Ballali aja

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Kama hii ina ukweli, basi inabidi awe muangalifu sana. Kama kweli hahusiki basi mafisadi hawatakubali ushahidi wake ujulikane kwa Watanzania hivyo wanaweza kumuua.
Ballali aja

na Charles Mullinda
Tanzania Daima

KASHFA ya ubadhirifu wa fedha za Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeanza kuchukua sura mpya, baada ya aliyekuwa gavana wa benki hiyo, Daudi Ballali, kuanza maandalizi ya kurejea nchini huku akiwa na vielelezo nyeti na muhimu vya sakata hilo zima.
Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumapili imezipata, zinaeleza kuwa Ballali anajiandaa kurejea nchini akiwa na vielelezo vinavyowaonyesha wahusika wakuu wa ubadhirifu huo, wakiwemo viongozi wa juu serikalini.

Mmoja wa viongozi wa juu wastaafu wa serikali ambaye amekuwa akiwasiliana na Ballali katika siku za karibuni, amelieleza gazeti hili kuwa alizungumza naye Alhamisi usiku wiki hii na kumhakikishia kwamba anajiandaa kurejea nchini akiwa na ushahidi wa wahusika wakuu wa sakata hilo.

Kiongozi huyo ambaye jina lake tunalihifadhi, alisema kwamba kwa siku kadhaa sasa tangu uteuzi wa wadhifa wake katika BoT ulipotenguliwa na Rais Jakaya Kikwete, amekuwa akiwasiliana na watu kadhaa mashuhuri wanaoheshimika hapa nchini pamoja na wanasheria.

Alisema Ballali ambaye sasa yuko nyumbani kwake nchini Marekani baada ya kutoka hospitalini, hali yake inaendelea vizuri na amekuwa akiongoza jitihada za kukabiliana na tuhuma zinazomkabili yeye mwenyewe, huku akisaidiwa na watu walio karibu naye.

Kiongozi huyo alimkariri Ballali akieleza kuwa alisikitika sana kuona sakata zima la kashfa hiyo likimwangukia yeye, wakati baadhi ya viongozi wakuu serikalini wakiwa wanafahamu fika kuwa alichokuwa akikifanya ni utekelezaji wa amri za wakubwa.

Katika kile kinachoonyesha kuunga mkono hoja hiyo ya Ballali, baadhi ya wataalamu waliobobea katika nyanja za uchumi na fedha, walilieleza gazeti hili kuwa kwa kawaida, gavana wa Benki Kuu hana mamlaka ya kuidhinisha utoaji wa fedha kwa ajili ya kuilipa kampuni au mtu fulani, ama kutolipwa mtu au kampuni fulani.

Mabingwa hao wa uchumi walieleza kuwa maelekezo ya kutolewa fedha za serikali kwa malipo ya aina yoyote, hutolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha.

Habari zaidi kutoka kwa watu walio karibu na Ballali, zinaeleza kuwa chanzo cha ugunduzi wa kashfa ya BoT ni malipo ya zaidi ya sh bilioni 30 yaliyofanywa kwa Kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd, fedha hizo zililipwa kwa kampuni hiyo ikiwa haijafanya kazi yoyote inayostahili kulipwa kiasi hicho cha fedha.

Hata hivyo, ilielezwa kuwa Ballali hakuhusika na uidhinishaji wa malipo hayo, bali yalifanywa kwa maelekezo ya kiongozi mmoja wa juu katika Serikali ya Awamu ya Tatu ambaye Ballali ana nakala yake ya kutoa maagizo maalumu ya maandishi ya kufanya malipo hayo.

Hili linaonyesha kuwa maelezo ya hivi karibuni yaliyotolewa na Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, yakieleza kwamba Ballali alimshauri kuidhinisha malipo hayo kwa ajili ya kazi maalumu za serikali si sahihi, bali Ballali alitumiwa kama mjumbe wa kutolewa kwa fedha hizo.

Inaelezwa zaidi kwamba sehemu ya fedha zilizochukuliwa katika Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) na kulipwa kwa Kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd, ziliingizwa isivyo halali katika kampeni ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2005, zikikinufaisha moja ya vyama vya siasa, kilichoshiriki uchaguzi huo.

Hata hivyo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba jana alilieleza gazeti hili kupitia simu yake ya kiganjani kuwa chama chake hakihusiki na kupatiwa fedha hizo.

"Kwanza, siijui kabisa kampuni hiyo ya Kagoda, na chama changu huwa hakipokei fedha kutoka kwenye makampuni, zikija za msamaria mwema kama wewe, nazipokea na ninatoa risiti…hesebu zetu ziko wazi, zimekaguliwa na juzi tu tumezipeleka kwa Msajili wa Vyama," alisema Makamba.

