Ballali alizifanyia nini fedha alizoiba??

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,811
2,765
Kama ilivyoada kwa mafisadi wengi hujitutumua sana kwa ajili ya kujionyesha kwamba wanamshiko wa nguvu wakaweza kujenga ama kununua majumba ya kifahari ama kununua magari ya kifahari, huyu Ballali alizaliwa Iringa Mafinga naomba mwenye picha ya makazi ya huko Mafinga aturushie ili tupate picha kamili. Nikitolea mifano ya mafisadi kama Lukaza, Mokubo wameonyesha waziwazi matumizi yao yasiyo ya kawaida ya pesa zetu wakajulikana ni mafisadi hasa, sina maana ya kumtetea huyu Ballali bali nataka kujua amefanyia nini fedha zetu????
 
Familia yake waliwahi kulalamika hapa kwamba hawana kitu.

Hata wangeamua kumzika kwao ingelikuwa balaa tupu. Jamaa anaenda kufungia ndoa Italy huku ndugu zake hata pa kulala panawapa shida.

Hao ndio wasomi wakuu na watumishi wa IMF, wanashindwa kusaidia ndugu zao, je watasaidia nchi?

Hizo pesa wanafaidi akina Anna Muganda huko USA. Sidhani kama familia ya Ballali itaona kitu.

Hii story inafanana sana na ya maboutu, sikuamini kuona anazikwa na watu kama sita baada ya kuiba mabilioni na kuyaacha Uswisi, Wazungu wakifaidi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom