Balozi Karume: ‘CCM pekee iwe inasimamisha mgombea urais Zanzibar’

Tume ya Katiba

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
4,896
1,862
Inaposemwa kuwa nchi haitolewi kwa vikaratasi huwa sio mzaha, ni kweli........



By Balozi Ali Karume

Baada ya kusoma makala yaliyoandikwa kwenye gazeti hili na mwandishi Salim Said Salim kuhusu kauli yangu niliyoitoa nikipendekeza CCM pekee iwe inasimamisha mgombea urais Zanzibar, nafafanua baadhi ya mambo.

Ni kweli kwamba nilitamka na nitaendelea kutamka kwamba-CCM pekee ndiyo iwe inasimamisha mgombea urais wa Zanzibar. Sababu nimezieleza kwa umahiri kwamba ni kwa nia ya kutuliza joto la kisiasa linalotokea kila wakati wa uchaguzi.

Joto hilo husababisha hali hatarishi kwa usalama na hali ya amani na utulivu katika nchi yetu. Sioni sababu ya msingi ya kuendelea na chaguzi za kushirikisha wapinga Mapinduzi, kwenye nchi ambayo ilipata uhuru kwa Mapinduzi yaliyofanyika ya Januari 12, 1964.

Tunapozungumzia Mapinduzi na kaulimbiu “Mapinduzi Daima”, tunakusudia kulinda Mapinduzi; kwa hali yoyote na Katiba yetu ndivyo inavyosema.

Kuendelea kuwaza kwamba chama cha wapinga Mapinduzi kinaweza kushiriki uchaguzi wa kumpata Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ni dhana potofu inayojikanganya na dhana ya kulinda Mapinduzi.

Kila mwenye kufikiri, anayo haki ya kutafakari niliyoyasema na kutoa maoni yake; na sishangai kauli hiyo kuzua mjadala. Nasema, tulifanya haraka kutengeneza Katiba inayoacha mwanya kwa wapinga Mapinduzi kutwaa madaraka ya urais kwa kushinda kura za urais hata kwa kura moja.

Mchambuzi wa hali ya kisiasa na historia ya Zanzibar mwenye kujiheshimu, hataweza kudharau nguvu ya hoja yangu. Katiba ya sasa ya Zanzibar siyo Katiba stahiki; ni Katiba ya Mapinduzi ‘kujitoa roho’.

Hilo halikubaliki kwa baadhi yetu tuliopania kulinda Mapinduzi yetu. Dawa yake, kama nilivyotamka ni kwa Katiba kurekebisha nafasi ya urais iwaniwe na Chama cha Mapinduzi na vyama vingine viwanie nafasi nyingine zote vikichuana na CCM.

Zipo nchi nyingi duniani za kimapinduzi, zinalinda Mapinduzi yao kikatiba. Iran walifanya Uchaguzi Mkuu unaohusisha vyama vyote, lakini siyo kwenye nafasi ya urais.

Wagombea wote kwenye nafasi hizo walitakiwa kutimiza masharti ya kukidhi dhana ya kulinda Mapinduzi ya Iran. Zaidi ya wagombea 250 walinyimwa fursa ya kugombea kwa kukosa sifa za kikatiba.

Sikueleweka

Ndugu yangu Salim hakunielewa kabisa kwenye matamshi yangu, hasa pale anapodai kwamba “kutokana na kauli zake (nyingi) za hivi karibuni nisingeshangaa kama angesema yeye pekee ndiye angelistahili kuwa mgombea”. Katika yote niliyosema, hata ukiondoa mabano, sioni uhalali wa mtu yeyote ambaye ni mchambuzi wa mambo ya siasa kuhalalisha dhana hiyo potofu.

Sijawahi kutamka neno lolote litakaloweza kumfanya mtu mwenye akili timamu kuikumbatia dhana hiyo. Pengine dhana hiyo imegubikwa na malalamiko.

Kama ni hivyo, malalamiko hayo yaelekezwe kwa mgombea wake wa urais huku Zanzibar (Maalim Seif Sharif Hamad), maana kwa tabia na vitendo vyake anajiona ‘yeye pekee ndiye anastahili kuwa mgombea.’

Alianza kuwania nafasi hiyo karne iliyopita, mwaka 1985 kupitia CCM katika kura za maoni alipitwa kwa kura saba na ‘akanuna’ hadi kuamua kupiga kampeni ya kumkosesha kura mgombea urais wa CCM wa wakati huo. Chama kilimhukumu na kumfukuza uanachama mwaka 1988.

