Balozi Hamis Kagasheki, familia yake na siasa za CCM Bukoba mjini!

Status
Not open for further replies.
Mkuu Jasusi,kwenye ka red hapo,sio kwamba 'pesa ni sabuni ya roho'?
Wahaya wanasema 'ekyalema amahela naga ( meaning 'kisichonunulika tupilia mbali hakifai').

Bishanga;
Ahaa haaa sasa tunafahamu kwa nini yule dada kaamua kuolewa na baba yake ili amazalie mjukuu; lakini una uhakika na hii tafsiri?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Jamani haya mambo mbona yapo karibia vyama vyote vya siasa hapa nchini! Ila ni kwa sababu kimoja kipo madarakani ndo mana haya yanaonekana sana, ila hata wapinzani wakichukua nchi haya yote yataonekana, mbona hata wengine wamejazana kwenye nafasi za chama na ni ndugu ndugu wengine na wake zao kabisa. Wachaga mbona wameteuana kwamba wao ndo watoza kodi wa hii nchi, na wanarisishana tu. Mbona hata huko marekani kuna wakina clinton na mambo kama haya, mbona wingereza wanarisishana sana tu, haya mambo yamejaa dunia nzima tangu zamani!
 
mimi naona kama wanafanya kazi zao vizuri na kama kulikua hakuna upendeleo wowote kwenye mchakato wa kugombania vyeo mimi sina shida. tunaona wakina george bush mkubwa na mtoto wote walikua marais. hata obama mtoto wake inasemekana anapenda siasa. unadhani democrats wanaweza kumzuia huko baadae.

Ndio maana wakati ule 92008) Bi Clinton akitafuta kuteuliwa kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Democrats nilikuwa ninaomba sala asipitishwe - na kweli muumba alisikia sala zangu. Kwa sababu baada ya muda si mrefu tungesikia watawala wetu wa Afrika wakiwarithisha urais wake zao kwa kutumia sababu hizo hizo - eti mbona Marekani wanafanya hivyo. Wamerkani wakitembea uchi, basi nasi tunajibwaga barabarani uchi tukiimba mbona na Wamarekani wanafanya hivyo - n.y.m.b.a.f.u
 
Inawezekana katika utafiti aliofanya amegundua kuwa maneno hayo ndiyo wapiga kura wake wanataka kusikia.
 
Ndio maana wakati ule 92008) Bi Clinton akitafuta kuteuliwa kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Democrats nilikuwa ninaomba sala asipitishwe - na kweli muumba alisikia sala zangu. Kwa sababu baada ya muda si mrefu tungesikia watawala wetu wa Afrika wakiwarithisha urais wake zao kwa kutumia sababu hizo hizo - eti mbona Marekani wanafanya hivyo. Wamerkani wakitembea uchi, basi nasi tunajibwaga barabarani uchi tukiimba mbona na Wamarekani wanafanya hivyo - n.y.m.b.a.f.u
democracy ilianzishwa america kama ulikua ujui. ndo maana nilitolea hiyo mifano. naelewa kwasababu gani umekasirika hii ishu ya familia moja kupata vyeo. lakini kumbuka kwamba hamna sheria inayo mkataza mtu kugombania vyeo kisiasa kwasababu ana ndugu mwenye madaraka.
Kwa mgombea uraisi hana budi kuwa ametimiza yafuatayo:

  1. Awe mtanzania
  2. Awe ametimiza miaka 40 na kuendelea
  3. Awe hajawahi kuhukumiwa makosa ya jinai na mauaji
  4. Awe na wanachama waliojiandikisha katika daftari la kupiga kura wasiopungua 200 kwa mikoa 10 ya Tanzania ikiwemo miwili ya Tanzania visiwani.
  5. Awe amelipia shilingi 100,000/=kwa ajili ya fomu
  6. Fomu yake iwe imesainiwa na kupigwa muhuri wa hakimu
  7. Arudishe fomu yake katika tume ya uchaguzi kabla ya saa kumi kamili alasiri siku iliyopangwa
  8. Fomu inapatikana katika ofisi ya tume ya taifa ya uchaguzi