Lakini Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willbrod Slaa, alipoulizwa kupitia simu yake ya kiganjani, alisema ushahidi wa mazingira unaonyesha kuwepo kwa uwezekano mkubwa wa fedha zilizochotwa BoT kutumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

Kwamba ushahidi huo unaonyesha kuwepo kwa uwezekano wa fedha hizo kutumiwa na CCM katika kusaka ushindi.

"Ukiangalia mwenendo wa uchotaji wa fedha hizo, utaona kuwa zilianza kuchotwa Agosti 1, 2005, wakati huo CCM ilikuwa katika mchakato wa kuwapata wagombea ubunge wa chama hicho.

"Ziliendelea kuchotwa hadi Oktoba 27, wakati aliyekuwa mgombea mwenza wa wadhifa wa urais kupitia CHADEMA alipofariki dunia, ndipo uchotaji huo ukakoma.

"Makamba anapaswa aeleze ni kina nani walioichangia CCM kutengeneza fulana na vifaa vingine, ilivyotumia katika kampeni za uchaguzi huo," alisema Dk. Slaa.

Wakati hayo yakiendelea, kwa wiki nzima sasa baadhi ya viongozi wakuu wastaafu wa serikali na watu wengine mashuhuri wamekuwa wakitafakari kwa kina suala hili la kashfa ya ubadhirifu katika akaunti ya EPA.

Tanzania Daima imethibitishiwa na watu walio karibu na viongozi hao kuwa mmoja wa viongozi hao ametahadharisha wenzake katika moja ya vikao vyao kuwa iwapo suala hilo litafuatiliwa kwa usahihi, baadhi ya viongozi wa juu waliopo madarakani sasa na baadhi ya waliokuwa madarakani katika Serikali ya Awamu ya Tatu ambao majina yao tunayo, wanaweza kupoteza nyadhifa zao, heshima zao, ama kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria kujibu tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa mbali na mfanyabiashara, Jayantkumar Chandubhai Patel, ambaye jina lake linaonekana katika kumbukumbu zilizoko kwa wakala wa utoaji wa leseni za biashara (BRELA), za orodha ya kampuni 22 zilizotajwa kuhusika na upotevu wa fedha katika akaunti ya EPA, baadhi ya watu wengine mashuhuri wanaotajwatajwa kuwemo katika suala hili majina yao hayaonekani, ingawa ushahidi wa mazingira unawahusisha moja kwa moja katika kadhia hii.

Taarifa nyingine zilizolifikia gazeti hili hivi karibuni zinaeleza kuwa mwanasheria mmoja maarufu ambaye taasisi yake imetajwa kuhusika katika suala hilo la EPA ameanza kuchukua hatua za kisheria kusafisha jina lake na kampuni yake, akiamini kuwa hakuhusika kwa namna yoyote kuliibia taifa.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, tangu uamuzi wa Rais Kikwete wa kutaka kufanyika uchunguzi dhidi ya kampuni zilizotajwa kuhusika katika kashfa hiyo, ikiwemo kampuni ya mwanasheria huyo, wateja kadhaa aliokuwa akiwawakilisha kisheria wamejiondoa kwake, hivyo kumsababishia hasara ya mamilioni ya shilingi.
 
Hili scandal ndio kwanza linachipua na wengi wataadhirika siyo tu kwa kumwaga unga bali pia hata kwenda jela na kufilisiwa mali zao. Wataanza kutajana mmoja baada ya mwingine.
 
Ni kweli anakwenda na hayo mawasiliano yamefanyika, au ndio mdogo wake kasema?
Kama ni kweli basi its a good move, ndio kutakuwa kumkoma nyani giladi kwenyewe hadi kwenye milima ya golani
 
Mimi najuzi nilisema na MWK akaitikia na leo mwanakijiji anasema. Nina uhakika kwamba watu wana boost PR hapa . Balali haendi kokote na kusema najua atasema when is the right time na Visa anayo .Sasa nawashangaa wanao kimbila kuandika sijui ndiyo kumfanya JK apande chart ? Sijui ila nakerwa na waandishi ambao hawajafanya uchunguzi wa habari zao na kuanza kuropoka . Ballali katulia anapiga hesabu namna ya kuwamaliza akina Meghji na wao wanalijua hili kabisa .Hajaenda Malta waka Washington.Yuko pale pale yaani pale
 
Mimi najuzi nilisema na MWK akaitikia na leo mwanakijiji anasema. Nina uhakika kwamba watu wana boost PR hapa . Balali haendi kokote na kusema najua atasema when is the right time na Visa anayo .Sasa nawashangaa wanao kimbila kuandika sijui ndiyo kumfanya JK apande chart ? Sijui ila nakerwa na waandishi ambao hawajafanya uchunguzi wa habari zao na kuanza kuropoka . Ballali katulia anapiga hesabu namna ya kuwamaliza akina Meghji na wao wanalijua hili kabisa .Hajaenda Malta waka Washington.Yuko pale pale yaani pale

Yuko palepale, anafanya mambo yaleyale kwa namna ileile, na yote anayotuhumiwa anakusudia kuyakana vilevile, nasi tutaendelea kunung'unika hapahapa, hivihivi. Teh teh teh!! Redykyulass!!