Baada ya kutangazwa mfumo wa vyama vingi, mwaka 1992 mgombea huyo alikuwa na fursa ya kufanya mambo mawili. Kwanza, angeweza kurudi CCM na kuomba kurejeshewa uanachama wake. Hilo linaruhusiwa kufanywa baada ya miaka mitano kupita. Angefanya maombi hayo mwaka 1993.

Baada ya kurejea CCM angeweza kuwania tena nafasi ya urais, lakini alifanya uamuzi wa makusudi wa kuunda chama cha kisiasa kwa sababu alikuwa na lake jambo.

Anayezijua vizuri siasa za Zanzibar atakubaliana nami kwamba huko siyo rahisi mtu kuunda chama cha siasa na kufanikiwa kwa haraka. Njia pekee ni kwenda ‘makaburini’ na kufufua vyama vya upinzani vilivyokufa.

Pia, tukumbuke kwamba baada ya Mapinduzi vyama vya upinzani vilipigwa marufuku na hawakuridhika na hilo walisubiri fursa ya kufufuliwa na Chama cha Wananchi (CUF).

Hapo ndipo narejea na nguvu ya hoja yangu kwamba CUF siyo chama kipya bali ni zao lililotokana na muungano wa vyama vya ZNP na ZPPP.

Nataka nimkumbushe rafiki na jirani yangu Salim kwamba, sijawahi kusema kwamba waanzilishi wote wa CUF wametokea ZNP na ZPPP. Waanzilishi wa CUF walitokana na vyama vingi pamoja na ASP, Umma , ZNP na ZPPP.

Hadithi yake ndefu ya kunikumbusha nani kaanzisha CUF imeamsha kumbukumbu yangu, lakini haikunishtua maana sijawahi kudai CUF ilianzishwa na ZNP na ZPPP pekee.

Maelezo yangu ni kwamba, baada ya CUF kuanzishwa na kushamiri imechukua sura na rangi ya muungano wa vyama vya ZNP-ZPPP. Hakuna anayeweza kupingana na hilo maana huo ndiyo ukweli wenyewe. Asemaye vinginevyo ndiye anapotosha historia ya Zanzibar.

Baada ya ZNP na ZPPP kupigwa marufuku baada ya Mapinduzi, viongozi wake na wafuasi waliondoka nchini. Wengi walikwenda Oman, Uingereza na nchi zingine za Uarabuni.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995

Mwaka 1995 baada ya CUF kujitangazia ushindi batili kwenye uchaguzi wa urais wa Zanzibar, wengi waliosherehekea walikuwa huko nje.

Mwaka jana, baada ya mgombea wa CUF kujitangazia urais ambalo ni kosa la jinai walisherehekea huko huko.


Hao wote ni vizazi vya wafuasi wa ZNP- ZPPP. Huo ndiyo ukweli ambao wengi hawataki kuukubali na nakubaliana na wazee waliposema “funika kombe mwanaharamu apite” na sikubaliani na mwandishi anapodai “funua kombe mwanahalali asimame.”

Kiongozi wa CUF ambaye ni mwakilishi wa kuchaguliwa kwenye jimbo huko Pemba ambaye pia ni Waziri katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), aliniambia kwamba yupo CUF kutokana na wosia aliopewa na baba yake.

Baba yake alikuwa ZPPP na alimhusia kwamba aingie CUF na ajaribu kuitoa CCM madarakani. Aliniambia, bila kumung’unya maneno kwamba watashinda na baada ya kushinda watarejesha mashamba yote, majumba yote na mali zote kwa wamiliki wa kabla ya Mapinduzi.

Aliniambia, “Balozi, Mapinduzi ilikuwa ni udhalimu tu na siku ya uhuru wa kweli ni tarehe 10 Desemba 1963”. Alisema wakichukua madaraka, siku hiyo ndiyo watasherehekea uhuru na Januari 12 itakuwa ni siku ya kawaida, siku ya kazi kwa watu kwenda kazini kama kawaida.

Kutokana na uzoefu wangu na ushahidi tosha nilionao naweza kujisifu na kauli yangu kwamba, CUF ni jora moja na muungano wa vyama vya ZNP na ZPPP. Wale waliopinduliwa mwaka 1964 wanataka kutumia Katiba dhaifu kurejea madarakani.

CUF ni jina tu jipya, lakini chini ya ngozi yao ya kondoo utamkuta ‘mbwamwitu’ wa muungano wa vyama vya ZNP-ZPPP. Anza na Jimbo la Mji Mkongwe ambalo kihistoria lilikuwa ZNP na mpaka leo ni jimbo la CUF. Wakazi wengi ni vizazi vya ZNP na Wapemba wa vizazi vya ZPPP.

