Ballali aja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ballali aja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 20, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,798
  Likes Received: 83,172
  Trophy Points: 280
  Kama hii ina ukweli, basi inabidi awe muangalifu sana. Kama kweli hahusiki basi mafisadi hawatakubali ushahidi wake ujulikane kwa Watanzania hivyo wanaweza kumuua.
  Ballali aja

  na Charles Mullinda
  Tanzania Daima

  KASHFA ya ubadhirifu wa fedha za Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeanza kuchukua sura mpya, baada ya aliyekuwa gavana wa benki hiyo, Daudi Ballali, kuanza maandalizi ya kurejea nchini huku akiwa na vielelezo nyeti na muhimu vya sakata hilo zima.
  Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumapili imezipata, zinaeleza kuwa Ballali anajiandaa kurejea nchini akiwa na vielelezo vinavyowaonyesha wahusika wakuu wa ubadhirifu huo, wakiwemo viongozi wa juu serikalini.

  Mmoja wa viongozi wa juu wastaafu wa serikali ambaye amekuwa akiwasiliana na Ballali katika siku za karibuni, amelieleza gazeti hili kuwa alizungumza naye Alhamisi usiku wiki hii na kumhakikishia kwamba anajiandaa kurejea nchini akiwa na ushahidi wa wahusika wakuu wa sakata hilo.

  Kiongozi huyo ambaye jina lake tunalihifadhi, alisema kwamba kwa siku kadhaa sasa tangu uteuzi wa wadhifa wake katika BoT ulipotenguliwa na Rais Jakaya Kikwete, amekuwa akiwasiliana na watu kadhaa mashuhuri wanaoheshimika hapa nchini pamoja na wanasheria.

  Alisema Ballali ambaye sasa yuko nyumbani kwake nchini Marekani baada ya kutoka hospitalini, hali yake inaendelea vizuri na amekuwa akiongoza jitihada za kukabiliana na tuhuma zinazomkabili yeye mwenyewe, huku akisaidiwa na watu walio karibu naye.

  Kiongozi huyo alimkariri Ballali akieleza kuwa alisikitika sana kuona sakata zima la kashfa hiyo likimwangukia yeye, wakati baadhi ya viongozi wakuu serikalini wakiwa wanafahamu fika kuwa alichokuwa akikifanya ni utekelezaji wa amri za wakubwa.

  Katika kile kinachoonyesha kuunga mkono hoja hiyo ya Ballali, baadhi ya wataalamu waliobobea katika nyanja za uchumi na fedha, walilieleza gazeti hili kuwa kwa kawaida, gavana wa Benki Kuu hana mamlaka ya kuidhinisha utoaji wa fedha kwa ajili ya kuilipa kampuni au mtu fulani, ama kutolipwa mtu au kampuni fulani.

  Mabingwa hao wa uchumi walieleza kuwa maelekezo ya kutolewa fedha za serikali kwa malipo ya aina yoyote, hutolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha.

  Habari zaidi kutoka kwa watu walio karibu na Ballali, zinaeleza kuwa chanzo cha ugunduzi wa kashfa ya BoT ni malipo ya zaidi ya sh bilioni 30 yaliyofanywa kwa Kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd, fedha hizo zililipwa kwa kampuni hiyo ikiwa haijafanya kazi yoyote inayostahili kulipwa kiasi hicho cha fedha.

  Hata hivyo, ilielezwa kuwa Ballali hakuhusika na uidhinishaji wa malipo hayo, bali yalifanywa kwa maelekezo ya kiongozi mmoja wa juu katika Serikali ya Awamu ya Tatu ambaye Ballali ana nakala yake ya kutoa maagizo maalumu ya maandishi ya kufanya malipo hayo.

  Hili linaonyesha kuwa maelezo ya hivi karibuni yaliyotolewa na Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, yakieleza kwamba Ballali alimshauri kuidhinisha malipo hayo kwa ajili ya kazi maalumu za serikali si sahihi, bali Ballali alitumiwa kama mjumbe wa kutolewa kwa fedha hizo.

  Inaelezwa zaidi kwamba sehemu ya fedha zilizochukuliwa katika Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) na kulipwa kwa Kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd, ziliingizwa isivyo halali katika kampeni ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2005, zikikinufaisha moja ya vyama vya siasa, kilichoshiriki uchaguzi huo.

  Hata hivyo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba jana alilieleza gazeti hili kupitia simu yake ya kiganjani kuwa chama chake hakihusiki na kupatiwa fedha hizo.

  "Kwanza, siijui kabisa kampuni hiyo ya Kagoda, na chama changu huwa hakipokei fedha kutoka kwenye makampuni, zikija za msamaria mwema kama wewe, nazipokea na ninatoa risitiĀ…hesebu zetu ziko wazi, zimekaguliwa na juzi tu tumezipeleka kwa Msajili wa Vyama," alisema Makamba.

