Balozi Iddi akutana na Rais Magufuli leo, amhakikishia wanasubiri Tarehe ya Uchaguzi itangazwe

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Idd amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa hali ya Zanzibar ni shwari na Wazanzibar wanasubiri kutangaziwa tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi.

Balozi Seif Ali Idd ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es salaam leo tarehe 20 Januari, 2016 mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli.

"Mimi nimekuja kumpa taarifa juu ya hali yetu Zanzibar inavyokwenda, nimemueleza kwamba Zanzibar ipo salama, Zanzibar ina utulivu na ina amani, nimeona nije nimueleze kwa kuwa yeye ni kiongozi wetu" alisisitiza Balozi Seif Ali Idd.

Makamu huyo wa pili wa Zanzibar ameongeza kuwa kutokana na uwepo wa amani na utulivu, wananchi wa Zanzibar wanaendelea na shughuli zao kama kawaida tofauti na inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

"Hayo yanayoandikwa kwenye magazeti kuwa Zanzibar kuna fujo, Zanzibar kutatokea machafuko sio kweli, na kama unavyojua uchaguzi ulifutwa na tume ya uchaguzi na tunasubiri tarehe mpya ya uchaguzi itangazwe na tume ili tufanye uchaguzi" amebainisha Balozi Seif Ali Idd.

Gerson Msigwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam.
20 Januari, 2016.
 
Mmmh! mi najua utulivu uliopo ni kwa sababu ya mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea! ngoja tuone!!
 
Huo uchaguz utakua wa Rais peke yake au na wawakilishi??,,,,kwann wao wasiendelee kutawala wasiwachoshe wananchi.huku walishasema nchi ya kimapinduz haitwaliwi kwa karatasi.
 
Huyu jamaa katili kama anashika kijiti yeye bas ukija kumkosoa tu anaweza kukuondoa kabisa
 
Uchaguzi wa nini dkt Shein amesema yeye rais halali? Will dr Magufuli entertain this nonsense. Time will tell ,the stage is set for the Zanzibar re run farce.
 
Habari njema hii..! Wale maajenti wa fujo hawatapenda kuisikia kamwe! Ila habari ndiyo hiyo, Zanzibar iko tayari kwa uchaguzi huru na hali.
 
Atuji japo mnatusubiri ila atutafanya tena uchaguzi maana tulishafanya tangu tarehe 24-October-2015! Huo unao rudiwa ni CCM na si wawazanzibar.. Pia hata Pemba wasihangaike hatutapiga kura!
 
Ni unafiki kudai Zanzibar hali ni shwari wakati baadhi ya Wanzanzibar wanatembea na mabango ya kuitanganzia dunia kuwa kuna wengine wakuja hati siWazanzibar halisi, hati machotara wale na hati Zanzibar niya waafrika!! Huyo mzee anayasema hayo kuuhadaa umma tu na kulinda mkate wake kwafaida yake na kizazi chake, kwanza anatajwa kuwa mmoja wa wanaokwamisha muafaka Zanzibar na hajakanusha hilo. Lakini ukweli unabaki palepale zanzibari inanuka arufu ya damu.
 
Balozi Seif Alli Idd ni tatizo na kikwazo kikubwa kwa Demokrasia ya Zanzibar!
 
Miongoni mwa watu wanaojifanyia booking ya tiketi za kuwapeleleka kule The Hague Uholanzi kwa Bensouda, basi walio katika top of the list ni huyo Balozi Sefu Iddi na Dr Shein.

Maswali machache ya kuwauliza hao mahafidhina wa CCM:

1. Hiyo bajeti ya huo uchaguzi wa marudio ambayo huyo Balozi Sefu ameitaja kuwa ni shilingi bilioni 7, imepitishwa na Baraza lipi la Wawakilishi wakati lile lililopita lilishavunjwa tokea mwezi wa 8 mwaka jana na wakati yeye Balozi Sefu akijua kuwa kisheria hakuna uwezekano wa fungu kubwa la matumizi ya aina hiyo linalokuwa halali kutumika bila kupitishwa na Baraza la Wawakilishi?

2. Kama hata huyo mtu wao Jecha alipokuwa akiutangazia Umma wa watanzania na Jumuiya ya kimataifa kuufuta uchaguzi huo tarehe 28/10/2015 alitaja moja ya sababu kuu ya kuufuta uchaguzi huo kuwa ni wajumbe wa ZEC kutoelewana hadi kusababisha kupigana.
Sasa kama sababu aliyoitaja ni genuine, inawezekanaje Tume hiyo ya uchaguzi ya 'mabondia' iwe na credibility ya kuendesha uchaguzi wa marudio ulio huru na wa haki?