Kwingine kote; Bumbwini, Nungwi ni ZNP. Kwa upande wa Pemba, kura zimekwenda kufuata matokeo ya uchaguzi kabla ya Mapinduzi. Maeneo ya ZNP na ZPPP yamechukuliwa na CUF karibu yote.

CCM imepata kura nyingi maeneo ya Kusini Pemba, ingawa haikupata jimbo. Kutamka kwamba ZNP-ZPPP imefukuka kwa umbo la CUF ndiyo kuielezea historia katika ukamilifu wake. Kudai kwamba CUF ni chama kipya chenye wanachama kutoka vyama vyote bila ya kuegemea ZNP-ZPPP ni kupotosha historia ya Zanzibar.

Hoja ya machotara

Kudai kwamba ubaguzi unaendekezwa na CCM hasa pale wanapodai kwamba CUF ni machotara ni kupoteza muda. Kama nimekusoma vizuri, basi kihistoria utakuwa umekosea.

ASP ambayo baadaye ilikuwa CCM haibariki ubaguzi wa aina yoyote na ndiyo maana baada ya Mapinduzi, Sheikh Abeid Aman Karume alipiga marufuku ubaguzi wa aina yoyote na vilabu vya kikabila.

Pia, alidiriki kushawishi Waafrika waoane na wakubali kuolewa na makabila mengine. Kuna binamu yangu ambaye alikataa kabisa kuolewa na Mwarabu, lakini alikubali baada ya Mzee Karume kumsihi akubali.

Yote hayo na mengineyo, Mzee Karume aliyafanya ili Wazanzibari tuwe kitu kimoja. Na kweli tulikuwa kitu kimoja mpaka ilipokuja hii dhana ya vyama vingi kuturejesha tena kule kule tulikokimbia baada ya Mapinduzi.

ASP ilikuwa mstari wa mbele kupinga ubaguzi na CCM imefuata mwiko. Katika uchaguzi wa mwaka 1961 kwenye Jimbo la Rahaleo, ASP haikuweka chotara, bali Mhindi, Rostam Sidhwa kuwania kiti. ZNP walimuweka Katibu mkuu wao, Abdulrahman Mohamed Babu.

Bila shaka yoyote ZNP ndiyo walikuwa wabaguzi. Na huyo Babu alifukuzwa ZNP kwa kushauri wagombea wa ZNP wenye asili ya Kiafrika wagombee kwenye majimbo yaliyokuwa na Waarabu wengi.

ZNP walikataa na kudai kwamba wagombea hao waende kwa Waafrika wenzao na wakishindwa shauri yao. Huo, kwa mtazamo wangu ndiyo ubaguzi. Madai kwamba ASP-CCM ni wabaguzi ni sawa na kudai kwamba kunakucha kwa sababu jogoo anawika.

Jogoo akiwika asiwike kutakucha tu. Jogoo wa ZNP hakuwika, lakini kulikucha siku ya Mapinduzi na Zanzibar Huru ikaja.

Nashukuru kwa wosia wa mwandishi kwamba, kama mtu hana jambo zuri la kusema ni bora akae pembeni.

Mwandisi ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kusini Unguja.


wenu,

Tume ya katiba


chanzo. mwananchi.co.tz
 
Yuko sawa maana hakuna haja ya kupanda mbegu wakati tayari msimamizi wa shamba ameandaa sehemu ya mavuno yanayomfaa yeye na siyo mkulima anayehangaika
 
Kiukweli mtu yoyote mwenye akili timamu ukizisoma hoja za Balozi Karume, utakubaliana na mimi kuhusu utimamu wa akili zake.

Wakati kaka yake wa tumbo moja toka ntoke, Amani Karume anamaliza kipindi chake cha urais wa Zanzibar, Balozi Karume alijaza fomu kugombea.

Akashauriwa kwa vile rais anayemaliza muda wake ni kaka yake wa tumbo moja, tena toka nitoke, Ali akipitishwa itaonekana urais wa Zanzibar ni usultani. Akaulizwa baada ya kuona kaka yako katawala miaka 10, kwanini na wewe uutake urais wa Zanzibar?.

Alijibu kitu cha ajabu sana kinachothibitisha huyu mtu sii mzima hata kidogo!.

Alisema sababu za Amani Karume kupewa urais wa Zanzibar ni kumuenzi muasisi wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, hivyo Amani Karume amepewa urais wa Zanzibar kwasababu tuu ni mtoto wa Karume!.