"Sisi wale tumekuja hapa tunajua kile kitu kimetuleta hapahapa. Na wale vijana kazi yenu inakuja kufanywa hapa leo. Na kazi yako unaijua! Kazi yako ukiwa mchezaji si kwenda kukaa kuangalia mpira! Kazi yako ni kupeleka mpira palepale! Na mutu akiuchukua huo mupira, munyang'anye, muwekee palepale! Na kama hutafanya kazi yako, utaashikwa, utakanyagwa, na kukusahau!"
[media]http://www.youtube.com/watch?v=dreSavBNCIo[/media]
 
I think this a big mistake, anatakiwa asiseme chochote kuhusu ujio wake, ikibidi ashukie nchi jirani. Waungwana wakishajua nia yake ya kurudi watakua wakimsubiri airport 24/7 na ni wazi watamchoma ndani kum silence.
 
kama kweli haya ni mapambano sidhani kama balali atakuwa tayari
kuwaeleza maadui zake anapanga kufanya nini. kama hii taarifa ni kweli inaweza kuwa diversion au zinga la deterence
 
...ha ahaha ahah haha...mtasubiri mpaka yesu arudi hapo,na ndio imetoka hiyo hamtamuona tena na mkichelewa hata wale waliotajwa nao watapotea kuanzia Jeetu patel mpaka kina Lukaza nasikia nao wameanza kuingia mitini,tayari nishaona hakuna mtu yeyote hapo atashtakiwa au itaishia WANATAFUTWA TUU kama yule muhindi wa radar...pesa wamekula na tunawajua na hatutazipata tena na kesi hakuna...yaani ni usanii tuu!
 
Hodi,
Mimi bado mgeni JF. Jamani naomba nielimishwe kidogo kuhusu msemo huu "kumkoma nyani giladi" nimekutana nao mara nyingi sasa. Nadhani kwa ugeni wangu kuuliza ni muhimu wakati huu naijifunza JF.
Thanks
 
Hodi,
Mimi bado mgeni JF. Jamani naomba nielimishwe kidogo kuhusu msemo huu "kumkoma nyani giladi" nimekutana nao mara nyingi sasa. Nadhani kwa ugeni wangu kuuliza ni muhimu wakati huu naijifunza JF.
Thanks

Shapu, Karibu jamvini!! Unaweza kupata maana sahihi ya neno hilo kwenye POST HII ILIYOPO KWENYE THREAD YA KUMPONGEZA Mzee ES (enzi hizo -August 2006)!! Nitainukuu hapa chini kwa wengine pia kusoma moja kwa moja:

1. Heshima ziwarudie wakuu wote wa hii forum, kuanzia waasisi kina Mzee Invisible the Admin, Mzee Mwanakijiji, Bob Mkandara, Mzee Mtanzania, Bros Ogah, Mkuu Willo, Mzee Mwalimu Moshi, Mzee wa kazi Nyani, Mzee Jasusi, na Mtu wa pwani.

2. Kwako Mzee TZ njema, heshima mbele mkuu wangu kwa kunikumbusha kitu ambacho hakikuwemo kabisa kichwani mwangu, kwamba ninakaribia mchango wa 2000!

3. Mzee wangu, nimefaidika sana na hii forum, kwanza kwa kupima skills zangu kisiasa, maana huu ni uwanja mkubwa sana, na pia kujifunza mawazo ya kimaendeleo ya wa-Tanzania wenzangu, na hasa kuvumilia mawe ambayo yamekuwa yakitupwa kuelekea kwangu, na pia cha muhimu kuliko yote nimejifunza mengi, kuanzia BCS, ambayo yalinisaidia sana kuisaidia kiushauri kambi ya makamu wa CCM, Dr. John Malecela, wakati wa kampeni za uchaguzi wa mgombea urais wa CCM, uliopita. Huu uwanja ulinisaidia sana kutoa ushauri wa kila siku, na hata tuliposhindwa, nikajiunga na kambi ya Muungwana, bado nilikuwa ninachota ideas nyingi sana hapa na kuzipenyeza, ni tabia ambayo ninaendelea nayo mpaka leo, ya kupenyezea wakuu, topic ambazo ni muhimu sana kwa taifa letu!

4. Toka nijiunge na BCS, TEF, na sasa ikawa JF, tumewahi kutoa topic niyngi sana muhimu, lakini ni zile za Kumtaka Mahita ajiuzulu, Richmond, na hii ya juzi ya BOT & Gavana ndio ninazichukulia kama the best to come out of this forums, ambapo I am proud to a part of!

5. Kukwazika imenitokea mara mbili so far, tukiwa BCS na wakati mmoja TEF, mabapo ilibidi nidanganye kwa mara ya kwanza kuwa ninaondoka, ili kuwapoteza lengo maadui zangu ambao walikuwa karibu sana, na mbao sasa nimewatupa mbali sana, otherwise siku zote imekuwa tu ni burudani ndani ya bulogu, I mean saaafi!

6. "Kumkoma Nyani Giladi", Kiungani amesema tayari ni lugha ya pwani na kibaharia, kwamba ukitaka kumpiga nyani, usimuangalie usoni, ikiwa na maana kuwa hapa forum tunmpiga nyani CCM, Serikali, Upinzani, na wananchi pia, ili tuwapige vizuri hatuwezi kuwaangalia usoni, kwa hiyo kumkoma nyani mbele na forum juu zaidi!

7. Mzee Philemon, heshima mbele mkuu maana hata wewe mkuu ukisema, basi kwangu ni amina, na kwa heshima yako nitamuomba Admin, anibadilishe jina la Komandoo na kuwa Field Marshall ES, wakati wowte atakapopata nafasi maana wengi hapa tunajaribu tu, lakini wewe viatu vyako hapa forum hatuwezi kuvivaa kabisa, kwa hiyo unachosema kwangu ni amina mkuu, na so be it!

8. Mzee Joka, na Gme Theory, ahsante wakuu nina mke tayari, na mimi ni mkristo safi mke mmoja tu!, lakini heshima mbele kwa offer!

9. Mzee Mtanzania, heshima yako kwangu ni muhimu sana, ikurudie mkuu maana wewe toka enzi zile za BCS, Mwawado you are the future power wa hii forum ongeza michango, na imarisha imege ya jina lako njia ni nyeupe! Jembax2, Mugongox2, Mtu wa pwani, Joka kuu, Masanja, Killtime, Kalamu, wote nyinyi ndio hasa the future wa hii foirum!

10. Mzee wangu Mswahili sijakuona, na mku wangu Engineer Mohd, nyinyi niwaite mabaharia wenzangu, keep it up!

Kumkoma Nyani Giadi, mpaka kieleweke!

Ahsanteni Wakuu Wangu Wote mliojitolea kutoa heshima kwenye hii thred, Mungu kama aliwapa jana kidogo, kesho awape kikubwa!

Inshallah!

SteveD.
 
Bubu said:


Katika kile kinachoonyesha kuunga mkono hoja hiyo ya Ballali, baadhi ya wataalamu waliobobea katika nyanja za uchumi na fedha, walilieleza gazeti hili kuwa kwa kawaida, gavana wa Benki Kuu hana mamlaka ya kuidhinisha utoaji wa fedha kwa ajili ya kuilipa kampuni au mtu fulani, ama kutolipwa mtu au kampuni fulani.

Mabingwa hao wa uchumi walieleza kuwa maelekezo ya kutolewa fedha za serikali kwa malipo ya aina yoyote, hutolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha.


Kuna watu walisema ya kuwa hakuna uhusiano kati ya BOT na wizara ya fedha , kitu ambacho ni tofauti na wataalamu wa uchumi wanachosema.
 
Hao wataalamu wa fedha ndugu yangu wanahitaji kusoma Sheria iliyounda BoT. Kama hawawezi wanaweza kumsikiliza Bi. Meghji kwenye KLH News kwani nilimuuliza swali hilo "kuna uhusiano gani wa kiutendaji au kiusimamizi kati ya Wizara ya fedha na Benki Kuu". Gavana wa Benki anawajibika kwa Rais.
 
Nyinyi endeleeni kudanganywa, siku Balali atakayo rudi TZ atarudi kabadilika Jina badala ya Balali atakuwa anaitwa MAREHEMU.....

Na stori nyingi utasikia na vyombo vya habari vitakuwa na heading hii BALALI AFARIKI NA HEART ATTACK. "kutokana na shutuma zilizokuwa zinamkabili mh. Balali ampeta ungonjwa wa shinikizo la damu na imempelekea kufariki dunia"HIVYO NDIO MAGAZETI NA TAARIFA ZA HABARI ZITAKUWA.......
 
Watanzania tunatakiwa kuingia mtaaani tumwambie JK kuwa tunataka
1.Riport original ya wakaguzi
2.Wale wote waliohusika bila kujali nafasi zao akiwamo yeye mwenyewe msumeno ufanye kazi yake.
Bila kufanya hivyo yeye na chama chake waanze kufunga virago kabla ya 2010
 
Back
Top Bottom