aleesha
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 792
- 1,144
Katika majadiliano ya jana kati ya Balozi Amina Salum Ali na mwandishi wa Nipashe unaweza kuuona muhma alionao baada ya kuhusika moja kwa moja katika uchafuzi wa suluhu iliowekwa na waliomtangulia tokea mwaka 2009. Alipoondoka kuenda kushika nafasi ya kidiplomasia nchini Marekani aliiwacha nchi ikiwa taabani kiuchumi na kijamii, na siku alipotua mguu wake nchini kwa dhamira ya urais wa Tanzania na kuukosa, alilolifanya ni kuirejesha nchi kule kule alipoiacha katika miaka ya tisini na kutumika si kuhujumu tu maelewano makubwa ya wananchi bali hata mfumo mzima wa kidemokrasia uliowekwa ambao haukutoa mshindi hasa baina ya CCM na CUF bali maslahi mapana ya wananchi na nchi kwa jumla.
Unaweza kujiuliza kulikoni hasa leo hii awe na kauli laini kufika hadi kuukubali ukweli wa walio wengi ndio waliogoma kushiriki katika uchafuzi wao wa March 2016? Anakiri kabisa kuwa kuna hasama kubwa baina ya wananchi, na hali iliopo katika ardhi hii hasa baada ya kurudi kwake ni bughdha, hasama, na uonevu tu kwa wananchi. Lakini labda leo tumtazame hasa kwa yakini kabisa ni nani Bi Amina na kuhusika kwake moja kwa moja kudidimia kwa maendeleo tokea aliposhika nafasi kuu Hazina miaka ya tisini halafu tujiulize hivi huyu mama anaweza kusimama akinadia haki, uadilifu na kuwa mwenye huzuni na haya yaliopo?
Katika historia ya uongozi wake akiwa Mkuu wa Hazina ndie waziri wa kwanza alieondoka akiiwacha nchi ikiwa imefilisika kabisa. Ndie waziri wa kwanza wa fedha katika historia ya nchi hii akiondoka huku akiiwacha serikali ikiwa haina hata mapato ya kulipa mishahara ya wafanyakazi wake kwa miezi sita. Anaondoka madarakani wizara ikiwa imejaa madeni, imejaa rushwa, inanuka ufisadi na ikiwa na madeni yasio mithilika. Yeye ni mmoja wa sehemu hasa ya miakataba mibovu ilioingamiza Zanzibar ikajiinamia na kupoteza sifa zote za kuwa kituo cha kibiashara katika Afrika Mashariki. Kaondoka akihakikisha Serikali ya Zanzibar ni fukara, leo ndie anaeitwa Waziri wa Biashara, utegemee mabadiliko kweli?
Moja ya madeni ambayo hadi hii leo tunadaiwa ni deni lililoasisiwa nae moja kwa moja pale alipojisukuma katika mkataba na Nimrod Mkono kuidai Serikali ya Jamhuri ya Muungano fedha ambazo SMZ ikiidai kwa makubaliano ya kamisheni ya asilimia 15 kulipwa Mkono kama fidia ya madai hayo. Hakukuwa na mkataba bali ni ile "retainer note" alioisaini mwenyewe inayotufunga sisi kimagirini kumlipa Mkono mamilioni ya pesa bila ya hata ushirikishwaji wa wanasheria wa serikali wakati ule. Deni hili hadi hii leo linadaiwa na Mkono na kalipandisha mpaka hadi sasa ni takriban Bilioni saba. Wakati ukishangaa ya mikataba ya mchanga wa dhahabu huku kwetu tulikuwa na karatasi moja tu ya Waziri alietuwekea deni lililofika sasa takriban bilioni 7.
