Balozi EU: Tanzania itumie rasilimali zake kujikwamua; swali ni je, kwa utawala upi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balozi EU: Tanzania itumie rasilimali zake kujikwamua; swali ni je, kwa utawala upi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magezi, Jun 2, 2010.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU) nchini, Tim Clarke, ameshangazwa na Tanzania kuendelea kuwa maskini licha ya rasilimali zilizopo, kuliko nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na ametaka zitumke vizuri ili kubadili hali ya umasikini iliyopo.

  Clarke alisema aliyasema hayo jana alipomtembelea Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

  Alisema anaijua Tanzania kwa miaka mingi na kutembelea mikoa mbalinmbali, lakini anaona maendeleo ya nchi bado ni kidogo.

  Alisema alianza kuijua Tanzania ikiwa na nusu ya idadi ya watu waliopo sasa, lakini katika kipindi hicho bado huduma muhimu za jamii hazikidhi haja zikiwemo za afya, elimu na kuondoa umaskini miongozi mwa Watanzania.

  Balozi huyo alisema katika kipindi chote alichokuwa hapa nchini, alikitumia katika kusaidia wanawake, watoto na watu wenye ulemavu ili kujikwamua kutoka katika umaskini.

  “EU siku zote itahakikisha maisha ya Watanzania yanakuwa mazuri kwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kupitia misaada. Hata hivyo alibainisha kuwa misaada pekee bila sera na mipango mizuri ya serikali, maisha ya Watanzania hayatabadilika.

  “Sijui tatizo ni nini, sera nzuri utekelezaji mbovu au utekelezaji mzuri, sera mbovu,” alisema Balozi huyo.

  Alisifu Tanzania kwa kuwa na amani na siasa nzuri, lakini akasema vitu hivyo havijaweza kuchangia kuwepo maendeleo kwa Watanzania.

  Aidha, Clarke alisema zinahitajika jitihada ili kuhakikisha Tanzania inashindana katika soko la nchi za Afrika.

  Kwa upande wa biashara alisema Tanzania ina nafasi kubwa ya kufanya biashara kuliko nchi za ukanda wa Afrika Mashariki, kutokana nafasi yake ya uenyekiti wa EAC.

  Alisema ili Tanzania iweze kufikia hayo, inahitaji utashi wa kisiasa na mipango mizuri ya kujiletea maendeleo.

  Alisema kijiografia Tanzania imekaa eneo zuri ambalo linaipa fursa ya kufanya biashara na nchi nyingine za Jumuiya ambazo hazina bandari, hivyo alitaka kuboreshwa kwa ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam, kuimarishwa kwa miundombinu kama reli na barabara ili ifaidi nafasi yake.


  Alipotakiwa kutoa maoni yake kwa Tanzania katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, alisifu mchakato unavyokwenda kwa Tanzania Bara na Visiwani.

  Balozi huyo alisema anaota siku moja Tanzania iwe kinara wa maendeleo katika ukanda wa Afrika Mashariki.

  Aidha, Clarke anatarajia kwamba akipata nafasi ya kurudi hapa nchini miaka 20 ijayo, angependa kuona watoto na wanawake vijijini wamebadilika, na kuwa na maisha mazuri.
  Alisema maisha hayo ni pamoja na kuondokana na matumizi ya jembe la mkono.

  Naye Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi alisema Tanzania bado inakabiliwa na maadui wakubwa watatu ambao ni ujinga, umasikini na maradhi.

  Alikiri kuwa Watanzania wengi wanakabiliwa na umaskini, lakini wanaweza kuondokana na hali hiyo ikiwa watajiamini na kuthubutu.

  Alisema ingawa serikali inasema uchumi umekua lakini bado mwananchi wa kawaida hajanufaika na ukuaji huo hivyo kutaka kuwepo kwa mabadiliko ambayo yatamfikia ili naye ainuke kiuchumi.

  Mengi alisema Watanzania wana macho lakini wanashindwa kuona nafasi mbalimbali za kuwasaidia ili kujiletea maendeleo, na kwamba wengi wao wanaogopa hata kujaribu jambo ambalo linawafanya washindwe kabla ya kuanza.

  “Watanzania wengi hawajiamini na wana macho lakini hawayatumii kuona nafasi mbalimbali za kujipatia maendeleo zinazowwazunguka,” alisema.

  Alimuomba Clarke kupitia Jumuiya ya Ulaya kuangalia uwezekano wa kuwasaidia wafanyabaishara, wazalishaji na sekta binafsi kwa ujumla waweze kupiga hatua.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Huwa najiuliza sana kila napokutana na hoja za watu wa nje ya Tanzania na hasa wahisani pale wanaposhangaa ni kwa nini Tanzania pamoja na utajiri ilionao lakini ni miongoni mwa nchi maskini zaidi duniani.

  Lakini kwa mawazo yangu moja ya sababu ya kushindwa kutumia vyema rasilimali zetu kwa manufaa ya wananchi na nchi kwa ujumla ni utawla mbovu wa CCM. Nayasema haya kwa sababu hakuna nchi yoyote duniani iliyopata maendeleo ya kiuchumi na kijamii bila kuwashirikisha na kuwa thamini wataalamu wake wa ndani.

  Moja ya sera za CCM ni kutowashirikisha wataalamu wake wa ndani ktk masuala muhimu ya uchumi wa nchi, mfano ni karibu mikataba mingi ya ubinafsishaji wa mashirika ya umma iliandalia nje ya nchi ikisha sainiwa na wajinga wa CCM wanasema ni siri.

  Angalia suala la uteuzi wa viongozi wa wizara na mashirika mbali mabli. linafanyw kisiasa badala ya kitaaluma. Inatakiwa kama CCM wanakumbatia siasa basi mawaziri wasiwe na final say ktk wizara bali makatibu wakuu ndo wanatakiwa wawe na kauli ya mwisho lakini livyo sasa eti makatibu wakuu ni washauri wa waziri, wakati huo huo waziri ndo mwenye signature ya mwisho....huo ni uhuni ktk utawla.

  Leo tunaimba ngonjera za kilimo kwanza lakini anayenunua matrekta ni mkurugenzi wa halmashauri ambaye hajui hata ni trekta gani lenye ubora wa kuhimili mazingira magumu ya Tanzania. Wahandisi wapo pale SUA (agricultural engineers) lakini huwezi sikia wamepewa jukumu hilo. Mfano ni trekta za power tillers, hizi hazifai maeneo ya milimani kitaalamu lakini nenda kaone wilaya nyingi zimeyanunua haya na wakulima wanaanza kushindwa kuzitumia kwani mtu akiitumia siku mbili lazima ataugua mgongo, kifua n.k.

  Bila CCM Tanzania bado inaweza kuwa na mwonekano mpya, tafakari na chukua hatua ktk uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
   
 3. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Nimeipenda sana hotuba ya huyu bwana. Anatukosoa na kutupa matumaini. Amekuwa muwazi sana. Wenye masikio na tusikie.
   
Loading...