Balozi Joy Mukanyange: Alichokiona, Watanzania Hatukukiona | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balozi Joy Mukanyange: Alichokiona, Watanzania Hatukukiona

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Oct 30, 2010.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Oct 30, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu Zangu,

  UZOEFU ni mwalimu mzuri. Unatufundisha, kuwa kuwasha moto ni jambo jepesi sana, lakini, kuuzima moto, yaweza kuwa ni kazi ngumu sana.
  Moto ulioanza kwenye nyumba moja ya nyasi kijijini, waweza kusambaa haraka na hata kuteketeza nyumba nyingine, mali na kuhatarisha maisha.


  Tumefundishwa, kuwa tusicheze na moto. Watanzania tunakwenda kupiga kura Jumapili Oktoba 31, 2010. Tunachokwenda kuamua ni mustakabali wa nchi yetu, taifa letu.
  Tunapokwenda kwenye uchaguzi tuyakumbuke maneno ya busara sana kutoka kwa Bi. Joy Mukanyange. Huyu alikuwa Balozi wa zamani wa Rwanda nchini Tanzania.
  Aprili 6, mwaka 1999 katika iliyokuwa Hoteli ya Kilimanjaro, Bi Joy Mukanyange alituambia Watanzania juu ya kile alichokiona lakini sisi Watanzania hatukukiona. Ilikuwa ni katika mjadala rasmi wa kumbukumbu ya maujai ya kimbari ya watu wa Rwanda ya mwaka 1994.
  Alisema: " Naogopa. Kwani nimeanza kuona dalili zinazojengeka za mgawanyiko wa kidini nchini Tanzania na eneo lote la Maziwa Makuu, hali ambayo inaweza kusababisha mauaji ya halaiki kama yale yaliyotokea nchini mwetu mwaka 1994," alisema Balozi huyo wa Rwanda kabla ya kuendelea kutoa ufafanuzi wa historia ya Rwanda na matukio yaliyosababisha mauji yale ya Wanyarwanda wao kwa wao. Ni kauli ya kuitafakari kwa makini.


  Watanzania tunakwenda kwenye uchaguzi. Katika chaguzi kuna kushinda na kushindwa. Wanaokwenda kushindana wajiandae na mawili; kushinda au kushindwa. Na mara nyingi wanadamu tumekuwa tukijiandaa zaidi na ushindi na si kupokea matokeo ya kushindwa. Hilo la mwisho ndilo huzua mfarakano na hata machafuko katika jamii.


  Kwa mara ya kwanza, tunakwenda kupiga kura huku nchi yetu ikiwa imepatwa na bahati mbaya ya baadhi ya Watanzania wenzetu kuanza kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwetu. Kuna wanaotaka tuanze kubaguana kwa misingi ya kidini. Hili ni jambo la hatari sana.


  Ni hulka ya mwanadamu, anapokuwa matatizoni humtafuta kondoo wa kafara. Mtu mwingine wa kummyooshea kidole kwa matatizo yake.Hali duni za maisha na umasikini wa watu wetu isiwe chachu ya kuanzisha vurugu za kijamii.


  Taratibu tumeanza kuizoea misamiati ya sisi na wao. Mathalan, sisi Wakristo na wao Waislamu. Sisi Wachagga na wao Wazaramo. Tunasahau, kuwa katika nchi yetu hii hakuna Sisi na Wao, kuna SISI tu.Tutakapokumbwa na maafa ya kitaifa watakaoathirika ni SISI, hakutakuwapo WAO.


  Hatari kubwa ninayoiona ni tatizo la baadhi ya Watanzania kuwa na ufahamu mdogo juu ya dunia tunayoishi sasa, kibaya zaidi,ufahamu mdogo wa historia yetu. Uelewa wa historia ya jamii husika ni jambo muhimu sana.


  Kiumbe huwezi kuelewa ya leo, kesho na kesho kutwa kama huelewi ya jana. Kuielewa historia yako ni kuelewa ulipo na unakokwenda. Historia ni kama maji ya mto, kamwe haijirudii. Historia ni wakati, ni muda. Kihistoria jana ni sawa na zamani.


  Karne nyingi zilizopita wahenga wetu walitafsiri muda kama mkusanyiko wa matukio ya zamani na sasa. Waliamini, kuwa yaliyotokea zamani na yanayotokea sasa ndiyo yenye kusaidia kubashiri yatakayotea kesho, yataamua mustakabali wetu.


  Dalili tunazoziona sasa za kupandikiza mbegu za chuki kwa misingi ya udini si dalili njema. Haya yatatupelekea kwenye maafa. Tuliopata bahati ya kutumia kalamu zetu hatuna budi kuliweka hili hadharani.


  Hii ni nchi yetu. Katika ulimwengu tunamoishi kuna mamilioni ya watu ambao hawana nchi. Wahenga wetu walishiriki katika kuijenga nchi hii, wametutarajia sisi tuendelee kuijenga na kuilinda hadhi ya nchi hii.


  Muda wetu wa kuishi humu duniani ni mfupi sana. Tuyachambue matatizo halisi ya jamii yetu. Kisha tusiishie kwenye kuyaorodhesha, hiyo ni kazi rahisi sana. Tutafute njia ya kuyatatua matatizo hayo.


  Kwenda kuwachagua viongozi bora na wenye kutambua umuhimu wa kuimarisha misingi ya umoja wetu wa kitaifa uwe ni wajibu wa wote wenye haki ya kupiga kura.
  Hatuna haja ya kubaguana kwa misingi ya ukabila, dini na rangi. Sisi wote ni Watanzania. Tuna historia ya kujivunia. Ni historia yetu wenyewe. Kinyume na baadhi yetu wanavyofikiri au wanavyotutaka tufikiri, historia yetu haikuanzia enzi za Mwarabu , Mjerumani au Mwingereza.  Historia yetu haikuanzia enzi za TANU wala Afro Shiraz.
  Historia ya nchi hii imeanzia kabla ya ujio wa Manabiii Yesu Kristo na Mtume Muhammad S.A.W. Kabla ya ujio wa Mwarabu na Mzungu. Hata mabingwa wa jiolojia (elimu ya viumbe) wamethibitisha kisayansi kuwa mtu wa kale zaidi hapa ulimwenguni aliishi katika nchi hii, Tanzania.


  Mtanzania halisi na mkweli kwa nchi yake atazungumzia matatizo ya Tanzania kwa ujumla wake. Hatakuwa na sababu ya kunyoosha kidole kwa Wahindi, Walutheli, Waprotestanti, Wasabato, Wakatoliki, Washia, Wasunni, Waismailia, wenye kuamini jadi, Wazaramo, Wagogo au Wachagga, kwamba ndio wa kulaumiwa.


  Wenye kuathirika na umasikini wa nchi hii ni wengi mno. Si Wakristo peke yao, si Waislamu peke yao, si Wapagani peke yao, si wamachinga peke yao na si Wazaramo peke yao.


  Wahenga walisema "kamba hukatikia pabovu". Kamwe huwezi kuwavuruga Watanzania na kuwafanya wachinjane kwa sababu za kudai kuna upendeleo wa ukabila au wa kisiasa. Nchi hii ina makabila zaidi ya 125 na utitiri wa vyama vya siasa.


  Mahala ambapo unaweza kuwagawa Watanzania na hata kufanikiwa wachinjane ni kwenye masuala ya imani. Tusikubali dini iwe ndiyo penye ubovu kwenye kamba inayotuunganisha Watanzania. Tuulinde umoja wetu wa kitaifa. Twendeni kupiga kura tukiitafakari Tanzania yetu.


  Maggid,
  Iringa, Jumamosi, Oktoba 30, 2010.  ( Makala yangu haya yalichapwa kwenye Raia Mwema ya juma hili)
   
 2. T

  The King JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaweza kututajia Watanzania hata wachache tu ambao wanapandikiza mbegu ya udini? Mimi nimefuatilia kampeni hizi tangu mwanzo mpaka mwisho na sikuona wala kusikia Mtanzania aliyepandikiza mbegu ya udini.
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Maggid pls, this is too low!
   
