Balozi Donald Wright: Vijana wa Tanzania wanapenda kuwa huru kujieleza

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,009
9,874
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald J, Wright amesema katika vijana aliokutana nao wameonesha kutaka kushiriki katika maisha ya kisiasa na kijamii, pia wanataka uhuru wa kujieleza sauti zao zisikike.

Ameyasema hayo Desemba 12, 2022 alipoungana na viongozi vijana zaidi ya 400 kutoka nchi 47 za Afrika katika uzinduzi wa #YouLead22.

Balozi amesema Marekani imedhamiria kwa dhati kuwasaidia vijana wa Kiafrika wanapofanya kazi ya kujenga mustakabali wanaoutaka. Ni muhimu kuhakikisha vijana wanakuwa na nafasi katika meza ya majadiliano kwa lengo la kuwezesha sauti zao kusikika na kuwa sehemu ya uamuzi wa masuala yanayowagusa.

Vijana waliokutana na balozi Donald ni wa mikoa mbalimbali ya Tanzania ikiwemo ya kusini mwa Tanzania na Kanda ya ziwa. Vijana wanataka kuwa huru kujieleza.
 
Aache kuwasemea watu. Mwisho wa siku ataanza kushinikiza uhuru wa kila kitu kwa hao vijana.

Wamarekani siyo watu wa kuwasikiliza hata kidogo.


Ndiyo hawa hawa wanaounga mkono ushoga na usagaji waziwazi, halafu wakati huo huo wanapinga ndoa za mitala!!!
 
Back
Top Bottom