Dr. Lugano Wilson
New Member
- Jul 29, 2015
- 2
- 15
Nimesikitika kusikia kifo cha mzee Kaduma sikujua hata kama alikuwa hospitali, ikiwa ni siku chache nimetoka kushiriki msiba wa Shujaa aliyekuwa hajulikani Bi. Atupakisye Tumpange Mwaipopo kule mkoani Mbeya.
Nilimfahamu Mzee Ibrahim Kaduma kwa kukutana nae kwenye vikao , yeye na mimi tukiwa wajumbe wa Baraza la vyuo vikuu vilivyokuwa chini ya KKKT, mimi nikiingia kama statutory member, namkumbuka kwa mambo makubwa mawili , Mzee Kaduma yeye alisimamia mchakato wa mazungumzo na African Development Bank kusaidia kuanzisha bodi ya mikopo ya Elimu ya juu ambayo ingekuwa chini ya mwamvuli huo ili kuwasaidia vijana ambao walikuwa wakikosa mkopo HESLB au waliokuwa waki yaipata pungufu ya 100%.
Alisadia kuandaa document na kuipigia debe pendekezo hilo mbele ya wajumbe wakiwemo maaskofu wa dayosisi mbali mbali nchi nzima na marais(student unions) na maprofesa wa vyuo vikuu husika.
Mchakato uliiva , na wajumbe wengine tuliufurahia, lakini kwa bahati mbaya ulikuja kukwama katika hatua za mwisho baada ya kushindwa kuelewana kwenye baadhi ya mambo ikiwemo mgawanyo wa Hisa.
Mbali na hilo, mzee kaduma alipenda maendeleo na alitufundisha maraisi wa vyuo vikuu maadili, na alikuwa very social, nakumbuka kila baada ya vikao kuna wakati walikuwa akikaa nasi akitufundisha kuhusu maadili, na katika mazungumzo yake alioonesha alichukia rushwa.
Mungu ailaze roho ya mahali pema peponi.
Nenda mzee Kaduma.
Nawasilisha.
Lugano Wilson.