Kwa mgombea ubunge na udiwani hana budi awe ametimiza yafuatayo:

  1. Awe mtanzania
  2. Awe ametimiza miaka 21 na kuendelea
  3. Awe anaweza kusoma na kuandika Kiswahili na kingereza
  4. Awe na wadhamini wasiopungua 25 na wamejiandikisha katika daftari la kupiga kura
  5. Awe amelipia shilingi 50,000 kwa ajili ya fomu ya kugombea
  6. Fomu iwe imesainiwa na kugongwa muhuri wa hakimu mkazi wa halmashauri ya manispaa husika
  7. Awe ana picha 4 za pasipoti
  8. Fomu aridishe kabla ya saa kumi kamili alasiri
 
Unashangaa nini wakati huu ndo utamaduni wa CCM?

Angalia Mwinyi, Karume, Nyerere, Kawawa, Malima,Makamba etc wote wanarithishana vyeo tu.

Huu ulimbukeni unaonyesha watu hawana kazi hawa.

Please please Nyerere aondolewe kwenye huu uroho wa madaraka
 
kagasheki sio tu msomi ni mwanabalozi aliebobea na kakaa njema ya nchini sana kutumikia wabongo, awezi kuongea upuuzi kama huo, wewe kamasio cdm basi mchagga.

Mnapenda sana kugombanisha makabila...!! Kama unasema Wachagga wapuuzi basi utakuwa uwaelewi wachagga. Ebu niambie uliona wapi Mpuuzi anafanya kazi kwa bidii, anakumbuka kwao na kujali ndugu zake ...!?

Nadhani hapo kwenye red ulipitiwa.

Mimi sio mchagga.
 
Jamani haya mambo mbona yapo karibia vyama vyote vya siasa hapa nchini! Ila ni kwa sababu kimoja kipo madarakani ndo mana haya yanaonekana sana, ila hata wapinzani wakichukua nchi haya yote yataonekana, mbona hata wengine wamejazana kwenye nafasi za chama na ni ndugu ndugu wengine na wake zao kabisa. Wachaga mbona wameteuana kwamba wao ndo watoza kodi wa hii nchi, na wanarisishana tu. Mbona hata huko marekani kuna wakina clinton na mambo kama haya, mbona wingereza wanarisishana sana tu, haya mambo yamejaa dunia nzima tangu zamani!

Kwa mtu anayefahamu wanamageuzi wa nchi hii magumu wameyapitia kufika hapa tulipo,atakua mtu wa mwisho kuvilaumu vyama vya upinzani. Katika mazingira ambayo watu waliogopa hata kuonekana ni ndugu ama marafiki wa ndugu ambaye yupo upinzani,basi ilihitaji familia jasiri na watu wa jamii jasiri kuwepo upinzani! Hii ni tofauti za chama dola kama CCM kujazana wanafamilia ktk uongozi wa chama. Hawana sababu za msingi,bali ni kuonyesha moja ya dalili za mwisho kwa chama kikongwe kinapokaribia kuondolewa madarakani na hata kufa!
 
Balozi Kagasheki ni mbunge wa Bukoba mjini. Abubakari Kagasheki ni mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa Wilaya ya Bukoba Mjini, jumuiya iliyoko chini ya CCM. Abdul Kagasheki anagombea awe Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kutokea Bukoba Mjini. Suedi Kagasheki anagombea awe mjumbe wa kuwakilisha Wilaya kwenye Mkutano Mkuu wa CCM Taifa tokea Bukoba Mjini.

Katika hotuba yake kwa wajumbe waliomchagua Abubakari Kagasheki, amesema na ninamnukuu, " Nawashukuru familia yangu kwa kuniwezesha Kwa hali na mali katika uchaguzi huu. Kwa namna ya pekee niwashukuru Abdul Kagasheki na Hamis Kagasheki kwa kuniwezesha kwa hali na mali kushinda uchaguzi huu.

