Balozi Majaar v/s Waislam UK

mzaramo

JF-Expert Member
Sep 4, 2006
6,371
5,175
NAONA KAGOMA HATA KUWAPA SALAM ZA IDDI.KISA? YUKO BIZE

Halafu anataka kuwa cloze na watanzania

Ndugu yetu saidi yakubu alikwepo naye hapo kwenye baraza la iddi manor park, east london, (sehemu ya london yenye watanzania wengi zaidi).

Maelezo yanatoka kwenye blog yake:

Lakini zaidi ya hayo ningependa kuchua nafasi hii kuwafahamisha kuwa balozi wetu bi mwanaidi majaar hajatoa salam zozote kwa watanzania waislam waliopo uk kwa sababu balozi tumeambi alikuwa "bizee" tofauti na balozi kibello aliyeondoka ambaye pamoja na mapungufu yote huwa alikuwa natoa slama na kujumuika nasi pale manor park.once again balozi kaonyesha jinsi gani alivyokuwa na nia ya kujumuika na watanzania kwa ujumla

Vile vile katika hali ya kushangaza ni kuwa mwenyekiti wa tanzania association uk bwana aboubakar faraji aligoma kutoa mchango wa kufanya baraza la iddi kwa sababu waislam wa north london walikataaa masharti yake ya kutaka kuweka matangazo yake western union!

Swali ni je tangu lini baraza la iddi likawa sponsored na matangazo?

PICHA:

1. Imam wa Ibada ya leo Ustadh Hamisi alifananisha mwezi wa Ramadhani uliomalizika kama ni chuo kikuu cha Ibada na kuelezea umuhimu wa kuendeleza uzoefu wa Ibada uliopatikana nje ya mwezi wa Ramadhani, nilipozungumza nae baadae alinielezea namna walivyo na afueni kwa kuruhusiwa kutekeleza uhuru wao wa kuabudu hapa Uingereza ukilinganisha na nchi nyingine za Ulaya.

2.Watu walikuwa ni wengi kwa hakika na mchango wa papo hapo kulipia ukumbi wa sala ya Iddi ulichangisha kiasi cha £425.00 na hakika eneo lote la chini lilijaa na wengine kulazimika kusali katika ghorofa ya juu na wengine nje. Matokeo kama haya yanakufanya udhani kisahihi kabisa kuwa wabongo tupo wengi...

3. Mwenye bakora ni Al Maarufu GARAMTENI...UKITAKA HALUA WE ULIZA TU..

4. Bingwa wa zamani wa kusoma Quran Ustadh Masudi alikuwepo na hapo akiwa mitamboni..

5.Ustadh Nassor wa EAST AFRICAN FOUNDATION nae pia alikuwepo na hapa alikuwa akizungumzia umuhimu wa kutoa zakatil fitr- ambayo alieleza ni lazima kutolewa na muislamu yeyote mwenye uwezo wa kula idd kwa wasio na uwezo huo ili nao wajisikie...

BLOG HII INAWATAKIWA WADAU WOTE IDD MUBARAK AGAIN...
IMG_1845.JPG
IMG_1844.JPG
IMG_1853.JPG
42[1].JPG
eid el fitr 244.JPG
eid el fitr 247.JPG
eid el fitr 248.JPG
eid el fitr 251.JPG
 
Hope mlimaliza salama, na kutokutoa salamu za iddi kwa muheshimiwa majaar kusiwasononeshe sana, si mlipeana wenyewe kwa wenyewe?
labda na yeye alitegemea kuwa mngemtumia pia, mlifanya hivyo?
si unajua unapojua kupokea ujue na kutoa vile vile.
Sikukuuu njema waungwana.
 
Huo usongo ulionao na balozi hauishi tu? Mwache mama afanye kazi yake hiyo ya kutoa hongera ilishafanywa na Jk kule nyumbani inatosha. Kama una issue nyingine weka hapa tuijadili.
 
kwani asipotea salam ya eid ina mapungufu gani au unaloko na huyu mama wa watu
 
Naunga mkono: Kama iko issue iwekwe wazi hapa. Sasa tunaanza kuwa trivial and petty, pale tunapofuata mambo ya blog zingine ambazo hutumika kama chombo cha mtu binafsi kufikisha chuki ama raha binafsi.
Balozi huyu anajali umoja wetu kuliko "mfalme" Yaa-kubu anaegombania kuua: Je Balozi alikaribisha? alikataa ama alikuwa na udhuru? kwa ubinadamu wake asingeweza kuwa na udhuru? Kukosekana salamu za Iddi ndilo jipya/ Za pasaka zilipokosekana ilikuwa ni dhidi ya ukristo? Si ufinyu wa fikra huo!
Huyu nadhani si Balozi wa bla bla; na vitendo tunaviona.Umoja wa watanzania Uk uko imara kuliko ambavyo umewahi kuwa tangu Uhuru. Salaam zote za za viongozi wetu, hazifiki ama? Tujenge hoja hapa JF, majungu na chuki tuwaachie hao wenye blog tata (au toto?)
 
Back
Top Bottom