3. Tunaomba pia huyo Balozi Sefu Iddi atueleze kama anaona ulikuwepo uhalali wa kurejea uchaguzi huo, atutajie ni Ibara ipi ndani ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na kifungu kipi cha sheria katika Tume ya uchaguzi ya Zanzibar kinachompa huyo Jecha wao mamlaka ya kuufuta uchaguzi huo?


Wakati gazeti la Mawio likitoa tahadhari kwa yale yanayoweza kutokea Zanzibar kutokana na misimamo ya wahafidhina wa design ya watu wa aina hiyo ya akina Balozi Sefu Iddi, badala ya gazeti hilo kupongezwa kutokana na kutoa tip hiyo, badala yake gazeti hilo linapata kibano kwa kupigwa LIFE BAN na hao akina Jecha waliosababisha mkwamo huu wa kisiasa ambao haukupaswa kuwepo kwa kuwa uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana ulikuwa huru na wa haki kwa mujibu wa waangalizi wote wa ndani na nje ya nchi ndiyo wanaendelea kupeta uraiani!

Ni vyema basi hao viongozi wa wahafidhina ndani ya CCM Zanzibar wakautangazia Ulimwengu kuwa wanaufuta rasmi mfumo wa siasa wa vyama vingi badala ya kuwatesa watu wasimame kwenye mafoleni kwa masaa kadhaa kwa kuwa tayari wameshawahi kutamka hadharani kama ambavyo aliwahi kutamka kada wao Asha Bakari ndani ya BMK mwaka 2014 kuwa Zanzibar kamwe haitakuja kutolewa kwa vijikaratasi vya kupigia kura!
 
Hii taarifa ya Greyson Msigwa sijui kama ilitakiwa iwe kwa vyombo vya habari, hii imekaa ki chama zaidi na sio kiserikari
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Balozi Seif Ali Idd amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa hali ya Zanzibar ni shwari na Wazanzibar wanasubiri kutangaziwa tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi.

Balozi Seif Ali Idd ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es salaam leo tarehe 20 Januari, 2016 mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli.

"Mimi nimekuja kumpa taarifa juu ya hali yetu Zanzibar inavyokwenda, nimemueleza kwamba Zanzibar ipo salama, Zanzibar ina utulivu na ina amani, nimeona nije nimueleze kwa kuwa yeye ni kiongozi wetu" alisisitiza Balozi Seif Ali Idd.

Makamu huyo wa pili wa Zanzibar ameongeza kuwa kutokana na uwepo wa amani na utulivu, wananchi wa Zanzibar wanaendelea na shughuli zao kama kawaida tofauti na inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

"Hayo yanayoandikwa kwenye magazeti kuwa Zanzibar kuna fujo, Zanzibar kutatokea machafuko sio kweli, na kama unavyojua uchaguzi ulifutwa na tume ya uchaguzi na tunasubiri tarehe mpya ya uchaguzi itangazwe na tume ili tufanye uchaguzi" amebainisha Balozi Seif Ali Idd.

Gerson Msigwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam.
20 Januari, 2016.
Hii taarifa mbona haipo kiformat kama habari zingine zinazotoka Ikulu?,kulikuwa na uharaka gani kuiwahisha au imechukuliwa simple kwa sababu imebeba maudhui ambayo yanazisuta nafsi zao?
 
Leo ndio ni meamini ikulu hatuna mtu jamani kama ndio taarifa ya kichochezi inatoka ikulu kama ya greyson wajuwe watvuna wanachopanda watatawala kwa shida kuliko tawala zote zilizowahi kutawala upinzani umekomaa serikali imeanza kuzidisha taabu kwa wananchi shida kubwa
 
Yaani kama huo uchaguzi uliopita umefutwa kwa sababu zilizotajwa na ZEC, sitegemei kama huo wanao uorganize utafanyika. Maana wale vijana wa CUF wakiingia mtaani siku ya uchaguzi mpya, itakuwa ni vumbi tu Unguja! Hata robo ya wapiga kura haitajitokeza. Kwamaneno mengine utakuwa worst kuliko huu uliofutwa. Sijui CCM hawalijui hili au wana pesa nyingine za kuchezea?

Pemba ndio usiitaje kabisa katika uchaguzi wa marudio. Hiyo siku ya uchaguzi huenda ikawa ni siku ya vita kati ya polisi na raia.
Ukikosa uongozi wenye busara katika nchi, matokeo yake ni ufujaji wa pesa na mauaji yasiyokuwa na sababu za msingi. Ila hili kwa CCM inawezekana kwa vile wao ni one way thinking tu huwa hawafanyi simulation analysis katika vikao vyao. Wanafikiri watu wote wanafikiri kama wao!

Ngoja tuone, kama Zanzibar ni ya weusi tu peke yao. Wapuuzeni wazanzibari walio wengi kwa tamaa ya madaraka muone kama na wao ni binadamu kama hao CCM.
 
Back
Top Bottom