Ndugu wajumbe, Familia yetu inayo historia kubwa katika CCM kiasi kwamba Marehemu Baba wa Taifa akidai Uhuru alilala kwa Baba yangu, na ndio maana hivi karibuni niliitwa Ikulu kwa ajili ya kupokea nishani iliyotolewa na rais kwa ajiri ya baba yangu. Hivyo Familia yetu inaijua CCM zaidi ya yeyote katika wilaya hii.Hivyo mtu wa FAMILIA YETU AKIGOMBEA TUTA HAKIKISHA ANAPITA KWA NJIA YOYOTE ILE" mwisho wa kunukuu.

Wanachama, wadau, na wakereketwa wa CCM Wilayani Hapa wamebaki na bumbuwazi na kujiuliza HIVI SIASA ZA CCM BUKOBA MJINI KUHODHIWA NA FAMILIA MOJA, ni kwa ajili ya MASLAHI YA CHAMA, WANACHAMA NA TAIFA AU NI ZA KUJINUFAISHA BINAFSI? NA JE, KWA VITISHO HIVI CHAMA BUKOBA MJINI KINA ELEKEA WAPI?

Kwa definition ya familia hiyo si familia moja kwa kuwa kila mmoja ana familia yake labda kama ungesema ndugu moja maana hapo kila mtu ana mke na watoto hivyo wameunda familia kila mmoja
 
Jamani haya mambo mbona yapo karibia vyama vyote vya siasa hapa nchini! Ila ni kwa sababu kimoja kipo madarakani ndo mana haya yanaonekana sana, ila hata wapinzani wakichukua nchi haya yote yataonekana, mbona hata wengine wamejazana kwenye nafasi za chama na ni ndugu ndugu wengine na wake zao kabisa. Wachaga mbona wameteuana kwamba wao ndo watoza kodi wa hii nchi, na wanarisishana tu. Mbona hata huko marekani kuna wakina clinton na mambo kama haya, mbona wingereza wanarisishana sana tu, haya mambo yamejaa dunia nzima tangu zamani!

Kwa hiyo haya yote kwako ni sawa tu. Kwenye nyekundu hawarithishani pale ni kisomo na utendaji wenye tija ndivyo vinavyotawala. Nani kapewa kazi bila kukidhi mahitaji ya kitaaluma na uchapa kazi wenye tija? Tena kwa kupitia usaili mkali. Unaonaje ungewataja ili umma uwafahamu washughulikiwe!! Tena uache kabisa sumu ya ukabila kwa maana itakuua bure! USHAURI WA BURE: Nenda shule na ndugu zako mkasome masomo yanayohusu kodi kwa bidii mje na nyie kutoza kodi.
 
democracy ilianzishwa america kama ulikua ujui. ndo maana nilitolea hiyo mifano. naelewa kwasababu gani umekasirika hii ishu ya familia moja kupata vyeo. lakini kumbuka kwamba hamna sheria inayo mkataza mtu kugombania vyeo kisiasa kwasababu ana ndugu mwenye madaraka.
Kwa mgombea uraisi hana budi kuwa ametimiza yafuatayo:

  1. Awe mtanzania
  2. Awe ametimiza miaka 40 na kuendelea
  3. Awe hajawahi kuhukumiwa makosa ya jinai na mauaji
  4. Awe na wanachama waliojiandikisha katika daftari la kupiga kura wasiopungua 200 kwa mikoa 10 ya Tanzania ikiwemo miwili ya Tanzania visiwani.
  5. Awe amelipia shilingi 100,000/=kwa ajili ya fomu
  6. Fomu yake iwe imesainiwa na kupigwa muhuri wa hakimu
  7. Arudishe fomu yake katika tume ya uchaguzi kabla ya saa kumi kamili alasiri siku iliyopangwa
  8. Fomu inapatikana katika ofisi ya tume ya taifa ya uchaguzi

Kwa mgombea ubunge na udiwani hana budi awe ametimiza yafuatayo:

