Balozi Mahiga: Mke wangu hakumtukana askari, walipishana kauli

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863
Amesema mke wake hakumtukana askari aitwaye Deogratias Mbando bali walipishana. "Nilifuatilia suala hili, walitofautiana tu kauli. Mama hakutukana" alisema. Hata hivyo alisema suala hilo limeisha na asingependa kuendeleza malumbano hayo.
===================

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga, amezungumzia sakata la mke wake kudaiwa kumtukana askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani.

Dk. Mahiga alisema kwamba mke wake alipishana kauli na askari huyo aliyefahamika kwa jina la Deogratius Mbango, na hakutoa lugha ya matusi kama inavyodaiwa.

Alisema baada ya kupokea taarifa hiyo, alifuatilia ili kujua ukweli, ikiwamo kusikiliza sauti ya majibizano baina ya askari huyo na mkewe, ambapo alibaini kuwa walipishana kauli.

Hata hivyo Balozi Mahiga alisema suala hilo kwa sasa limemalizika na asingependa kuingia kwenye malumbano zaidi kwa jambo lililopita.

“Ni kweli mama (mke wake) alikuwa katika barabara ya Namanga, ambako alipishana kauli na askari wa usalama, nami nilifuatilia suala hili kwa undani sana. Ninachoweza kusema sitaki kuingia kwenye malumbano juu ya suala hili kwa kuwa limemalizika.

“Wewe umesikiliza hiyo ‘clip’ (sauti ya mazungumzo) je, umesikia neno tusi? Hilo ndilo ninalojua kwa sasa, mengine sijui yanayoendelea,” alijibu kwa kifupi Balozi Mahiga.

Alipoulizwa kuhusu kusambaa kwa picha inayomdhalilisha, Dk. Mahiga alisema kwamba alishangazwa na picha hiyo huku akishindwa kuelewa lengo la watu walioitengeneza na kuisambaza.

“Hata mimi sijui lengo lao nini kuisambaza ile picha, maana mimi niliiona kama ulivyoiona wewe,” alisema.

Picha ya Balozi Mahiga inayoonyesha suruali yake imelowa sehemu ya mbele, imekuwa ikizunguka katika mitandao ya kijamii kwa takriban wiki moja sasa.

Chanzo: Mtanzania
 
Amesema mke wake hakumtukana askari aitwaye Deogratias Mbando bali walipishana. "Nilifuatilia suala hili, walitofautiana tu kauli. Mama hakutukana" alisema. Hata hivyo alisema suala hilo limeisha na asingependa kuendeleza malumbano hayo.

Chanzo: Mtanzania
hivi huyu anapata wapi jeuri ya kubishana na rais? ina maana kile cheo alichokitoa rais makufuri kwa askari ni feki? mahiga ni JIPU! kwa kuwa matusi hayakuwa recorded ndio maana anakuwa na jeuri ya kukataa. nadhani hata yale mabishano yasingekuwa recorded angebisha tu.
 
Amesema mke wake hakumtukana askari aitwaye Deogratias Mbando bali walipishana. "Nilifuatilia suala hili, walitofautiana tu kauli. Mama hakutukana" alisema. Hata hivyo alisema suala hilo limeisha na asingependa kuendeleza malumbano hayo.

Chanzo: Mtanzania
kwa hiyo yule askari alipandishwa cheo kmakosa?...
 
Huyu jamaa nadhani hata kwenye #Bunge la Katiba akishirikiana na yule #Chenge pana kiburi fulani walikuwa wakionyesha waziwazi, yaani hawa watu sijui wanajiaminia kitu gani ?

Pombe wavuruge hawa viumbe maneno maneno yaishe, maana waTanzania wanasema eti hawa hawakamatiki,
 
Back
Top Bottom