 4. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Maggid mbona makala zako zimejaa chuki dhidi ya wapenda mageuzi.Nakwambia endelea kupiga debe lako kesho watanzania watapiga kura kuondoa mafisadi madarakani.

  Kikwete na kikundi chake kidogo ameshindwa kulinda rasilimali zetu,ameshindwa kuwadhibiti wezi wa mali ya umma,ameshindwa na mwisho ameshindwa kuongoza taifa yote umegoma kuzumgumzia badala yake umekimbilia kuleta habari za udini hazina nafasi Tanzania.
   
 5. m

  maggid Verified User

  #5
  Oct 30, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kabonde,

  Hata mimi napenda mabadiliko. Sina ninayemchukia. Naipenda sana nchi niliyozaliwa, na niliyoyaandika ni fikra zangu huru. Nimesukumwa kuandika kutokana na mapenzi yangu kwa nchi niliyozaliwa. Kama hilo ni kosa, nitaendelea kulifanya.
   
 6. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2010
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Maggid,

  Nimesoma makala zako kibao hasa kipindi cha uchaguzi kiwango chako kimeshuka sana sijui mafisadi wamekukatia kido dogo
   
 7. T

  The King JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Eti una mapenzi na nchi? mapenzi gani uliyokuwa nayo kwa nchi? Sema una mapenzi kwa thithiem, usituletee usanii. :peace::peace::peace:
   
 8. m

  maggid Verified User

  #8
  Oct 30, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kabonde,
  Nafurahi kuwa umesoma makala zangu kibao. Ni ajabu kuwa unasema umesoma makala zangu kibao ikiwamo na hii ya leo. Bado Kabonde huyo huyo unadai kuwa kiwango changu kimeshuka! Nakushukuru sana kwa kuendendelea kunisoma.
   
 9. T

  The King JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Oh! Sasa unajifagilia! :nono::nono::nono: unataka akwambie nani kama kiwango chako kimeshuka ili umuamini? JK? Mimi sijui hata kama uliwahi kuwa na kiwango, labda cha kuandika pumba! Hebu tuondelee usanii wako hapa! :peace::peace::peace:
   
 10. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Mnazungumzia sana Udini, Ukabila ni kweli si mzuri kwa nchi yetu, but kama wote tunajua hayo tuwaadhibu wanaozungumzia mambo hayo, Hukumsikia hata JK alisema udini na ukabila upo kwenye vyombo vya habari! Inamaana kuwa nyinyi washika karamu ndo mnaleta upuuzi wenu huu! Halafu eti mnaipenda nchi???? acheni upumbavu huo bwana! Kama jk uwezo wake mdogo ni mdogo tuu si kwa sababu ni Muslim au Mkristo, na kama hajiwezi si sababu ni mkwele no! Ukweli ni kuwa jk aliharibu saaana miaka 5 iliyopita! ACHENI KUTUGOMBANISHA NYINYI! Sisi mtaani tupo na ndugu zetu wakristo na waislam hakuna hata siku moja nikasikia watu wamepigana bcs ya udini tunafanye sherehe pamoja na kushirikiana sana tuu! HAYO MNAYOYASEMA MNAYATOA WAPI?
  Watanzania tunajua kwa sasa adui yetu mkubwa ni UFISADI!
  Nyinyi mnakumbatia ufisadi unategemea nini!?
   
 11. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Maggid mimi binafsi sina tatizo na makala zako, ila nna tatizo na mtiririko especially hapa JF wakati huu wa kampeni. Kila mwenye akili na kusoma makala zako btn word and lines atagundua you have an agenda tht u r tryin to push thru. In fact you are not consistent juzijuzi tu ulikuwa unaua mdahalo wa Dr. Slaa pale movenpick lakini hatukusikii tena ukiongelea the same kuhusu wa Lipumba and the most boring one wa muungwana jana.