Ndipo Balozi Ali Karume akasema, kama kaka yake Amani amepewa urais wa Zanzibar kwa sababu ni mtoto wa Karume, basi aliyestahili kupewa urais wa Zanzibar ni yeye na sii kaka yake kwasababu (naomba nisimalizie mambo mengine ni siri za familia)

Na uthibitisho umeletwa humu JF Zanzibar 2020 - Urais Zanzibar 2020: Barua kwa Balozi Ali Abeid Amani Karume (Barua ikilenga kumchafua)

Kwenye uzi wangu wa

Hivyo kufuatia utimamu huo, na mimi Pasco wa jf, kwa kauli moja, naunga mkono hoja, kuwa CCM ndio pekee iruhusiwe kusimamisha mgombea urais wa Zanzibar, tena sio tuu CCM ndio pekee wagombee urais Zanzibar, bali CCM ndio pekee wagombee urais wa JMT, kwa sababu CCM ndicho chama pekee chenye hati miliki ya urais wa JMT na Zanzibar kiliopewa na Mungu!, hii ni kufuatia long euksipiriensi ya uzoefu wa muda mrefu kwenye urais!.

CCM Oyeee...!.

Pasco
 
Kiukweli mtu yoyote mwenye akili timamu ukizisoma hoja za Balozi Karume, utakubaliana na mimi kuhusu utimamu wa akili zake, hivyo kufuatia utimamu huo, na mimi Pasco wa jf, kwa kauli moja, naunga mkono hoja, kuwa CCM ndio pekee iruhusiwe kusimamisha mgombea uais wa Zanzibar, tena sio tuu CCM ndio pekee wagombee urais Zanzibar, bali CCM ndio pekee wagombee urais wa JMT, kwa sababu CCM ndicho chama pekee chenye hati miliki ya urais wa JMT na Zanzibar kiliopewa na Mungu!, hii ni kufuatia long euksipiriensi ya uzoefu wa muda mrefu kwenye urais!.

CCM Oyeee...!.

Pasco

Ninapata picha kwa nini machafuko hayaishi duniani, kwa sababu kuna watu kama Balozi Ali Karume.
 
Kiukweli mtu yoyote mwenye akili timamu ukizisoma hoja za Balozi Karume, utakubaliana na mimi kuhusu utimamu wa akili zake, hivyo kufuatia utimamu huo, na mimi Pasco wa jf, kwa kauli moja, naunga mkono hoja, kuwa CCM ndio pekee iruhusiwe kusimamisha mgombea uais wa Zanzibar, tena sio tuu CCM ndio pekee wagombee urais Zanzibar, bali CCM ndio pekee wagombee urais wa JMT, kwa sababu CCM ndicho chama pekee chenye hati miliki ya urais wa JMT na Zanzibar kiliopewa na Mungu!, hii ni kufuatia long euksipiriensi ya uzoefu wa muda mrefu kwenye urais!.

CCM Oyeee...!.

Pasco
Unaumwa wewe !
 
Huyu Karume Ni mtu mjinga,kwani ZNP naZPPP sio wanzanzibari?
Ceucescu aliyeongoza mapinduzi Romania aliishia wapi kama mapinduzi Ni hoja
Kama CUF inakubalika na Wanzanzibar wengi hoja ya mapinduzi hata kama inakubalika na wachache ni muflsi
 
Wapumbavu ni wengi!Basi tuseme mapinduzi hayakulenga kuleta usawa na haki kwenye jamii,kama tunachagua baadhi ya haki na nyingine kuminya sidhani kama ni lengo la mapinduzi!
 
Mnyoa na yeye hutokea siku moja akanyolewa tu!

Kina Karume na CCM yake wanajiona ni wanamapinduzi, hata ninyi mnaweza kupinduliwa tu kwa sababu hii ya sasa si dunia ya wakati ule wa Sultan wa Oman!!
 
Woga huu wa kihistoria ndiyo unaleta matatizo huko Zanzibar. Kuna watu wanaogopa vivuli vyao, miaka karibu 50 bado unafikiria tu ya ASP ZNP, ZPPP! Ubaguzi ni sawana kula nyama ya mtu ukianza hautoacha.
 
Yuko sahihi kabisa na ndilo lililopo znz kwa sasa. Vyama vyote vinaruhusiwa kutoa Mgombea Urais ila chama kimoja tu ndio kinaruhusiwa kutoa Rais
 
Back
Top Bottom