Balozi Liberata Mulamula: Naamini nitakuwa mshauri mkuu kwa Mhe. Rais

Shadow7

JF-Expert Member
Sep 28, 2020
5,357
2,000
Baada ya kuapishwa Bungeni leo Mhe. Liberata Mulamula ambaye aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya jana kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amefunguka haya:

...lakini kwa kumsaidia Rais, kama mulivyosikia ameniteua kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa East Africa. Lakini, mnajua mahusiano yetu na nchi za nje ni mapana sana. Na wakati huu kuna chemchem sana ya kuweza kukuza hayo mahusiano. Kwahiyo, mimi nitakuwa mshauri mkuu kwa Mh. Rais.

Bahati nzuri, Mh. Rais wetu Mama Samia anajua mambo ya nje sana, pengine hata kunizidi. Lakini pia, amekuwa mstari wa mbele katika kukuza mahusiano mazuri na kanda yetu Afrika Mashariki, na nchi zote za SADC. Na mtaona hata wakati wa kuapishwa, wakati wa msiba mzito tuliokuwa nao; viongozi wengi sana waliokuja ni kutoka kanda ya SADC.

Kwahiyo, mimi nitaanzia kwenye kanda. Na kama mnavyojua mimi nilikuwa [Ukanda wa]Maziwa Makuu kwa kipindi kirefu; ni kanda ambayo ina mambo mengi -- migogoro. Lakini ni sehemu ambayo tuna mahusiano mazuri.
 

Chillah

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
5,867
2,000
`|°

IMG_20210401_124114.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom