Balozi Mbelwa Kairuki: Mpaka sasa hakuna Mtanzania hata mmoja aliyeambukizwa maradhi ya Corona

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
Leo Februari 11, 2020 Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki amezungumza kuhusu video inayowaonesha vijana wa Kitanzania wanaosoma China wakiomba msaada wa kurejeshwa makwao.

Balozi ameeleza kuwa mpaka sasa hakuna Mtanzania hata mmoja aliyeambukizwa maradhi hayo kutokana na kufuata maelekezo wanayopata kutoka kwa mamlaka za China.

Amesema mara kwa mara huwasiliana na wanafunzi hao pamoja na serikali ya China ili kufahamu na kutatua changamoto ndogo zinazowakabili na ameishukuru serikali ya China kwa ushirikiano wanaotoa kwa vijana wa Kitanzania.

Balozi akasema dawa imegunduliwa na Idadi ya watu wanaopona imeongezeka huku Idadi ya maambukizi ikipungua kwa asilimia 50 nje ya mji wa Wuhan ambao ndio kitovu cha virusi hivyo hatari.

Balozi akasema kuwa kuishi kwa kufuata maelekezo ndilo jambo linalomfanya hata yeye kubaki hai. Amesema hawaruhusiwi hata kutoka nje na kwamba kitendo cha kukusanyika walichokifanya vijana hao ni hatari sana kwa afya zao.

Kuhusu ombi la vijana hao kurejeshwa Tanzania, Balozi Kairuki amesema hakuna usafiri wowote unaoruhusiwa kutoka ama kuingia kwenye mji wa Wuhan na kwamba Japan ilijaribu kuwaokoa vijana wake lakini kwa bahati mbaya wakaambukizwa na kuvibeba virusi hivyo mpaka nchini kwao.

Balozi akasema virusi hivyo ni hatari na kwamba serikali ya Tanzania haitafanya kitendo chochote kitakachokuja kuwadhuru Watanzania walio wengi.

Balozi huyo akasema kitendo walichokifanya vijana hao kimetokana na msongo wa mawazo unaotokana na kukaa ndani ya uzio wa makazi yao bila ruksa ya kutoka nje.

Balozi Kairuki akatoa wito kwa Watanzania kumuombea yeye na Watanzania wengine wanaoishi China ili Mwenyezi Mungu awavushe salama na kadhia hiyo. Pia amewaomba wazazi kuwapa faraja vijana wao waliopo China ili waondokane na msongo wa mawazo.

Nukta Muhimu: Tatizo lililopo China lisitumiwe kisiasa kwani serikali haiwezi kutumia nguvu kwenda kuwachukua vijana hao kwakua imejifunza kutokana na dosari zilizojitokeza wakati wa Serikali ya Japan ilipoamua kuwarudisha raia wake nchini mwao waliokuwa wanaishi China.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini Serikali yetu hukibilia Mungu kwa jambo linalohitaji utekelezaji? Akili tuliyopewa na Mungu na kodi tunayotoa kama haiwezi kuwasaidia watu wetu tunalipa kodi ya nini.

Halafu unakimbilia eti tatizo hilo isitumike kisiasa wakati siasa ni maisha na ni kila kitu acheni kudanganya watu. Haya mambo yanakera sana
 
Blah blah blah

Tumuamini Kairuki maana yeye ni mkweli?

Kuna mtu yeyote wa hii serikali ni wa kuamini akisemacho?

Tunaamini wale watoto, wao ndio wakweli zaidi ya yeyote!

Wanaomba kurudi nyumbani maana ni kwao

Wakifika wawahifadhi mahali maalumu mpaka wawe salama kutoka

Serikali bana, inakwepa majukumu kwa sababu za uongo mtupu!
 
Wyatt Mathewson,
Hahaha wao wanafanya siasa kwenye hili, waliambiwa na balozi wa China Tanzania kwamba China itawasaidia kwa kila hali.

Lakini walioko huko ambao ni wanafunzi wameonyesha kua hawapati huo msaada wa hali na mali. This is all politics.

Ngoja wakianza kufa utasikia statement zao, kwamba Magufuli hakuleta Corona virus.
 
kwa nini serikali yetu hukibilia mungu kwa jambo linalohitaji utekelezaji? Akili tuliyopewa na mungu na kodi tunayotoa kama haiwezi kuwasaidia watu wetu tunalipa kodi ya nini.

Alafu unakimbilia eti tatizo hilo isitumike kisiasa wakati siasa ni maisha na ni kila kitu acheni kudanganya watu. haya mambo yanakera sana
Tupe wewe basi maelezo yako.
 
Tuwaombee wenzetu walioko huko Wuhan, China wasije wakaambukizwa hilo liugonjwa na jinsi ngozi nyeusi tunavyochukiwa, sidhani kama watapatiwa matibabu mazuri zaidi ya kuachwa wakufe.

Lakini najiuliza kwanini balozi anashindwa kuwatafutia makazi mbadala maana inaonekana makazi yao hayako salama kwa kuwa yamegeuzwa wodi ya kuwahudumia wagonjwa; labda pengine kwa sababu waliobaki hapo chuoni ni Waafrika tupu.
 
Kuna statement inasema chuo walichopo ndipo wagonjwa wanapopelekwa, kama ni kweli hapo huwezi kuwa na matumaini hata kwa kusali.

Mkuu.,kama pana mwana Jamiiforums yeyote alie Eneo la tukio au mwenye kujuana na yeyote huko awasiliane nae/nao labda tunaweza kupata Taarifa Sahihi zaidi。
 
Mkuu.,kama pana mwana Jamiiforums yeyote alie Eneo la tukio au mwenye kujuana na yeyote huko awasiliane nae/nao labda tunaweza kupata Taarifa Sahihi zaidi。
Pointi yangu imebase katika aya yake ya pili anaposema 'waache kudanganya watu'.Ndo nasubir alete ripoti yake inayopingana na hii au wewe uliyemwelewa waweza nijibu.
 
Tiba ipo kama unaipata maana hata waliopo nchi zingine au kuleta hii Coronavirus wamepona
Kwa hiyo ni bora wakae huko kwenye dawa na wafuate masharti tu
Tuna watoto huko tuwape faraja tu


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Sitegemei kuona serikali ikilikalia kimya ombi lao,sijui watajibiwa nini ila ningependa kujua serikali itaamua uamuzi upi wa busara na hekima!

Sisi hata tukijadili huku mitandaoni kwamba waje au wasije bado mwenye mamlaka ya uamuzi na utendaji ni serikali.. itakuwa vyema jambo hili pia likijadiliwa bungeni ili tuone watetezi tuliowateua wanaamua nini juu ya watanzania wenzetu...
 
Back
Top Bottom