Uingereza yaadhimisha kumbukumbu ya mashujaa
Mwandishi Wetu
HabariLeo; Monday,November 12, 2007 @00:06
SERIKALI ya Uingereza jana iliadhimisha kumbukumbu ya mashujaa wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola waliofariki dunia nchini wakati wa Vita ya Kwanza ya Dunia. Kumbukumbu hiyo ilifanyika katika makaburi ya mashujaa hao yaliyopo Makumbusho, Dar es Salaam.
Wengi wa mashujaa hao ni wanajeshi, wanamaji, wanaanga na raia wa kawaida walishiriki katika vita hivyo vilivyotokea kati ya mwaka 1914 hadi 1918 na pia Vita ya Pili ya mwaka 1939 hadi 1945.
Maadhimisho rasmi yalianza kwa gwaride la heshima lililofanywa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), mbele ya Balozi wa Uingereza nchini, Philip Parham likifuatiwa na sala kutoka katika dini za Waislamu, Wakristo na Wahindu.
Akizungumza katika hotuba yake baada ya sala, Balozi Parham alisema nia ya kumbukumbu hiyo ni kuonyesha kuthamini kazi iliyofanywa na mashujaa hao ambao wengi wao ni kutoka katika mataifa ya Uingereza na Ujerumani.
Wakati wa vita hivyo Uingereza na Ujerumani zilikuwa zikipigana kwa kushirikisha mataifa marafiki na makoloni yao.
"Hii ni kumbukumbu ya muhimu kwetu na kwa jamii ya Watanzania kwani vita ile ilitugusa sote na kufanya hivi ni kukubali umuhimu wa mashujaa wetu na pia kutambua kuwa wapo waathirika bado wa vita hiyo na hasa ya pili katika nchi hii ambao wanahitaji kuendelea kusaidiwa," alisema.
Wapiganaji wa nchini katika hafla hiyo waliwakilishwa na Ally Sykes ambaye pia aliendesha sala ya jumla na kuomba uhusiano mwema baina ya mataifa utakaojenga imani na kuisababisha dunia kuwa na amani ya kudumu.
Mataifa yaliyowakilishwa katika kumbukumbu hiyo ni Nigeria, Kenya, Uganda, Ujerumani, Uingereza, Malawi, India, Afrika Kusini, Zimbabwe, Italia, Zambia, Canada, Msumbiji, Russia, Ufaransa, Ubelgiji na washirika wengine wakiwamo Marekani.