  1. Awe mtanzania
  2. Awe ametimiza miaka 21 na kuendelea
  3. Awe anaweza kusoma na kuandika Kiswahili na kingereza
  4. Awe na wadhamini wasiopungua 25 na wamejiandikisha katika daftari la kupiga kura
  5. Awe amelipia shilingi 50,000 kwa ajili ya fomu ya kugombea
  6. Fomu iwe imesainiwa na kugongwa muhuri wa hakimu mkazi wa halmashauri ya manispaa husika
  7. Awe ana picha 4 za pasipoti
  8. Fomu aridishe kabla ya saa kumi kamili alasiri
Sahihisho dogo tu: Demokrasia haikuanzia Amerika. Ilianzia Ugiriki.
 
Watanzania tuwe makini kuwachunguza watawala wetu kabla ya kuanza kuwapamba na kuwasifia sifa wasiokuwa nazo. Shule ya Kagasheki ni ya kawaida sana,aliweza panda na kupewa hadhi ya ubalozi kwasababu ya mahusiano ya kifamilia na Rais Mwinyi. Aliondoka Uswizi na kuja kugombea ubunge wa Bukoba,baada ya scandal kubwa ya wizi wa pesa ktk shirika la WIPO alikokua mmoja wa wakurugenzi waliotuhumiwa kuiba pesa. Nawashangaa sana wale wanaotarajia huyu jamaa apambane na rushwa za Maliasili na Utalii. Anazo pesa nyingi,wapinzani wake wasiojiweka sawa atawajaza ndugu zake!

kiongozi, hizi tuhuma ulizomwaga hapa unaushahidi mpya? manake hili suala la wipo lilipata zungumzwa hapa jamvini
na watu wakashindwa kutoa maelezo mazuri kuhusu hizo tuhuma. sasa wewe kama umepata ushahidi mpya hebu zimwage hapa. kuhusu ubalozi je unahakika kwamba hakuwa amefika ngazi ya kuteuliwa ubalozi? kumbuka mambo yaa nje balozi ni ngazi ya ukurugenzi.
 
Je, mnahabari kuwa huko alikokuwa anafanya hizo kazi zenu za UBALOZI alifukuzwa kazi kwa ubadhirifu???

kagasheki hakuwahi kuwa balozi wa kituo. aidha sidhani kama ni sahihi kusema alifukuzwa kazi kwani hajapata fukuzwa kazi "za ubalozi"
 
Kagasheki amefika pale kutokana na kuoa kwa Mwinyi na si uhusiano wa baba yake na Mwalimu Nyerere. Nyerere hakuwa mpuuzi kiasi hicho. Hapa anatumiwa kwa vile hayuko hai kujitetea. Huyu naye ni gamba ndiyo maana ameshupalia ufisadi mbuga za wanyama akiacha ule uliotendwa na baba mkwe wake na Muhidin Ndolanga kwenye kashfa ya Loliondo iliyouza mbuga zetu kwa waarabu. Shame on you! Anachohubiri Kagasheki ni nepotism.
 
Sahihisho dogo tu: Demokrasia haikuanzia Amerika. Ilianzia Ugiriki.
jasusi kuna nchi gani inayotumia demokrasia ya ugiriki. amerika ndo inchi ya kwanza kua na demokrasia ambayo ipo dunia nzima [ kwa sasa]. huwezi kuniambia demokrasia ya ugiriki ndo inatumika tanzania na nchi zingine duniani. ni kweli demokrasia ilianza ugiriki
 
kagasheki hakuwahi kuwa balozi wa kituo. aidha sidhani kama ni sahihi kusema alifukuzwa kazi kwani hajapata fukuzwa kazi "za ubalozi"

Kama hujui kaa kimya waachie watu wa wizara ya mambo ya nje waje wafunguke hapa; kweli alikuwa hana kituo lakini alikuwa anafanya kwenye taasisi [WIPO] iliyompa hiyo hadhi yenu ya ubalozi!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom