Ballali Anyang'anywa Viza ya Marekani & Wengine Wasema Tayari Keshakimbilia Malta !

Hii case inazidi kuwa kubwa na kama jamaa wanaitumia state dept ya US kumsakama Balali basi wajue kuwa wanaikuza hii case bila sababu yoyote. Kuna watu wengi sana wamehusika na wizi huu BOT. Kashfa hii inakwenda mpaka mlangoni mwa usalama wa taifa (TISS). Balali inabidi ajue kuwa anacheza na watu hatari sana na inabidi awe kwenye record bora haraka sana iwezekanavyo.


Bibie Mwafrika nakubaliana nawe fika;

Inawezekani pia wanatoa oyo kwa wengine ambao wamekimbilia marekani kujificha. Mimi ningependa wigo huu utanuke na hawa wamerekani wachukue interest ya ku-investigate hii scandali kwa vile hata kina Mgonja na majumba yao San Fransisco anakoishi ($800,000) mkewe pia wamulikwe.

Kama huyu balozi wa marekani atatishia ku block the $680 million za MCC kama alivyosema, huenda JK akafurukuta na kubwaga manyanga na kuwatosa wenziwe, which as I know him he can being an opportunist na mpenda sifa!

Balali was warned by TISS and PCB several times, hata baada ya ile document ya Jitu ku be circulated alifuatwa na TISS akaambiwa vipi bwana, lakini hakusikia kwa vile Mkapa was on his side, wakati Mkapa mwenyewe keshaondoka. Nakumbuka walipokutana BWM na akapewa kazi hiyo Hilton Washington DC 1997 baada ya kuwa introduced na Anna Muganda through Anna Mkapa! Ama kweli dunia tambara bovu .. can you believe akamwacha mkewe akamchkua Anna Muganda and they had their wedding vows kwenye Canals kule Venice Italy! Sasa kazi hana akiwa DC tena ten years later!

Sikio la kufa halisikii!
 
Nadhani sasa mchezo unakuwa mtamu.Balali aseme kwa nini DeepGreen haikom katika list ama walichagua mengine na kuacha mengine ? Kuna connection kubwa ya TISS na Deep Green

Mzee Lunyungu.. kuna mtu aliniambia kwamba habari za Deep Green na TISS ni classified, so sahau kabisa kusikia habari zake kwenye ripoti ya wakaguzi.. na ndicho kilichotokea.
Kuna ishu nzito imekaliwa zaidi ya inavyoelezwa.. na nina wasiwasi kama Balali anaweza kusema lolote zaidi ya Blah bllah ya kujitetea.
So far huyu jamaa akiamua anaweza kukaa US for the rest of his life.. unless Serikali iamue kumfikisha Mahakamani.. na hata akifika huko possibility ya kuwa kama Prof mahalu na Ditopile iko pale pale!
Bongo yetu ni noma!
 
Ni kweli mtanzania,uwezi kuwa na viza mbili kwa wakati mmoja ni lazima ifutwe moja na kuapply nyingine.ukisha ingia kwenye hizi nchi si rahisi kumuondoa mtu kutokana na sheria zao,zina thamini utu wa mtu.
 
Good News.....mtoto Wa Mkulima Swala La Mali Zake Kuwa Freezed Hilo Tayari Kaka Na Lina Mwezi Sasa,,na Kwa Taarifa Tu Maliza Yule Fisadi Mwingine Na Mala.....a Aliekuwa Anaonga Madadazetu Kwa Kuwapa Magari Mzee Lyumba Nazo Ziko Mikononi Mwa Polisi Pamoja Na Acc Yake Uko Swiss,,mwingine Ni Mzee Tunonge Hawa Ndio Waliokuwa Connction Halisi Ya Huyu Mzee Ni Wachafu Toka Rohoni Mpaka Mwilini,,,mali Zao Ziko Mikononi Mwa Serikali,,,lingine Ni Kwa Taarifa Tu Ukweli Halisi Wa Haya Makampuni Ya Wizi Ulipatikana Juzijuzi Walipokuwa Wanahaia Kwenye Ofisi Mpya Wakiwa Huko Kile Kitabu Kikadondoka Wakiwa Na Ma Nyoka Wakashindana Ndipo Mwisho Wakaangalia Na Kukuta Hamad Aibu Tupu,,,katika Hayo Makampuni Ya Slaa Yapo Mengi Tuu,,,hawakutaka Kutaja Wana Jf Tusubiri Kama Huyu Bwana Atatoa Hiyo Report,,kama Asipoitoa Kama Ilivyo Shaka Hakuna Hapa Ni Jf....tusubiri Wajichanganye Wenyewe Kwanza....
 