  At last unakuja na hii scaremongering techniq. By so saying haimaanishi nakubaliana na migogoro ya kidinik au kikabila whatsoever, ila wht I see ni kwamba hizi ni careful cultivations and seeding za chama tawala plus some journos. Toka kampeni zimeanza hatujamsikia Lipumba wala Slaa kukutana na viongozi wa dinik iwe kwa siri au hadharani lakini JK amefanya hivyo mara kadhaa and yet is the guy anakemea udini.

  To cut the long story short, my bro it is too late!
   
 12. c

  chanai JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii makala ni ya kuwasifia mafisadi. Hakuna lolote la maana
   
 13. Gottee

  Gottee Senior Member

  #13
  Oct 30, 2010
  Joined: Sep 7, 2008
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Yale yale ya TBC kuanza kuonyesha Wakimbizi! Hivi kweli Balozi wa Rwanda ndio anaweza kutufundisha ubaya wa Udini kweli? Maggid wanaoleta udini unajua kabisa hawako hapa WAFUATE huko waliko ukawaambie hapa unapoteza muda! How much are you getting for this? Hapa unajua kabisa CCM imekataliwa na CHADEMA imekubaliwa. Basi. Mapenzi na NCHI? Nchi gani? Labda Sweden!
   
 14. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ukiamua kulamba makalio ya mafisadi hatukuzuii lakini sisi hatutofanya hivyo. Go on poor journalist
   
 15. M

  Mamboleo Member

  #15
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 15
  Crap!
   
 16. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,920
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Too loo maggid!! Unauwa taaluma yako.
  Kama unakubali kutumiwa na mafisadi kupitia taaluma yako hufai kuitwa Mzalendo.
  Endapo Kikwete akabahatika Kushinda, Mateso tunayoyapata sisi watanzania, Laana zake zisiishie kwa Kikwete tu. Bali nawewe pia unayetumia taaluma yako kumuingiza tena Ikulu.
  Hebu niambie Ni lini umesikia Dr. au Prof. wakipanda Mbegu ya Udini kama sio JK anayeihubiri kwenye Campaign zake?
   
 17. Sidanganyiki10

  Sidanganyiki10 Member

  #17
  Oct 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 93
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maggid,
  Where is your theme?Selective objectivity?Hebu angalia migawanyiko mingine ya nchi hii kama Walalaheri,walalahai na walalahoi!Mafisadi dhidi ya waadilifu,wapenda mabadiliko dhidi ya status quo!english medium vs shule za kata n.k,n.k,n.k!
  Wake up!
   
 18. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kuna makundi mawili au matatu. Moja linapiga kampeni kwa issue ya "ufisadi, usafi na maendeleo" na kundi la pili linapiga kampeni kwa msingi wa "dini, undugu, ushirikina, kulindana na urafiki", kinachosemwa na kinachoenekana vinaweza kuwa tofauti na hali halisi. Lakini wenye macho huwa hawaambiwi tazama.
   
 19. Sidanganyiki10

  Sidanganyiki10 Member

  #19
  Oct 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 93
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maggid,
  Where is your theme?Selective objectivity?
  Hebu angalia migawanyiko mingine ya nchi hii kama Walalaheri,walalahai na walalahoi!Mafisadi dhidi ya waadilifu,wapenda mabadiliko dhidi ya status quo!english medium vs shule za kata n.k,n.k,n.k!
  Wake up!


  :israel:

  "True freedom must be expressed through the human ability to think critically, to analyze and to make informed decisions about oneself, his society and the world "- Sidanganyiki2010
   
 20. Power to the People

  Power to the People JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2010
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 1,193
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Damu itamwagika tz siku ambayo wasionacho watakasirika na kukosa matumaini kabisa ya kuishi baada ya kutumia kila mbinu mbadala kubadilisha maisha yao wakashinda huku wakiona wenzao watanzania kama wao wanapeta kwa raha zao huku wakila na kusaza kutokana na wizi wa rasilimali za raifa hili.
   
Loading...