Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,797
- 11,959
"MTOTO ALIYEANDIKA BARUA YA KUACHA SHULE ANA AKILI SANA" RC TABORA
"Niliongea na mkuu wa mkoa wa Mtwara baada ya kuona barua ya mtoto aliyetaka kuacha shule, nikamwambia huyu mtoto ana akili sana kwasababu haiwezekani mwanafunzi mtoro aandike barua kama hiyo, nikamwambia mkuu wa mkoa wa Mtwara mtafute huyu mtoto na kweli amemtafuta na kutatua changamoto zake na sasa amerudi shule mwenyewe, kwahiyo walimu wasaidieni watoto kuwajenga kisaikolojia"-Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Batilda Buriani katika kongamano la walimu na uchumi.
Taufiki Salumu mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Msimbati Mkoani Mtwara ambaye aliandika barua ya kuacha shule kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo amesema lengo kubwa la kutaka kuacha shule ni hali ngumu ya maisha ambayo imemlazimu yeye kuchukua maamuzi hayo.
Chanzo cha habari ni CGFM Tabora
Pia, soma:
1). Mtwara: Mwanafunzi wa kidato cha 1 aandika barua kwa Mwalimu Mkuu akisema Shule imemshinda