Jamani Kama Wamemdeport Si Mtujulishe Yuko Na Ndege Gni Tuwhi Kumpokea Na Matarumbeta Hapa Jnia
 
Jamani Kama Wamemdeport Si Mtujulishe Yuko Na Ndege Gni Tuwhi Kumpokea Na Matarumbeta Hapa Jnia

Hawajamdeport bado maana hata wao wanaogopa kuchafuka na hii skendo ya karne! Tanzania hii sio safi kama watu walivyokuwa wanafikiri! kuna amani kwa vile watu wengi wamekubali tu yaishe ila kuna mafia mbaya sana imeshika madaraka ya nchi hiyo
 
Ni bora huyo Balali awataje wote aliokula nao haraka iwezekanavyo au hata akishindwa basi aandike japo email au something ikiwataja wote na pia Waziri Meghji naye ajiuzulu kwa kuwa yalitokea akiwa anaangalia.

-Wembe

Wembe M: Nafikiri atawataja msukumo ni mkubwa.. pata hiii!!! Kutoka Raiamwema: http://www.raiamwema.co.tz/08/01/16/3.php
Ndugu wamshinikiza Ballali kujibu mapigo ya Serikali

Mwandishi Wetu Januari, 16, 2008

Sasa anaweza kuzungumza
ALIYEKUA Gavana wa Benki Kuu (BoT) Dk. Daudi Ballali, ameanza kupata nafuu na anashinikizwa na ndugu ajibu mapigo ya tuhuma za Serikali zilizosababisha ang’olewe wiki iliyopita.

Taarifa za karibu na ndugu zake zilizopatikana wiki hii, zinasema sasa Dk. Ballali anazungumza baada ya kuwa amepoteza fahamu kwa muda mrefu, na matarajio ya wanafamilia yake ni kwamba muda si mrefu akiendelea hivyo, ataijibu Serikali.

Mmoja wa wanafamilia ameiambia Raia Mwema kwamba kuna shinikizo la familia na marafiki, la kumtaka ajisafishe dhidi ya tuhuma za ubadhirifu ndani ya BoT ambazo ndizo msingi wa kuondolewa kwake.

Kwa mujibu wa habari hizo, Ballali amekuwa akipata shinikizo kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki ili aweze kujitokeza na kutoa maelezo ya nini kilichomsibu, hasa baada ya Serikali kushindwa kutoa taarifa halisi ya hali yake ya ugonjwa.

Mbali ya kuzungumzia hali ya afya yake, Ballali anashinikizwa pia azungumzie kuhusu hatima yake hasa baada ya mwenyewe kuomba kujiuzulu na kujikuta akitimuliwa akiwa mgonjwa badala ya kujibiwa barua yake ya kuomba kujiuzulu ambayo haijapata kutangazwa rasmi nchini.

Kwa mujibu wa habari hizo, yeye mwenyewe amekuwa akitoa kipaumbele kwa afya yake kwanza badala ya kuingia katika malumbano na wakuu wake, na kwa kuwa kimsingi hajaondolewa katika utumishi wa umma.

Taarifa za ugonjwa wa Ballali zimekua zikitatanisha, zikizongwa na usiri mkubwa kiasi cha kuibuka uvumi wa kuwa amekwisha kufa. Serikali haijatoa taarifa ya kina kuhusu hali yake.

“Serikali kwa kawaida haiwezi kuzungumzia ugonjwa wa mtu bila ridhaa kwanza ya familia, na familia ndiyo inayoweza kutoa taarifa ama kuiomba Serikali itoe taarifa kwa kushirikiana nayo, na hili la Ballali ni katika mantiki hiyo,” alisema ofisa mmoja mwandamizi wa Serikali.

Ofisa huyo alisema Ballali amekuwa akiumwa kwa muda mrefu sasa japo amekuwa akipata matibabu ndani na nje ya nchi na kwamba kabla ya kwenda Marekani aliwahi kutibiwa nchini Afrika Kusini.


Mawaziri wahojiwa

Mwandishi Wetu Januari, 16, 2008



HALI si shwari ndani na nje ya Serikali kuhusiana na matukio ya Benku Kuu (BoT) na sasa imebainika kwamba baadhi ya wanasiasa, wakiwamo mawaziri, wa sasa na wa zamani, wanatuhumiwa kuhusika na ufisadi ndani ya benki hiyo.

Habari za ndani ya Serikali zinaeleza kwamba tuhuma hizo zimetokana na ukweli kwamba baadhi ya wanasiasa na watendaji waliojificha nyuma ya wafanyabiashara, wamenufaika na fedha zilizopotea ndani ya BoT.....http://www.raiamwema.co.tz/08/01/16/1.php

Malizia story: http://www.raiamwema.co.tz/08/01/16/1.php
 
Kuna baadhi ya nyadhifa za kiserikali zinazompa mtu pasi maalum. Watu kama Director of TISS, IGP, CDF, Govenor etc hawa wote wanapata diplomatic passport (pamoja na mawaziri, etc). Kwa hiyo nafikiri bwana Ballali imebidi arudishe diplomatic passport yake ambayo itamwondolea immunities zote alizokuwa nazo za kukamatwa.

Kitu kinachoweza kuleta utata ni kuwa kuwa na green card hapa Marekani sio kitu cha kutisha sana. Ukionyesha una biashara yenye at least $100,000 na unataka iwe Marekani utaipata tu hiyo green card (wahindi wengi wana vituo vya mafuta kwa ajili hii). Sasa Ballali ana nyumba Bethesda, Maryland, ambako ni makazi ya wenye fedha zao za kutosha, viongozi wakuu wengi, na diplomats. Chances ni kuwa bado ataweza kubakia kivyake vyake na si kama mtumishi wa URT.

Vinginevyo, kama Marekani wamechefushwa vya kutosha na ufisadi wake, hata hiyo greencard (kama anayo) inaweza ikawa revoked. Cha muhimu kwa serikali ya Marekani ni kuzidi kumbana JK ili Ballali na wapambe wake woote (inaelekea ni wengi na wenye nguvu) wafikishwe mbele ya sheria. Na wakifika mbele ya sheria, wapate kile wanachostahili na sio kwa mahakama kuwaogopa.
 
Kuna umhimu wa kuwa na "TimeLine' iayoeleeka tokea huyu bwana alipofika hospitali kutibiwa.

Kama alikuwa kwenye 'coma' kama inavyosemekana, barua ya kujiuzuru aliiandika lini?
 
Jamani JK anaweza kweli kumfiksha mbele ya sheria Balali? Kwani tayari ameshamkingia kifua mkapa Kuhusiana na kufanya biashara IKULU, Na anajuwa wazikua katika hilo la balali na benj yumo?
 
Jamani kuna kitu hapa kinanichanganya. Watu wengi wanasema Balali akirudishwa TZ siri zitafichuka. Ni siri gani hizo ambazo bado hazijafichuka? Au mnataka zifichuke mara ngapi na kwa nani?

Ripoti ya wakaguzi ilifichua siri zote na hakuna aliyeziona zaidi ya hao hao wahusika wakuu. Sasa mnategemea kupata siri gani zaidi kutoka kwa Balali?

Atazifichua nakubali lakini zitafichwa tena. Mchezo utabaki huo huo. Akizifichua mna uhakika zitatufikia? Hapa sioni kitu mimi, bado mazingaombwe tu.

Tunajiridhisha bure jamani.
 
Ufisadi BoT: Baada ya kufukuzwa kazi, Marekani yamfutia viza Dk Ballali
* Ubalozi wasema hastahili kuishi nchini humo
* Wasema hawajui anakotibiwa

* Ndulu asisitiza kuwa bado ni mgonjwa


Dennis Msacky na Ramadhan Semtawa


SERIKALI ya Marekani ikiwa imetangaza kumfutia viza aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daud Ballali, anadaiwa kuwa ametorokea kwenye Visiwa vya Malta.


Kufuatia kufutiwa viza, Ballali sasa haruhusiwi kuishi wala kwenda nchini Marekani.


Katika hatua nyingine kumhusu mtuhumiwa huyo wa ufisadi, Mbunge wa Karatu, Dk Willibrod Slaa amedai kuwa baada ya Ballali kufukuzwa kazi wiki iliyopita alitorokea katika Kisiwa cha Malta kwa lengo la kujificha.


Katika mahojiano na Mwananchi, Dk Slaa alidai kuwa amepata habari kuwa wiki iliyopita Ballali aliondoka Marekani kwa ndege ya kukodi kuelekea Kisiwa cha Malta ili asiweze kurejeshwa nchini kujibu tuhuma za ufisadi zinazomkabili.


"Nimepata taarifa kwamba Ballali wiki iliyopita alikodi ndege kwenda kujificha katika Kisiwa cha Malta ili asirejeshwe nchini, pia nimeambiwa aliondoka na madaktari watatu, baadaye nitatoa majina yao na namba za ndege aliyotumia," alisema Dk Slaa.


Awali, Msemaji wa Ubalozi wa Marekani nchini, Jaffery Salaiz, alisema wameamua kumfutia viza baada ya serikali ya Tanzania kuulizia hadhi ya gavana huyo anaposafiri au kuwako nchini mwao.


Alisema kwamba kwa mujibu wa sheria za uhamiaji za nchi hiyo, kuanzia sasa Ballali hawezi kuishi katika nchi hiyo wala kusafiri kwa kuwa viza yake imefutwa.


"Hakuna njia yoyote Ballali anaweza kuishi Marekani kwa kuwa viza yake imefutwa, hata kama ana mali kule," alisema.


Pia Afisa Balozi huyo alipoulizwa kama wana habari kuhusiana na Ballali kuwako katika matibabu nchini Marekani, alisema mpaka sasa hawajui kama kweli yuko nchini mwao, kwani wao wamekuwa wakisoma katika vyombo vya habari vya ndani.


"Mpaka sasa hatuna uhakika kwamba Ballali yuko Marekani, habari za kuwako kwake Marekani tumezipata kupitia vyombo vya habari vya ndani, lakini kama ubalozi hatuna taarifa rasmi kwa hilo," alisema.


Alisema Ballali alikuwa na viza ambayo alipewa kwa wadhifa wake wa kuwa Gavana wa BoT, lakini baada ya kufukuzwa kazi kwa madai ya ufisadi, imefutwa.


Hata hivyo, alisema kama Ballali atakuwa nchini Marekani basi itambidi arejee nchini Tanzania kwa kuwa hana kibali cha kuishi nchini humo.


Katika taarifa ya awali ya ubalozi, ilisema hatua hiyo inatokana na Ballali kutokuwa tena gavana wa BoT baada ya kuachishwa kazi.


Ballali ameachishwa kazi na Rais Jakaya Kikwete, baada ya kubainika ufisadi wa zaidi ya Sh 133 bilioni ambazo zililipwa chini ya uongozi wake.


Ufisadi huo unahusu Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ambayo ukaguzi wa Kampuni ya Ernst&Young, ulithibitisha kufanyika katika kipindi cha mwaka 2005/06.


Marekani ikizungumzia zaidi sakata hilo, ilisema Tanzania iliulizia kuhusu hadhi ya Ballali, baada ya kuachishwa kazi kufuatia kubainika ufisadi huo mkubwa wa fedha za umma katika akaunti moja.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo, serikali ya Marekani tayari imeitaarifu Serikali ya Tanzania kuwa inabatilisha viza ya Ballali kwa sababu haiwakilishi tena Tanzania.


