia diplomasia ya pande mbili yaani “ping-pong diplomacy” ambayo ilitoa njia ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Marekani katika mwaka 1979, na kutangaza nia yake ya kujenga uhusiano huu uwe wa busara zaidi, uwe imara, na kuweza kusimamiwa vizuri.”

Hii ndio China na hii ndio tabia ya muungwana anayotakiwa kuionesha kwa mwenzake. Busara ni kitu muhimu sana katika uongozi wa ngazi yoyote ile, uongozi usio na busara ni mithili ya chombo kinachokwenda mrama.

Lakini hii haimaanishi kwamba China itaendelea kunyamaza kimya tu na kuridhia vitendo vya kuipaka matope, la hasha!Ppale inapolazimika kujibu, huwa inajibu ili kuondoa utata unaojitokeza kwenye kauli chafu zinazotolewa.

Katika jukumu lake jipya, Balozi Qin atakuwa mstari wa mbele kuendeleza juhudi za rais wa China, Xi Jinping, za kuunda upya uhusiano wa China na Marekani ambao unaonekana kuwa na madoa mengi katika miongo ya hivi ya karibuni. Tunatarajia mabalozi wote wawili watawakilisha nchi zao kwa kufuata kanuni za kidiplomasia na kuheshimu nchi mwenyeji. Pia ni vyema kuonesha kwa vitendo nia yetu ya kuishi kwa maelewano duniani.
 
Wewe utakuwa CCM, Tena CCM uchwara. China with all this nasty history of gross basic human rights violations, unaisifu China? Umelogwa! Ukiwa CCM huwezi kufikiria sawasawa
 
Get shit off inside your head,na ujifunze kukubaliana na Imani za watu
 
Back
Top Bottom