Balozi Juma Mwapachu ateuliwa kuwa Mwenyekiti Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma

Kivumah

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,428
1,050
mwapachupix.jpg

Balozi Juma Mwapachu
--
Mhe.Dkt.JakayaMrishoKikwete,Rais waJamhuriyaMuunganowa Tanzania amemteua Balozi Juma Mwapachu kuwaMwenyekitiwaBaraza la Chuo Kikuu cha Dodoma kuanzia tarehe 14 Septemba 2011.Atakuwa kwenye nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minne (4)

Balozi Mwapachu anachukua nafasiiliyoachwa wazinaMhe. Dkt. Mohamed Ghalib Bilal ambaye alikuwaMwenyekiti wa kwanza na sasa ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania.

Mhe.Balozi Juma Mwapachu amewahikushika nyadhifa mbalimbali ndani na nje ya nchi zikiwemo KatibuMkuu waJumuiya ya AfrikaMashariki, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa ikijumuisha nchi zaUhispania, Ureno, Tunisia, Morocco na Algeria.

Aidha Mhe.Balozi Juma Mwapachu amekuwa mjumbe wa Bodi mbalimbali hapa nchini na amewahikushika nyadhifa zaj uu katikaTaasisi zaUmma na binafsi.Kwa muda mrefu alikuwa naibu Mwenyekiti wa baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Mhe.BaloziJuma Mwapachu amehitimu shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki na alikuwa Mtanzania wa kwanza mwenye shahada ya Chuo Kikuu kujiunganaJeshi la Polisi nchini.

Mhe.Balozi JumaMwapachu aliwahikutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa falsafaya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na amewahi kuhariri nakuchapisha majarida na vitabumbalimbali.

Uongozi w aJumuiya nzima ya Chuo Kikuu cha Dodoma inamkaribisha na kumtakia kila la kheri Balozi Juma Mwapachu katika majukumu yake mapya.

Source: Haki Ngowi Blog

Akili mgando tuu!huyu mzee hana jipya kwanza kiasi kikubwa yeye ndugu yake ndiye aliyeua ATC akauza ndege zote akanunua mbovu!pia ktk ubunge wake tanga aliua ule mji kabisa.kwa ufupi huko ni kulindana ili aendelee kupata posho za vikao!
 
Ni dini gani huyu jamaa? Maana jana niliona thread ya mambo ya udini udom.. Kazi kwetu kutoa maoni great thinkers! Hongera balozi juma mwapachu...
 
Haya huyu bwana nae anaruka mkojo anakanyaga mavi,baada yakuwapa vijana nafasi anaenda kupewa huyu mzee ......
 
Ckujua km aliwahi jiunga na Jeshi la Polisi - hivyo alikua Polisi au mfanyakazi wa kawaida alieajiriwa na polisi?

Ila wa siku nyingi? Wanatoka huku wanaenda huku....... Vijana tunang'aa sharubu tu kitaa........
 
Rais wetu mtukufu nafurahi kukujulisha kuwa wewe ni mvivu sana. Kwani hawa wazee mpaka leo hii wameshindwa kutuletea maendeleo hilo hulijui hata uawang'anga'nie? Mbona zipo damu changa nzuri sana na zilizozoea mazingira ya wanavyuo ambazo zinaweza kuikabili mikimiki ya wanafunzi. je umekuwa mvivu hata hukupekua mafaili yao kuona wasivyo na tija? TUMECHOSHWA na wazee hawa. Hawana lolote. hawana tija sasa. Wangelikuwa na tija pesa walizokwisha zizoa ktk nyazifa zao mbali mbali wangelikuwa wameanzisha viwanda ambamo vijana wetu wangekuwa wanapata ajila. Rais acha uvivu!!!
 
Kama aliwahi kuwa Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Dar es Salaam pengine hicho ndicho cheo pekee katika orodha ya vyeo tunavyoambiwa kitakachomsaidia kuendesha Baraza za Chuo Kikuu Dodoma. Tufahamu kuwa kuwa mwenyekiti wa Baraza la Chuo ni tofauti kabisa na kuwa kiongozi wa kiutawala au kiutendaji sehemu nyingine yeyote. Lazima uwe na uelewa na uendeshaji wa chuo kikuu. Kazi yake kubwa ni kuongoza maamuzi ya kisera ya kuendesha chuo kikuu chake, hivyo, bila kuwa na mwanga wa kitaaluma huwezi na utaishia kuchekwa wakati wa vikao. Kazi yake ni tofauti sana na MKUU WA CHUO KIKUU (Chancellor) ambacho ni cheo cha heshima tu. Labda tujiulize kitu kimoja: Kwanini uongozi wa juu wa UDOM umejazwa na watu wa dini moja? Sitaki kuingiza hoja ya udini hapa bali uhalisia wa mambo unaoonekana waziwazi ndani ya uongozi wa juu wa chuo kikuu hiki. Tafakari, chukua hatua.
 
Mwapachu na Fisadi Kikwete wote wanatumia Masaburi kufikiria, hakuna jipya hapo tegemeeni Elimu kuporomoka kwa Kasi mpya, Ari mpya
 
TUMECHOSHWA na wazee hawa
Jina Mwapachu kwenye madaraka nimelisikia nikiwa darasa la kwanza way back, waaaay waaaay back, mpaka leo hii midingi bado inapeana mashavu, na si kama hana kazi, si yuko kwenye payroll ya Barrick huyu mzee? Na nina hakika yuko kwenye vikamati na vibodi vingine vingi tu. Mzee Kikwete, kwa nini unalimbikiza mishahara kwa mtu mmoja???

TUMEWACHOKA!
 
Mwapachu tangu sijazaliwa namsikia.

Jamani tusiwaonee haya hawa wazee wasio na mapya, yupo pia Wasirrrrrrra. Toka sijazaliwa!!!!!!
Hawana changamoto yoyote ya kuiendeleza nchi hii. Cha ajabu ni viongozi hao hao waliouwa SU zetu na wasichukuliwe hatua ila kwa kuwapongeza katika hilo, kila asubuhi wanarundikiwa vyeo kama kwamba ni wao tu wasomi. Wanatufanya sisi wasomi tuhisi kudhalilishwa. RAIS ACHA UVIVU.
 
Kama aliwahi kuwa Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Dar es Salaam pengine hicho ndicho cheo pekee katika orodha ya vyeo tunavyoambiwa kitakachomsaidia kuendesha Baraza za Chuo Kikuu Dodoma. Tufahamu kuwa kuwa mwenyekiti wa Baraza la Chuo ni tofauti kabisa na kuwa kiongozi wa kiutawala au kiutendaji sehemu nyingine yeyote. Lazima uwe na uelewa na uendeshaji wa chuo kikuu. Kazi yake kubwa ni kuongoza maamuzi ya kisera ya kuendesha chuo kikuu chake, hivyo, bila kuwa na mwanga wa kitaaluma huwezi na utaishia kuchekwa wakati wa vikao. Kazi yake ni tofauti sana na MKUU WA CHUO KIKUU (Chancellor) ambacho ni cheo cha heshima tu. Labda tujiulize kitu kimoja: Kwanini uongozi wa juu wa UDOM umejazwa na watu wa dini moja? Sitaki kuingiza hoja ya udini hapa bali uhalisia wa mambo unaoonekana waziwazi ndani ya uongozi wa juu wa chuo kikuu hiki. Tafakari, chukua hatua.

Unataka kutuambia akifa leo basi itatubidi kutafuta mtaalamu toka nje?! Acha hizo.
 
Ckujua km aliwahi jiunga na Jeshi la Polisi - hivyo alikua Polisi au mfanyakazi wa kawaida alieajiriwa na polisi?

Ila wa siku nyingi? Wanatoka huku wanaenda huku....... Vijana tunang'aa sharubu tu kitaa........
Jamii ya vijana kwa kweli INAUMA
 
Sina shaka nae! Uwezo anao ingawa sijui kwanini hajiiti DR
Kuitwa/kujiita Dr,(PHD)?? katika Nchi hii kwa sasa haina maana kama huutumii Ujuzi na Elimu ulionayo katika kutatua matatizo lukuki ambayo Nchi hii inapitia.
 
Ckujua km aliwahi jiunga na Jeshi la Polisi - hivyo alikua Polisi au mfanyakazi wa kawaida alieajiriwa na polisi?

Ila wa siku nyingi? Wanatoka huku wanaenda huku....... Vijana tunang'aa sharubu tu kitaa........
...Uki-google, utaona moja ya Professional Experience zake. Aliwahi kuwa Askari Polisi
6. PROFESSIONAL EXPERIENCE

April 1969 – Sept.1969
: First Tanzania Graduate to join the Tanzania Police Force (Asst. Supt. of Police) then reverted to Attorney General's Chambers, Government of Tanzania, (State Attorney)
 
Kama aliwahi kuwa Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Dar es Salaam pengine hicho ndicho cheo pekee katika orodha ya vyeo tunavyoambiwa kitakachomsaidia kuendesha Baraza za Chuo Kikuu Dodoma. Tufahamu kuwa kuwa mwenyekiti wa Baraza la Chuo ni tofauti kabisa na kuwa kiongozi wa kiutawala au kiutendaji sehemu nyingine yeyote. Lazima uwe na uelewa na uendeshaji wa chuo kikuu. Kazi yake kubwa ni kuongoza maamuzi ya kisera ya kuendesha chuo kikuu chake, hivyo, bila kuwa na mwanga wa kitaaluma huwezi na utaishia kuchekwa wakati wa vikao. Kazi yake ni tofauti sana na MKUU WA CHUO KIKUU (Chancellor) ambacho ni cheo cha heshima tu. Labda tujiulize kitu kimoja: Kwanini uongozi wa juu wa UDOM umejazwa na watu wa dini moja? Sitaki kuingiza hoja ya udini hapa bali uhalisia wa mambo unaoonekana waziwazi ndani ya uongozi wa juu wa chuo kikuu hiki. Tafakari, chukua hatua.
.............. hebu shauri mgao uweje !
 
Back
Top Bottom