Serikali ya Jamhuri iliridhia kulipa sehemu ya deni baada ya Mkono kuzungumza nao akijuwa kabisa malipo yake si chini ya milioni sabini katika milioni 400 zilizotolewa na SMT. Haya ndio matunda ya Balozi Amina, mgombea wa urais na alietawadhwa kuwa Waziri mpya wa Biashara baada ya genge lao kutumika kuvunja maelewano yaliokuwapo awali, kuvunja katiba ya wananchi na mabadiliko yake ya mwaka 2010 na zaidi kuiangusha ile dhamana ya makubaliano yalioasisi Serikali ya Umoja iliokuwa na afuweni kwa jamii nzima ya wananchi hapa visiwani. Umasikini wetu huu umechangiwa pakubwa na mfano wa viongozi wa namna hii. Unafikiri kama si masilahi binafsi wangekuwa na ushawishi wa kuufuta uchaguzi huru? Unawahesabu washiriki wakuu na kuhesabu pia madhambi yao na maslahi yao.
Mwaka 2000 wakati wa uongozi wa Dr Karume, Nimrod Mkono akaja tena na madai kutokana na ile ile "retainer note" ya Waziri, mara hii akidai sasa bilioni mbili kama sehemu ya kamisheni yake anayoidai serikali ya Zanzibar. Hakufanikiwa maana alipuuzwa lakini hakuishia hapo bali akarudi tena baada ya kutangazwa Dr Shein kuwa Rais mwaka 2010 na mara hii deni lake likapanda kufikia takriban bilioni 7. Wakati Bara wakilalamika na wanaoitwa wanyonyaji wa nje, Zanzibar inaliwa na wanyonyaji wa ndani na hawa kina Mkono na bughdha ya deni la kidhalimu.
Hili lilipingwa na waliobeba dhamana ya kusimamia sheria za nchi na serikali na halikufanikiwa katika kipindi kwa muda wa 2010 mpaka 2015 kwa sababu kulikuwa na waliobeba dhamana hasa ya kuhakikisha hatuwi tena kichwa cha mwenda wazimu kinachonyolewa na kila mtu. Wakati akijipanga kwa urais wa 2015 hakuna aliemkumbusha namna gani hazina alivyoiacha Zanzibar na kuifisidi na kudaiwa kila pembe ya nchi. Hakuna aliemkumbusha "Retainer Note" yake ilioibebesha Serikali na umma huu mabilioni ya pesa kwa deni hewa ambalo ni yeye alieingia mkataba nalo na kutuachia hadi hii leo likitusumbua. Hakuna anaemkumbusha hivi sasa matokeo ya kukurupuka katika uongozi wake uliotutia hasara kirahisi rahisi.
Ukitaka kuzijua nia za hawa watu basi usishangae kwa sasa anaeshikilia deni hili lilipwe ni huyu huyu "Bwana Sifanyi Chochote", nae pia balozi kama alivyo Waziri wake. Inakufanya wakti mwengine ufikiri hivi mpaka lini viongozi wa Zanzibar watahadaiwa na "viji-appartment" vya Kigamboni huku wakidhamiria Kabisa kuitia umaskini nchi? Unafika mtu nafasi ya kuwa msimamizi mkuu wa Serikali, lakini huridhiki wala huna huruma ya wanyonge na watoto wanaolalia uji na kuamkia uji patupu. Halikuumi basi tumbo unapowakuta watoto wa kimasikini wakijaa vumbi kwa kukosa hata madawati ya shule wakati kuna Bilioni saba zinazotaka kuangamizwa kienyeji enyeji?
Fikiri hizi Bilioni saba zingewasaidia wananchi kwa namna ipi hasa ukisikia Hospitali hazina dawa? Haya mafuriko na kiburi cha kuwaambia wananchi wanajenga bila ya mpangilio jee zisingeweza kusaidia kuirejesha miundo mbinu na kutusogezea maendeleo? Hivi kweli zisingeweza kutusaidia sisi tunaozaliana bila mpangilio katika maendeleo kama ambavyo Dr Shein alivyolalamika? Fikiri wale waja wazito wanaohangaika na vichanga hospitalini kwa afya ya kubahatisha kabisa jee zingewasogeza wapi fedha hizi? Basi hata Mungu hamumuoni na huu ulaji uliokithiri na kuvuka mipaka basi hata ya utu? Tuna deni la umeme jee halilipiki?
