Kivumah
JF-Expert Member
- Jan 7, 2008
- 2,428
- 1,050
Balozi Juma Mwapachu
--
Mhe.Dkt.JakayaMrishoKikwete,Rais waJamhuriyaMuunganowa Tanzania amemteua Balozi Juma Mwapachu kuwaMwenyekitiwaBaraza la Chuo Kikuu cha Dodoma kuanzia tarehe 14 Septemba 2011.Atakuwa kwenye nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minne (4)
Balozi Mwapachu anachukua nafasiiliyoachwa wazinaMhe. Dkt. Mohamed Ghalib Bilal ambaye alikuwaMwenyekiti wa kwanza na sasa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania.
Mhe.Balozi Juma Mwapachu amewahikushika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya nchi zikiwemo KatibuMkuu waJumuiya ya AfrikaMashariki, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa ikijumuisha nchi zaUhispania, Ureno, Tunisia, Morocco na Algeria.
Aidha Mhe.Balozi Juma Mwapachu amekuwa mjumbe wa Bodi mbalimbali hapa nchini na amewahikushika nyadhifa zaj uu katikaTaasisi zaUmma na binafsi.Kwa muda mrefu alikuwa naibu Mwenyekiti wa baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Mhe.BaloziJuma Mwapachu amehitimu shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki na alikuwa Mtanzania wa kwanza mwenye shahada ya Chuo Kikuu kujiunganaJeshi la Polisi nchini.
Mhe.Balozi JumaMwapachu aliwahikutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa falsafaya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na amewahi kuhariri nakuchapisha majarida na vitabumbalimbali.
Uongozi w aJumuiya nzima ya Chuo Kikuu cha Dodoma inamkaribisha na kumtakia kila la kheri Balozi Juma Mwapachu katika majukumu yake mapya.
Source: Haki Ngowi Blog