Balozi Hamis Kagasheki, familia yake na siasa za CCM Bukoba mjini!

Status
Not open for further replies.
Another input, wakati anagombea ubunge kwa mara ya kwanza, baba yake JK Nyerere akihutubia alishangaa na kuuliza hivi kweli mnataka kumpa Makongoro ubunge, kweli Makongoro, lakini jamaa akachaguliwa.
 
Love it folk. Umenikumbusha mbali kwa list hiyo.

Ni utamaduni wa CCM kuhodhi na kujimilkilisha. Ni utamaduni wao wa ki-sultan na wa kifsadi uliosisiwa na kushamiri miaka ya 80'. Mfumo wao huo ndio unaoifanya CCM ife mbele ya macho yetu kama ilivyo leo. Ni ushahidi mwingine wa nzi kufia kwenye kidonda.
 
Hakuna cha ajabu, siko familia kibao za kisiasa duniani, kuna kina Kenedies na Bush US, Gadhi, India, Marcos na Aquino, Bandaranike, Castros, Kenyettas, Karumes, Mwinyis, Kikwetes, coming down to Kagashekis etc, mimi nina rafiki yangu mmoja kwa jina la Alfred Mwambeleko, Babu yake alikuwa TAA, Baba yake alikuwa kiongozi wa TANU, yeye alizaliwa CCM, ameshika uongozi chipukizi, then UVCC sasa anaelekea CCM Taifa, mwanae ni kiongozi wa Chipukizi na mkewe ni kiongozi wa UWT!.

Tuyaseme tuu haya ya CCM, lakini haya mengine...kama ...
Kuna chama kiongozi wake ni mkwe wa muasisi, kuna watu mule bungeni wako chama kimoja na wake zao, na wadogo zao na wazazi wao, au wazazi na watoto wao hadi na vimada wao, tunawaona tuu lakini wao hatuwasemi as if its the right thing na wole waliomo is their right kuwemo!.!.
 
nimeipenda hii FAMILIA YETU AKIGOMBEA TUTA HAKIKISHA ANAPITA KWA NJIA YOYOTE ILE"
 
Nakubaliana na Kiranga kwa observation yake hiyo. Kwamba as long as jina la baba yako likitokea katika utawala wa nchi hii, then it almost becomes hereditary kwamba nawe utaingia katika siasa. Na in an even bigger picutre ni kwamba huo utamaduni kwa sasa unaanza kupindukia mpaka upinzani.
 
Correction: Nyerere akiwa hai hakurithisha mtoto wake hata mmoja cheo. Makongoro amepata ubunge Arusha kwa kutegemea kura za "walevi" wenzake. Amepata uenyekiti wa CCM mkoa wa Mara licha ya kwamba Lowassa alimwaga shillingi milioni 300 kumwangusha. Amepata ubunge wa Afrika mashariki bila kuhonga hata senti tano, tofauti na kijana wa Malecela. It is a minor correction but heavy.

good correction.si dhani kama nyerere aliamini katika kurithisha wanae.
 
Naongelea utamaduni wa kurithishana vyeo katika chama cha CCM, regardless ya Nyerere kataka hilo au la.

Halafu Nyerere is not above nepotism, sie yeye aliyewajaza Wakurya jeshini na Wazanaki usalama wa Taifa?

Rosemary Nyerere hajawahi kuwa mbunge wa viti maalum wakati wa uhai wa Nyerere?

Wkt hao wanapata hizo fursa, Nyerere hakuwa madarakani,
wala hawakuzipata kwa msaada wake.
 
Back to the big picture assesment, utamaduni wa kurithishana vyeo CCM kama sehemu ya "kuzawadiana" ni systemic.

Ndo maana unakuta kina Karume wamepewa urais na ubalozi.

Mwinyi kapewa uwaziri.

Kina Nyerere wamepewa ubunge several times. Ditto Kawawa, Malima, Makamba etc.

Sasa mpaka kina Le Mutuz wanajisikia entitled simply because ya jina la baba wakati hata kujieleza tu, achilia mbali kucheza underwater 3D Chess, hawawezi.

Kwa hiyo hawa kina Kagasheki hiyo impunity naweza kusema ni tacky, na labda wanazidisha tulivyozoea, lakini bottom line ni kwamba wanatekeleza utamaduni wa CCM tu.

Ebu tujikite na fursa na madhara ya utaratibu huo. Fursa niionayo ni kujiona mwenyewe nisivyo na kauli juu ya mstabali wa uongozi nchini. Baada ya kijiona napata fursa ya kukataa kila kitu cha upuuzi huu. Madhara yako mengi, la kwanza ni ombwe la uongozi na matokeo yake ni vurugu zinazoendelea.

Kwa hali ya utandawazi ilipofikia hawawezi kujificha po pote na kwa kauli yo yote.
 
Correction: Nyerere akiwa hai hakurithisha mtoto wake hata mmoja cheo. Makongoro amepata ubunge Arusha kwa kutegemea kura za "walevi" wenzake. Amepata uenyekiti wa CCM mkoa wa Mara licha ya kwamba Lowassa alimwaga shillingi milioni 300 kumwangusha. Amepata ubunge wa Afrika mashariki bila kuhonga hata senti tano, tofauti na kijana wa Malecela. It is a minor correction but heavy.

Nyongeza.......kwa kupitia NCCR-Mageuzi na sio CCM (Baba yake akiwa hai)
 
Balozi Kagasheki ni mbunge wa Bukoba mjini. Abubakari Kagasheki ni mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa Wilaya ya Bukoba Mjini, jumuiya iliyoko chini ya CCM. Abdul Kagasheki anagombea awe Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kutokea Bukoba Mjini. Suedi Kagasheki anagombea awe mjumbe wa kuwakilisha Wilaya kwenye Mkutano Mkuu wa CCM Taifa tokea Bukoba Mjini.

Katika hotuba yake kwa wajumbe waliomchagua Abubakari Kagasheki, amesema na ninamnukuu, " Nawashukuru familia yangu kwa kuniwezesha Kwa hali na mali katika uchaguzi huu. Kwa namna ya pekee niwashukuru Abdul Kagasheki na Hamis Kagasheki kwa kuniwezesha kwa hali na mali kushinda uchaguzi huu.

Ndugu wajumbe, Familia yetu inayo historia kubwa katika CCM kiasi kwamba Marehemu Baba wa Taifa akidai Uhuru alilala kwa Baba yangu, na ndio maana hivi karibuni niliitwa Ikulu kwa ajili ya kupokea nishani iliyotolewa na rais kwa ajiri ya baba yangu. Hivyo Familia yetu inaijua CCM zaidi ya yeyote katika wilaya hii.Hivyo mtu wa FAMILIA YETU AKIGOMBEA TUTA HAKIKISHA ANAPITA KWA NJIA YOYOTE ILE" mwisho wa kunukuu.

Wanachama, wadau, na wakereketwa wa CCM Wilayani Hapa wamebaki na bumbuwazi na kujiuliza HIVI SIASA ZA CCM BUKOBA MJINI KUHODHIWA NA FAMILIA MOJA, ni kwa ajili ya MASLAHI YA CHAMA, WANACHAMA NA TAIFA AU NI ZA KUJINUFAISHA BINAFSI? NA JE, KWA VITISHO HIVI CHAMA BUKOBA MJINI KINA ELEKEA WAPI?

Chama Cha MA-KAGASHEKI
 
mimi naona kama wanafanya kazi zao vizuri na kama kulikua hakuna upendeleo wowote kwenye mchakato wa kugombania vyeo mimi sina shida. tunaona wakina george bush mkubwa na mtoto wote walikua marais. hata obama mtoto wake inasemekana anapenda siasa. unadhani democrats wanaweza kumzuia huko baadae.
 
Kiranga,
Kwa Wakurya kujaa jeshini unamwonea Nyerere. In fact ni Nyerere ndiye aliyefungua milango ya kuandikisha vijana wa Kichagga na makabila mengine jeshini. Kabla ya hapo, enzi za Mwingereza, jeshi lilijaa Wakurya na Wanyakyusa. Ngoja nikupe historia ya usalama wa taifa. Hii department kwa muda mrefu ilikuwa chini ya Kambona mpaka mwaka 1967 ndipo ikawekwa chini ya Kawawa. Maafisa wote wa ngazi za juu walitoka kusini kuanzia mzee Mzena, Mahiga, Kitine, hata Apson. Aliyeandikisha vijana wa kizanaki, ambao pia hawakuwa wengi ni mwalimu mmoja wa Kisukuma (nimesahau jina lake,) alifundisha pale Musoma Alliance. Alipojiunga na usalama wa taifa alichukua wanafunzi wake wengi kama recruits na ndipo rafiki zangu wengi wa Kizanaki wakaajiriwa kule. Rose Nyerere aliteuliwa mbunge wa viti maalumu na Mkapa baada ya kifo cha Nyerere, not before.

Jasusi - ongeza na Dr. Gama hapa kwenye list, naye ni kusini.ila big up, sina pc ninge-ku like, kwa ku set record right mana kuna watu kila mara kutaka tu kumchanganya Mwalimu na majuha!
 
Correction: Nyerere akiwa hai hakurithisha mtoto wake hata mmoja cheo. Makongoro amepata ubunge Arusha kwa kutegemea kura za "walevi" wenzake. Amepata uenyekiti wa CCM mkoa wa Mara licha ya kwamba Lowassa alimwaga shillingi milioni 300 kumwangusha. Amepata ubunge wa Afrika mashariki bila kuhonga hata senti tano, tofauti na kijana wa Malecela. It is a minor correction but heavy.

Uko sahihi Jasusi mwalimu hakumrithisha hata mwanae mmoja cheo, in fact mwalimu aliwashangaa wananchi wa Arusha kwa kumchagua Makongoro na kumuacha Mtei!!! Kuhusu uchaguzi wa ubunge wa Afrika Mashariki ni kweli yeye binafsi hakuhonga lakini kuna MAFISADI toka mkoa wa Mara ambao hawataki Makongoro aendelee na uenyekiti wa Mkoa ndio waliohonga on his behalf wakidhani akichaguliwa ataachia kiti cha uenyekiti wa Mkoa. Uwepo wake kwenye NEC ya magamba kunawatesa sana!!
 
kagasheki sio tu msomi ni mwanabalozi aliebobea na kakaa njema ya nchini sana kutumikia wabongo, awezi kuongea upuuzi kama huo, wewe kamasio cdm basi mchagga.

Je, mnahabari kuwa huko alikokuwa anafanya hizo kazi zenu za UBALOZI alifukuzwa kazi kwa ubadhirifu???
 
Mkuu Jasusi,kwenye ka red hapo,sio kwamba 'pesa ni sabuni ya roho'?
Wahaya wanasema 'ekyalema amahela naga ( meaning 'kisichonunulika tupilia mbali hakifai').

Hee umefikaje huku Bishanga? au kwa vile inahusu wahaya wenzio?
 
Last edited by a moderator:
Mjukuu akifuata nyayo za babu yake au baba yake kwa nia nzuri,kuna shida gani?Nani alikwambia kuwa kuna ukomo wa wa familia mmoja kuwania mamlaka ya kisiasa? Kuna mifano hai ya koo za Kennedy na Bush.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom