Balozi Hamis Kagasheki, familia yake na siasa za CCM Bukoba mjini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balozi Hamis Kagasheki, familia yake na siasa za CCM Bukoba mjini!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PROF. MASHANKARA, Aug 28, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. P

  PROF. MASHANKARA New Member

  #1
  Aug 28, 2012
  Joined: Aug 28, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Balozi Kagasheki ni mbunge wa Bukoba mjini. Abubakari Kagasheki ni mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa Wilaya ya Bukoba Mjini, jumuiya iliyoko chini ya CCM. Abdul Kagasheki anagombea awe Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kutokea Bukoba Mjini. Suedi Kagasheki anagombea awe mjumbe wa kuwakilisha Wilaya kwenye Mkutano Mkuu wa CCM Taifa tokea Bukoba Mjini.

  Katika hotuba yake kwa wajumbe waliomchagua Abubakari Kagasheki, amesema na ninamnukuu, " Nawashukuru familia yangu kwa kuniwezesha Kwa hali na mali katika uchaguzi huu. Kwa namna ya pekee niwashukuru Abdul Kagasheki na Hamis Kagasheki kwa kuniwezesha kwa hali na mali kushinda uchaguzi huu.

  Ndugu wajumbe, Familia yetu inayo historia kubwa katika CCM kiasi kwamba Marehemu Baba wa Taifa akidai Uhuru alilala kwa Baba yangu, na ndio maana hivi karibuni niliitwa Ikulu kwa ajili ya kupokea nishani iliyotolewa na rais kwa ajiri ya baba yangu. Hivyo Familia yetu inaijua CCM zaidi ya yeyote katika wilaya hii.Hivyo mtu wa FAMILIA YETU AKIGOMBEA TUTA HAKIKISHA ANAPITA KWA NJIA YOYOTE ILE" mwisho wa kunukuu.

  Wanachama, wadau, na wakereketwa wa CCM Wilayani Hapa wamebaki na bumbuwazi na kujiuliza HIVI SIASA ZA CCM BUKOBA MJINI KUHODHIWA NA FAMILIA MOJA, ni kwa ajili ya MASLAHI YA CHAMA, WANACHAMA NA TAIFA AU NI ZA KUJINUFAISHA BINAFSI? NA JE, KWA VITISHO HIVI CHAMA BUKOBA MJINI KINA ELEKEA WAPI?
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Unashangaa nini wakati huu ndo utamaduni wa CCM?

  Angalia Mwinyi, Karume, Nyerere, Kawawa, Malima,Makamba etc wote wanarithishana vyeo tu.

  Huu ulimbukeni unaonyesha watu hawana kazi hawa.
   
 3. B

  BULOLE BUKOMBE JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2012
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kaburini
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Correction: Nyerere akiwa hai hakurithisha mtoto wake hata mmoja cheo. Makongoro amepata ubunge Arusha kwa kutegemea kura za "walevi" wenzake. Amepata uenyekiti wa CCM mkoa wa Mara licha ya kwamba Lowassa alimwaga shillingi milioni 300 kumwangusha. Amepata ubunge wa Afrika mashariki bila kuhonga hata senti tano, tofauti na kijana wa Malecela. It is a minor correction but heavy.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  mmm...!
   
 6. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Yeah! Kuna binti mmoja, Sofia Kagasheki nilikuwa naye O level baadae nilikuwa naye chuo; thereafter alikwenda Uturuki. Amerudi na anaandaliwa kuwa MP kwa tiketi ya sisiemu! Si ajabu, historia inajirudia.
   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Naongelea utamaduni wa kurithishana vyeo katika chama cha CCM, regardless ya Nyerere kataka hilo au la.

  Halafu Nyerere is not above nepotism, sie yeye aliyewajaza Wakurya jeshini na Wazanaki usalama wa Taifa?

  Rosemary Nyerere hajawahi kuwa mbunge wa viti maalum wakati wa uhai wa Nyerere?
   
 8. patience96

  patience96 JF-Expert Member

  #8
  Aug 28, 2012
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 1,187
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Alijaza Wakerewe (Mkerebe ni mpele); wala si Wazanaki (umekuja na nini?).
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Aug 28, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kiranga,
  Kwa Wakurya kujaa jeshini unamwonea Nyerere. In fact ni Nyerere ndiye aliyefungua milango ya kuandikisha vijana wa Kichagga na makabila mengine jeshini. Kabla ya hapo, enzi za Mwingereza, jeshi lilijaa Wakurya na Wanyakyusa. Ngoja nikupe historia ya usalama wa taifa. Hii department kwa muda mrefu ilikuwa chini ya Kambona mpaka mwaka 1967 ndipo ikawekwa chini ya Kawawa. Maafisa wote wa ngazi za juu walitoka kusini kuanzia mzee Mzena, Mahiga, Kitine, hata Apson. Aliyeandikisha vijana wa kizanaki, ambao pia hawakuwa wengi ni mwalimu mmoja wa Kisukuma (nimesahau jina lake,) alifundisha pale Musoma Alliance. Alipojiunga na usalama wa taifa alichukua wanafunzi wake wengi kama recruits na ndipo rafiki zangu wengi wa Kizanaki wakaajiriwa kule. Rose Nyerere aliteuliwa mbunge wa viti maalumu na Mkapa baada ya kifo cha Nyerere, not before.
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Back to the big picture assesment, utamaduni wa kurithishana vyeo CCM kama sehemu ya "kuzawadiana" ni systemic.

  Ndo maana unakuta kina Karume wamepewa urais na ubalozi.

  Mwinyi kapewa uwaziri.

  Kina Nyerere wamepewa ubunge several times. Ditto Kawawa, Malima, Makamba etc.

  Sasa mpaka kina Le Mutuz wanajisikia entitled simply because ya jina la baba wakati hata kujieleza tu, achilia mbali kucheza underwater 3D Chess, hawawezi.

  Kwa hiyo hawa kina Kagasheki hiyo impunity naweza kusema ni tacky, na labda wanazidisha tulivyozoea, lakini bottom line ni kwamba wanatekeleza utamaduni wa CCM tu.
   
 11. U

  Uriria JF-Expert Member

  #11
  Aug 28, 2012
  Joined: Jul 28, 2012
  Messages: 744
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 45
  milioni 300!!! Kwa uwenyekiti Mara?inawzekana, we unajua sana ,utakua MRS LOWASA.
   
 12. U

  Uriria JF-Expert Member

  #12
  Aug 29, 2012
  Joined: Jul 28, 2012
  Messages: 744
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 45
  kagasheki sio tu msomi ni mwanabalozi aliebobea na kakaa njema ya nchini sana kutumikia wabongo, awezi kuongea upuuzi kama huo, wewe kamasio cdm basi mchagga.
   
 13. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #13
  Aug 29, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mkuu sasa hii ndio nini tena! Mimi sioni tatizo lolote hapo, kama wanafuata taratibu zote za kugombea nafasi za uongozi kichama wanakosea nini? yaani jina la KAGASHEKI ndilo liwafunge pingu wasiwanie nafasi yoyote kwa kuogopa KUSEMWA.

  Mleta post hii sijuhi ana lengo gani hasa - hivi BUBA anaweza kweli kusimama jukwaani na kusema familia (koo) ya Kagasheki itakuwa inahakikisha kwamba member wa ukoo wao akiwania nafasi lazima ashinde come rain or SHINE! Buba hana hulka ya kusema such unhelpful REMARKS, tujaribu kuwa wakweli.
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Aug 29, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Waliozila hizo hela walisema. Lakini at the end of the day wakampigia kura Makongoro. Money can't buy love.
   
 15. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #15
  Aug 29, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ndiyo kujipanga huko.
   
 16. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #16
  Aug 29, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Watanzania tuwe makini kuwachunguza watawala wetu kabla ya kuanza kuwapamba na kuwasifia sifa wasiokuwa nazo. Shule ya Kagasheki ni ya kawaida sana,aliweza panda na kupewa hadhi ya ubalozi kwasababu ya mahusiano ya kifamilia na Rais Mwinyi. Aliondoka Uswizi na kuja kugombea ubunge wa Bukoba,baada ya scandal kubwa ya wizi wa pesa ktk shirika la WIPO alikokua mmoja wa wakurugenzi waliotuhumiwa kuiba pesa. Nawashangaa sana wale wanaotarajia huyu jamaa apambane na rushwa za Maliasili na Utalii. Anazo pesa nyingi,wapinzani wake wasiojiweka sawa atawajaza ndugu zake!
   
 17. A

  Africa_Spring JF-Expert Member

  #17
  Aug 29, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yote mmeongea na kuchangia inaonyesha mnajali maslahi ya nchi hii,sasa msifanye tena makosa dawa ya kuwadhibiti hawa akina manyuzi sijui kakasheki ni kubadili mfumo mzima wa kijima kwa kuweka utawala mpya.

  Maana akija mtu mpya hawa kidogo kidogo watakosa nguvu na mwishoe watakua kama ilivyo kua kwa waizrael katika utawala wa MANAZI.

  CHADEMA FOR 2015-TII KIU YAKO
  ,.
   
 18. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #18
  Aug 29, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Tusiwalaumu waliogombea, tuwalaumu waliowachagua (kama kuwachagua wa familia moja ni kosa). Hata hivyo, maji hufuata mkondo; hatuwezi kupingana na asili.
   
 19. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #19
  Aug 29, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Mkuu Jasusi,kwenye ka red hapo,sio kwamba 'pesa ni sabuni ya roho'?
  Wahaya wanasema 'ekyalema amahela naga ( meaning 'kisichonunulika tupilia mbali hakifai').
   
 20. H

  HAPPY MAKUKU Senior Member

  #20
  Aug 29, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 116
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ....[/QUOTE]
  Tatizo ni kwamba wewe ni mpika majungu, kama wewe unataka kunusuru hii hali kuna mtu anakuzuia,? kwani hukijui kile chama ambacho baba, wakwe na wakeze wote wamo kwenye keki ya chama.

  Nakushauri acha kulalama na wewe changamkia fursa kama umeliona hilo, na usilaumu familia za watu, kwani jukumu la familia ni kuhakikisha mtu yeyote katka familia anapata elimu bora na kazi nzuri.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...