  Lakini Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willbrod Slaa, alipoulizwa kupitia simu yake ya kiganjani, alisema ushahidi wa mazingira unaonyesha kuwepo kwa uwezekano mkubwa wa fedha zilizochotwa BoT kutumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

  Kwamba ushahidi huo unaonyesha kuwepo kwa uwezekano wa fedha hizo kutumiwa na CCM katika kusaka ushindi.

  "Ukiangalia mwenendo wa uchotaji wa fedha hizo, utaona kuwa zilianza kuchotwa Agosti 1, 2005, wakati huo CCM ilikuwa katika mchakato wa kuwapata wagombea ubunge wa chama hicho.

  "Ziliendelea kuchotwa hadi Oktoba 27, wakati aliyekuwa mgombea mwenza wa wadhifa wa urais kupitia CHADEMA alipofariki dunia, ndipo uchotaji huo ukakoma.

  "Makamba anapaswa aeleze ni kina nani walioichangia CCM kutengeneza fulana na vifaa vingine, ilivyotumia katika kampeni za uchaguzi huo," alisema Dk. Slaa.

  Wakati hayo yakiendelea, kwa wiki nzima sasa baadhi ya viongozi wakuu wastaafu wa serikali na watu wengine mashuhuri wamekuwa wakitafakari kwa kina suala hili la kashfa ya ubadhirifu katika akaunti ya EPA.

  Tanzania Daima imethibitishiwa na watu walio karibu na viongozi hao kuwa mmoja wa viongozi hao ametahadharisha wenzake katika moja ya vikao vyao kuwa iwapo suala hilo litafuatiliwa kwa usahihi, baadhi ya viongozi wa juu waliopo madarakani sasa na baadhi ya waliokuwa madarakani katika Serikali ya Awamu ya Tatu ambao majina yao tunayo, wanaweza kupoteza nyadhifa zao, heshima zao, ama kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria kujibu tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma.

  Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa mbali na mfanyabiashara, Jayantkumar Chandubhai Patel, ambaye jina lake linaonekana katika kumbukumbu zilizoko kwa wakala wa utoaji wa leseni za biashara (BRELA), za orodha ya kampuni 22 zilizotajwa kuhusika na upotevu wa fedha katika akaunti ya EPA, baadhi ya watu wengine mashuhuri wanaotajwatajwa kuwemo katika suala hili majina yao hayaonekani, ingawa ushahidi wa mazingira unawahusisha moja kwa moja katika kadhia hii.

  Taarifa nyingine zilizolifikia gazeti hili hivi karibuni zinaeleza kuwa mwanasheria mmoja maarufu ambaye taasisi yake imetajwa kuhusika katika suala hilo la EPA ameanza kuchukua hatua za kisheria kusafisha jina lake na kampuni yake, akiamini kuwa hakuhusika kwa namna yoyote kuliibia taifa.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo, tangu uamuzi wa Rais Kikwete wa kutaka kufanyika uchunguzi dhidi ya kampuni zilizotajwa kuhusika katika kashfa hiyo, ikiwemo kampuni ya mwanasheria huyo, wateja kadhaa aliokuwa akiwawakilisha kisheria wamejiondoa kwake, hivyo kumsababishia hasara ya mamilioni ya shilingi.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jan 20, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kuna mtu anamseti mtu mwingine.. mimi simo! chess chess chess protect the King!
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,798
  Likes Received: 83,172
  Trophy Points: 280
  Hili scandal ndio kwanza linachipua na wengi wataadhirika siyo tu kwa kumwaga unga bali pia hata kwenda jela na kufilisiwa mali zao. Wataanza kutajana mmoja baada ya mwingine.
   
 4. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2008
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Ni kweli anakwenda na hayo mawasiliano yamefanyika, au ndio mdogo wake kasema?
  Kama ni kweli basi its a good move, ndio kutakuwa kumkoma nyani giladi kwenyewe hadi kwenye milima ya golani
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jan 20, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  haendi kokote... wangoje tu..
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mimi najuzi nilisema na MWK akaitikia na leo mwanakijiji anasema. Nina uhakika kwamba watu wana boost PR hapa . Balali haendi kokote na kusema najua atasema when is the right time na Visa anayo .Sasa nawashangaa wanao kimbila kuandika sijui ndiyo kumfanya JK apande chart ? Sijui ila nakerwa na waandishi ambao hawajafanya uchunguzi wa habari zao na kuanza kuropoka . Ballali katulia anapiga hesabu namna ya kuwamaliza akina Meghji na wao wanalijua hili kabisa .Hajaenda Malta waka Washington.Yuko pale pale yaani pale
   
 7. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Yuko palepale, anafanya mambo yaleyale kwa namna ileile, na yote anayotuhumiwa anakusudia kuyakana vilevile, nasi tutaendelea kunung'unika hapahapa, hivihivi. Teh teh teh!! Redykyulass!!

  "Sisi wale tumekuja hapa tunajua kile kitu kimetuleta hapahapa. Na wale vijana kazi yenu inakuja kufanywa hapa leo. Na kazi yako unaijua! Kazi yako ukiwa mchezaji si kwenda kukaa kuangalia mpira! Kazi yako ni kupeleka mpira palepale! Na mutu akiuchukua huo mupira, munyang'anye, muwekee palepale! Na kama hutafanya kazi yako, utaashikwa, utakanyagwa, na kukusahau!"
  [media]http://www.youtube.com/watch?v=dreSavBNCIo[/media]
   
 8. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 135
  I think this a big mistake, anatakiwa asiseme chochote kuhusu ujio wake, ikibidi ashukie nchi jirani. Waungwana wakishajua nia yake ya kurudi watakua wakimsubiri airport 24/7 na ni wazi watamchoma ndani kum silence.
   
 9. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2008
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  kama kweli haya ni mapambano sidhani kama balali atakuwa tayari
  kuwaeleza maadui zake anapanga kufanya nini. kama hii taarifa ni kweli inaweza kuwa diversion au zinga la deterence
   
 10. K

  Koba JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...ha ahaha ahah haha...mtasubiri mpaka yesu arudi hapo,na ndio imetoka hiyo hamtamuona tena na mkichelewa hata wale waliotajwa nao watapotea kuanzia Jeetu patel mpaka kina Lukaza nasikia nao wameanza kuingia mitini,tayari nishaona hakuna mtu yeyote hapo atashtakiwa au itaishia WANATAFUTWA TUU kama yule muhindi wa radar...pesa wamekula na tunawajua na hatutazipata tena na kesi hakuna...yaani ni usanii tuu!
   
 11. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2008
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,920
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hodi,
  Mimi bado mgeni JF. Jamani naomba nielimishwe kidogo kuhusu msemo huu "kumkoma nyani giladi" nimekutana nao mara nyingi sasa. Nadhani kwa ugeni wangu kuuliza ni muhimu wakati huu naijifunza JF.
  Thanks
   
 12. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #12
  Jan 21, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Shapu, Karibu jamvini!! Unaweza kupata maana sahihi ya neno hilo kwenye POST HII ILIYOPO KWENYE THREAD YA KUMPONGEZA Mzee ES (enzi hizo -August 2006)!! Nitainukuu hapa chini kwa wengine pia kusoma moja kwa moja:

  SteveD.
   
 13. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #13
  Jan 21, 2008
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Kuna watu walisema ya kuwa hakuna uhusiano kati ya BOT na wizara ya fedha , kitu ambacho ni tofauti na wataalamu wa uchumi wanachosema.
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Jan 21, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hao wataalamu wa fedha ndugu yangu wanahitaji kusoma Sheria iliyounda BoT. Kama hawawezi wanaweza kumsikiliza Bi. Meghji kwenye KLH News kwani nilimuuliza swali hilo "kuna uhusiano gani wa kiutendaji au kiusimamizi kati ya Wizara ya fedha na Benki Kuu". Gavana wa Benki anawajibika kwa Rais.
   
 15. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #15
  Jan 21, 2008
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nyinyi endeleeni kudanganywa, siku Balali atakayo rudi TZ atarudi kabadilika Jina badala ya Balali atakuwa anaitwa MAREHEMU.....

  Na stori nyingi utasikia na vyombo vya habari vitakuwa na heading hii BALALI AFARIKI NA HEART ATTACK. "kutokana na shutuma zilizokuwa zinamkabili mh. Balali ampeta ungonjwa wa shinikizo la damu na imempelekea kufariki dunia"HIVYO NDIO MAGAZETI NA TAARIFA ZA HABARI ZITAKUWA.......
   
 16. Nyangumi

  Nyangumi JF-Expert Member

  #16
  Jan 21, 2008
  Joined: Jan 4, 2007
  Messages: 508
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania tunatakiwa kuingia mtaaani tumwambie JK kuwa tunataka
  1.Riport original ya wakaguzi
  2.Wale wote waliohusika bila kujali nafasi zao akiwamo yeye mwenyewe msumeno ufanye kazi yake.
  Bila kufanya hivyo yeye na chama chake waanze kufunga virago kabla ya 2010
   
 17. Mack Wild

  Mack Wild JF-Expert Member

  #17
  Dec 23, 2017
  Joined: Apr 25, 2013
  Messages: 4,323
  Likes Received: 2,746
  Trophy Points: 280
  bado hajafika niko eapoti
   
Loading...