Usiende mbali zaidi katika majutar wa nchi hii ambao ni hatari kwa maslahi ya uchumi wetu ni huyu huyu Hamad Rashid ambae sasa ndio kawa mshenga hasa wa Mkono kuhakikisha hizi Bilioni saba za wanyonge na walipa kodi wanaoteseka zinabebwa na kugaiwa kiholela. Unajuwa kama yeye ndie anaetembea na mamilioni ya hongo mkobani kuwashawish wanasheria wetu kuridhia malipo haya kama ndio bahshish ya wino wa kuanza kazi. Watazame hawa wote ndio "cream" ya uongozi wa Bwana Mkubwa, asieondoshwa na yoyote mwenye ubavu. Huyu anaejitambulisha kuwa Waziri wa Kilimo anaewasumbua vijana wabeba mchanga wa Donge ndie aliekuwa akitembea na begi la milioni 20 kule St Gasper Dodoma tayari wakati huo kashaziweka ndani thalathini kuwa za kwake akijaribu kumlaghai mwengine aridhie na kututia hasara isiomithilika. Hata hio hongo aliokabidhiwa tayari kashajigawia thalathini za kwake, ishirini ziko mkobani kutafuta msitiri wa dhulma kwa umma huu unaoishi kwa chini ya dola moja kwa siku. Unafikiri hawamjui na hawayajui haya anayoyafanya?
Sasa vuta picha ya kule Uwanja wa Ndege na haya yanayofanyika, tazama ile meli ilionunuliwa ikidaiwa kuwa ni mpya, tazama pia namna gani kila penye nia ya maendeleo hakuna linaloendea yote kwa sababu ya mazowea ya nchi chini ya watawala hawa ya kujinufaisha binafsi. Wakati tukipiga kelele kwa hili sakata la mchanga wa dhahabu na hii mikataba yetu basi na huku Zanzibar chini ya mawaziri hawa ndio sababu ya kukwama kwa kila nyenzo ya maendeleo. Ikiwa Msimamizi Mkuu wa Serikali ambae anaewajibika na kuiwakilisha serikali hadi kwenye chombo cha kutunga sheria ndie anaeshadidia kuitia nchi katika hasara ya namna hii hivi hao anaowasimamia watakuwaje?
Tumalize kwa kujiuliza hivi kweli huyu mama anaweza kunyanyuka na kutuusia wananchi maadili, uadilifu na umoja wakati yeye binafsi ni sehemu kubwa ya mtafaruk uliopo kwa sababu tu ya mazowea ya ubinafsi na maslahi yake mwenyewe? Hivi huyu mama atasimama lini na kutuomba radhi wananchi kwa naqama aliotuwachia wakati akiwa Waziri wa Fedha na hizi "Retainer Notes" zilizotufikisha hapa kiasi ya kudaiwa bilioni saba kirahisi rahisi? Hivi tuseme hawa wangelikuwa upande wa pili wangelisalimika na utumbuaji unaoendelea? Hivi haoni haya kabisa kwa hii "legacy" yake visiwani?
Anataka awaaminishe wana CCM kuwa tatizo lao kukosa kura Zanzibar ati ni kwa sababu ya wapemba kuletwa Unguja kupiga kura. Ikiwa ni wapemba wanapungua kwa idadi hio kisiwani Pemba sasa kwa nini basi na hio idadi ndogo waliobaki bado CCM haitakiwi? Au kwa nini kuna ongezeko la kura za upinzani katika kila mkoa wa kisiwa cha Unguja, hivi anataka kuwaambia wananchi kuwa ni wapemba walioko Kaskazini mpaka Makunduchi?
Ukweli ni kuwa anguko la CCM ni kwa sababu ya mazowea ya uongozi wa aina yake. Yaani karatasi ya ukurasa mmoja tu inayoidhinishwa na yeye binafsi imetufikishia deni la bilioni sabiini halafu kweli atuonyeshe mchawi ni nani? Haya ndio yaliopelekea kulazimishwa kuchukuwa mapumziko wakati ule akiwa Hazina. Leo anahubiri uadilifu, maadili na wema angelianza kwa vitendo kwanza kwa kukata mshahara wake kulipa fidia ya hasara aliotuingiza.