Marekani ilisema Ballali alipewa viza hiyo kutokana na wadhifa wake kama mwakilishi wa Serikali ya Tanzania.


"Kwa hiyo, kwa sababu ajira yake sasa imesitishwa, haiwakilishi tena serikali ya Tanzania na hastahili kuwa na viza aliyo nayo sasa hivi ambayo siyo ya kuhamia Marekani (non-immigrant visa status).


"Kuongeza uwazi na kupiga vita ufisadi ni maadili makuu mawili ambayo

Serikali ya Marekani na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

vinayathamini sana," ilisema taarifa hiyo.


Taarifa hiyo ilisema kuwa Marekani inaunga mkono uamuzi wa Serikali ya Tanzania kufanya uchunguzi kuhusu ubadhirifu uliofanywa kwenye BoT na inaamini kuwa uamuzi huu unadhihirisha azma ya Rais Kikwete kupambana na vitendo vya rushwa.


Katika taarifa hiyo, Marekani ilisema kuwa uchunguzi na ufunguzi wa mashtaka

wa haraka kwa wahusika katika kadhia ya BoT ni muhimu.


"Nchi zetu mbili zinafanya juhudi za dhati kufanya kazi pamoja kwa karibu katika

kung'oa mizizi ya rushwa na kumpeleka mbele ya vyombo vya sheria, mtu

yeyote atakayepatikana na makosa ya kujihusisha na vitendo vya rushwa," ilisema taarifa hiyo.


Katika hatua nyingine, Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alimweleza mwandishi wa gazeti hili ofisini kwake jana kwamba, haijajulikana lini Ballali atarejea nchini kwa kuwa bado anaendelea na matibabu.


Profesa Ndulu alifafanua kwamba, Ballali kwa sasa anapata matibabu katika hospitali ambayo iko karibu na nyumbani kwake.


"Siwezi kujua atarejea lini nchini kwa sababu bado anaumwa, kuumwa anaumwa kweli," alisema Profesa Ndulu.


Kumekuwa na utata kuhusu Ballali kwamba amekuwa na uraia wa nchi mbili yaani Tanzania na Marekani hivyo kuwepo hofu ya kutorejea nchini.


Hata hivyo, uamuzi huo wa Marekani unaweza kuwa hatua moja mbele katika kushirikiana na serikali ya Tanzania kumrejesha Ballali nchini iwapo atahitajika kuja kujibu tuhuma za ufisadi.
 
Hii sasa ni very interesting, kama serikali ya Tanzania imemwulizia, ina maana USA hawawezi kumpa visa. Hapo hii habari inaanza kuwa tamu.

Huenda kweli jamaa kakimbia.

Wengine yetu macho. Huenda spinning zote hizi ni danganya toto wakati ana panga moves zake, hii sasa ni chess.
 
Hii sasa ni very interesting, kama serikali ya Tanzania imemwulizia, ina maana USA hawawezi kumpa visa. Hapo hii habari inaanza kuwa tamu.

Huenda kweli jamaa kakimbia.

Wengine yetu macho. Huenda spinning zote hizi ni danganya toto wakati ana panga moves zake, hii sasa ni chess.

Mtanzania,

chukua pop corn na pepsi usubirie movie hii kwa sababu ndio mwanzo sasa pesa za wizi zilizomweka Kikwete ikulu zimeanza kuwasha na kila aliyezigusa ameanza kupanic.

Balali ni kansa kwa Kikwete na mafisadi wenzake. Mramba na Mgonja nasikia wako kwenye simu 24 hours kufuatilia maendeleo ya this guy.
 
anikagawie ili nimhoji.. na ukata wa KLH News.. shoot! ila sinitakuta na mimi ninatafuna hela zetu au ndio nitahurumiwa kwa sababu nazitafuna kwa ajili ya "usalama wa Taifa"..?

Anyway, I hope Dr. Slaa is right kwamba Balali amekimbilia Malta, maana kama atakuwa bado yupo hapa na anazungumza na kuonekana na watu wanaotaka kumuona naye kuwaona.. basi Dr. Slaa inaweza akawa setup kumpunguzia credibility.. I'll tread very careful..
 
Back
Top Bottom