Balozi Liberata Mulamula ni chachu ya maendeleo ya Tanzania na Mataifa ya Nje

Chee4

Member
May 17, 2021
31
125
Balozi Liberata ni mwanamama hodari na mchapakazi. Pamoja na kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Liberata ameonekana akipiga kazi kwa kasi ya 5G.

Tangu uongozi wake, MulaMula amekutana na Viongozi mbali mbali wa nje ya nchi kama Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Idadi ya Watu (UNFPA) Dkt. Natalia Kanem, pia Balozi Liberata amefanikisha kumleta Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni kwa ajili ya kusaini mkataba wa mradi wa bomba la mafuta na pia amezesha mkutano kati ya Rais Samia na Rais wa Kenya Mhe. Kenyatta kujadili jinsi gani wataboresha masuala ya kiuchumi. Haya yote ni kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wetu kama nchi na mataifa mengine nje ya nchi.

Balozi Liberata ni mwanadiplomasia mashuhuri na sifa moja wapo ya kuwa mwanadiplomasia ni kuweza kuratibu majadiliano baina ya nchi zaidi ya moja. Ameweza kushiriki vikao vingi vya ndani na nje ya nchi na ameonekana ni kiongozi muadilifu na mweye uweledi mzuri kwenye kazi yake.

Kwa kumalizia, Balozi Liberata ameweza kuiwakilisha na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania huko nchini Kanada, Marekani na Mexico.
 

Mr Q

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,727
2,000
Nilifuatilia kongamano fulani alijitambulisha kama mama msipitwe. Ilikuwa huko kwa trump wakati bado akiwa balozi.

Anaonekana yuko vizuri kwenye masuapa yahusuyo mataifa
 

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
1,954
2,000
WATANZANIA KWA KUSIFIA VITU VIDOGOVIDOGO NAKUACHA VIKUBWA AU KUACHA KUFIKILIA KWA UNDANI NI UGONJWA WA AJABUNA UPUUZI..YAANI RAIS WA UGANDA KUJA TANZANIA NDO TUNAONA NI ISSUE
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom