Elections 2015 Balozi Mahiga, Pinda, Kitine, Makongoro na wengineo jitokezeni. Ukweli utawaweka huru

mayenga

JF-Expert Member
Sep 6, 2009
4,118
1,966
Ni takribani wiki mbili sasa mchakato WA kumpata mgombea ndani ya Chama tawala umemalizika.Katika michakato yote ambayo chama hiki imefanya,Ni wazi kuwa mchakato huu ulikuwa na changamoto kubwa kuliko yote.

Wanachama wakongwe na wenye heshima zao kabla hata mchakato kuisha,walijitokeza na kuonesha kwa jinsi ambavyo hawakuridhika na mwenendo WA mambo.Sophia Simba,Nchimbi,Kimbisa na wengineo,SI watu WA kubeza ndani ya chama,Ni watu ambao wana mchango uliotukuka ndani ya chama.

Hisia zao,ziliungwa mkono na wajumbe wa mkutano Mkuu ambao waliimba bila kujali kuwa mbele Yao Yuko Mwenyekiti na wazee wakongwe chamani.Kitendo,cha kumtaka mgombea ambaye hakuwa kwenye majina yale matano,ilikuwa Ni changamoto ya aina yake,kwa maneno yake mwenyewe Rais anakiri kuwa hakuwa kushuhudia.

Katika viunga vya mji wa Dodoma,hali haikuwa shwari.Makundi ya kila aina yalionesha hisia za wazi.Kila mmoja kwa nafasi yake alieleza kutoridhika na mchakato kwa namna tofauti.

Mzee mkongwe na mwanachama WA siku nyingi mwenye kadi namba 8na mwasisi WA chama,Mzee Kingunge,hakutaka kuvumilia.Aliwaita waandishi nyumbani kwake na bila kupepesa aliongea maneno mazito.Itakuwa Ni ukosefu wa fadhila kama anaweza kumbeza Mzee yule.Mzee huyu kama amesikilizwa vema,anachosema Ni procedural irregularities zilizojitikeza na wala hazungumzii kufaa na kutofaa kwa mgombea aliyepatikana.

Mzee huyu anasema kanuni ambazo ndo msingi wa mchakato zimevunjwa.Mpaka sasa hakuna majibu ya kuridhisha,badala yake Msekwa na Nape,wamekuwa na majibu mepesi mno.

Ni wazi kuwa kila aliyekuwa mgombea anafahamu kanuni,na bahati nzuri nyinyi wagombea waliokatwa mmekuwa wasimamizi WA kanuni hizo.Jaji Ramadhani umekuwa msimamizi WA haki,na sasa umeijongea altare ya bwana,Ni wazi kuwa ukiongea lipi lilitokea,ukweli utakuweka huru.

Wassira,wewe ndo umeandaa ilani ya chama,chama umekitetea kwa Kila hali katika dhoruba na machafuko yaliyo kikumba,jitokeze PIA utuambie Ni kipi kilikupata mpaka ukakatwa na kushindwa kukurupuka.

Bilal na Pinda nyie Ni watu muhimu katika taifa itakuwa Ni aibu kuzidi kuwawajibisha watendaji ndani ya serikali,kama mlishindwa kusimamia kanuni ambazo ziliwaengua na hata msijulikane kama mliingia kumi bora,ishirini bora au thelathini bora.

Mzee wangu Kitine wewe Ni mkurugezi WA usalama mstaafu,Balozi Maiga uadilifu Wako hautiliwi shaka.Sasa Ni kipi kiliwapata.

Jitokezeni mtuambie.
 
Kapatikana mmoja sahivi kundi lao ni CCM ..wewe unataka ya ndani yaletwe nje kwa faida ya nani? nendeni kwa kilaza na mropokaji Kingunge aendelee kuwasimulia vigano na ngano zake
 
Hizi ndio akili mufilisi!
Hebu fanyeni yenu, ya CCM tuachieni wenyewe!
Ukawa wenyewe mmeshindwa kuafikiana kupata mgombea hadi leo, badala mjadili nini kimewasibu mnahangaika kutuchafua, Magufuli hazuiliki bwana ndogo!
 
makongoro alishasema Kuwa aliongoza kwa Kuwa na alama zajuu toka kamat ya maadili na akaongeza kwa kusema aliingia tano bora.. ILa kiongoz mmoja mkuuuubwa aliliondoa jina lake na kuweka la mtu mwingine....akasema anamsamehe kiongoz huyo 7*70....
 
Rekebisha andiko lako ili ionekane kweli wewe ulifuatilia mchakato ndani ya Chama...kwanza hata wiki haijafika (ni siku sita tu baada ya uteuzi); pili siyo Mkutno Mkuu walipoimba wimbo wa imani kwa Lowassa, bali ni Halmashauri Kuu (NEC).

Ukishafanya hayo basi sasa jenga hoja yako. Lakiji kumbuka siyo lazima hao watu waongee hadaharani mawazo yao kuhusu mcahakato. Hatuna (au hasa Chama) utamaduni huo, huo ni utamafuni wa magharibi ambao ni wa kibeberu na kibepari tusioutaka.
 
Rekebisha andiko lako ili ionekane kweli wewe ulifuatilia mchakato ndani ya Chama...kwanza hata wiki haijafika (ni siku sita tu baada ya uteuzi); pili siyo Mkutno Mkuu walipoimba wimbo wa imani kwa Lowassa, bali ni Halmashauri Kuu (NEC).

Ukishafanya hayo basi sasa jenga hoja yako. Lakiji kumbuka siyo lazima hao watu waongee hadaharani mawazo yao kuhusu mcahakato. Hatuna (au hasa Chama) utamaduni huo, huo ni utamafuni wa magharibi ambao ni wa kibeberu na kibepari tusioutaka.

Niliyoandika nimeandika
 
Hawawezi kujitokeza kwa sababu wanajua taratibu na kanuni za chama ni kuwa malalamiko yote hutolewa kwenye vikao vya chama na si katika vyombo vya habari.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom