Balozi apongeza Vyombo vya habari Tanzania kwa kupambana na ufisadi

Mama

JF-Expert Member
Mar 24, 2008
2,848
58
Balozi apongeza Vyombo vya habari Tanzania kwa kupambana na ufisadi
Na Furaha Kijingo

BALOZI wa Sweden nchini Tanzania, Staffan Herrstrom amevipongeza vyombo vya habari kwa kupinga na kupambana na vitendo viovu ikiwa ni pamoja na rushwa.

Hayo aliyasema jana wakati akifungua mkutano wa kitaifa wa uangalizi wa maendeleo ya jamii nchini ulioandaliwa na wanachama wa kutetea haki za Binadamu kusini Mwa Afrika (SAHRiNGON) wenye lengo la kujaidili Haki na amani ya Mtanzania na maendeleo endelevu.

Herrstrom alisema vyombo vya habari ni msingi mkuu wa demokrasia na kwamba anamatumaini kuwa kasi hii ya vyombo vya habari vya nchini, inaweza kuifanya Tanzania iendelea katika nyanja mbalimbali ikiwamo ya uchumi.

Aliongeza kuwa habari ni kama hewa ya oxyjeni ilivyo muhimu kwa bianadamu, hivyo na Tanzania ili iendelee kiuchumi na kijamii, inatakiwa vyombo vya habari vifanye kazi kwa uhuru.

"Habari ni muhimu kwa binadamu kama ilivyo muhimu hewa ya oksijeni kwake" alisema Herrstom.

Kwa upande wake mkurungenzi wa Haki za Binadamu Hereni Kijo bisimba alisema ulinzi wa wawananchi wa kijadi umepotea hivyo wanahitaji serikali iaandae ulinzi kwa mtu hata kama akizeeka, akiugua, akikosa kazi serikali iweze kumsaidia.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa SAHARINGON, Rehema Kerefu alisema kulingana na kauli mbiu ya mkutano huu, inayosema "Utu,Haki na Maendeleo kwa wote" wanaitaka serikali hivyo vijisent vibadiliki na yawe mabilioni yatakayo waletea maendleo watanzania.

Mkutano huu ulitanguliwa na maandama ya amani yaliyo anzia katika viwanja vya mnzi mmojakuelekea kwenye ukumbi wa karimjee ambako wana harakati walijadili maada mbalimbali kuhusu maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni kuzingatia taarifa za utafiti zilizofanywa na matandao mwaka jana.
 
Back
Top Bottom