Ballon d'Or 2019: Lionel Messi ashinda tuzo ya sita ya Ballon d'Or awabwaga Virgil Van Dijk na Cristiano Ronaldo

mzabhe

JF-Expert Member
Jul 16, 2017
261
279
Tuzo ya Ballon d'Or ya 2019 inatarajiwa kutolewa leo Desemba 2, 2019, huko Theatre du Chatelet, Paris. Sherehe rasmi itaanza saa 19:30 GMT (1:00am, Desemba 3, IST).

Luka Modric alishinda tuzo ya Ballon d'Or mnamo 2018 na kuvunja utawala wa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wa tuzo hiyo kwa miaka 10 iliyopita

Ronaldo na Messi wote wameshinda tuzo hiyo mara tano, lakini utawala wao unaweza kuvunjwa tena mwaka huu na nyota wa Liverpool na Uholanzi, Virgil van Dijk. Beki huyo alipewa tuzo ya Mchezaji wa Mwaka wa UEFA, huku akiwashinda wawili hao

1.jpg

Messi kwa sasa anapewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo yake ya sita ya Ballon d'Or, licha ya kupoteza kwenye Ligi ya Mabingwa na Copa del Rey na kuinua kombe la Liga na Barcelona.

Alishinda Kiatu cha Dhahabu cha Europa akiwa na mabao 36, ingawa kushindwa kushinda Copa Amerika na Argentina msimu huu wa joto kunaweza kuathiri nafasi zake

Mwezi Septemba alipewa tuzo ya Mchezaji bora wa Wanaume wa FIFA na hiyo inaweza kumsaidia kushinda tuzo hiyo dhidi ya Van Dijk

2.png

Hata hiyo kumesambaa icha katika mitandao ya kijamii ikionesha kuwa Mshindi wa msimu huu wa tuzo hiyo ni Lionel Mesii akiwa amemshinda Van Vijk huku Cristiano Ronaldo akiwa katika nafasi ya nne
*****

My take:
King leo lazima achukue ballon d or yake ya sita, anayebisha afanye kama anajikuna
**

UPDATES
Orodha ya Wachezaji bora walioshika nafasi ya 11 hadi ya 30 kama ilivyotolewa na Waandaaji wa tuzo ya Ballon d'Or
1.PNG

Orodha ya Wachezaji 10 katika Utoaji wa tuzo ya Ballon d'Or iliyotolewa na kushuhudiwa Messi akinyakuwa tuzo hiyo kwa mara ya sita
1.jpg

Mshambuliaji wa Klabu ya Barcelona na Timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi ametangazwa kuwa Mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia (Ballon D'or) kwa mwaka 2019

2.jpg


 
Nasikia kura zimeshavuja, The GOAT! Messi kachukua afu Mzee wa kuvizia kashika nafasi ya NNE nyuma ya Salah. Nasikia na wandaaji wa tuzo wiki iliyopita walikua Barcelona kuchukua video za Messi na kufanya mahojiano nae.
Note, sio official lakini ni rumors
 
Nasikia kura zimeshavuja, The GOAT! Messi kachukua afu Mzee wa kuvizia kashika nafasi ya NNE nyuma ya Salah. Nasikia na wandaaji wa tuzo wiki iliyopita walikua Barcelona kuchukua video za Messi na kufanya mahojiano nae.
Note, sio official lakini ni rumors
Na iwe hivo kama ulivosema mkuu
 
Leo jumatatu 02/12/2019 kunafanyika sherehe za 64 za ugawaji wa tuzo za Mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2019.

Tuzo hizo zinazotolewa na jarida la France Football, zitafanyika leo jijini Paris. Wachezaji wanapigiwa chapuo kutwaa tuzo hiyo ni Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, Virgil Van Dijk.

Sherehe hizo zitaanza Saa 2:30 usiku kwa masaa ya Afrika Mashariki kupitia Dstv.

Tutakuletea yanayojiri hapa.
IMG_20191202_111930.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom