Balile na Dr Slaa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balile na Dr Slaa...

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ngareni3, Aug 25, 2010.

 1. N

  Ngareni3 Member

  #1
  Aug 25, 2010
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Makala ya Bw Deodatus Balile katika gazeti la Mtanzania toleo no 0856-5678 lenye kichwa cha habari "Dk Slaa avunja ndoa" imenishangaza sana. Imenishangaza kwa sababu kadhaa, kwanza, mtu kama Balile, ambaye ana kadigrii ka uzamili bado hana upeo wa kujua kuna maisha binafsi ya mtu, ambayo kuyaingilia ni sawa na kuvaa chupi ya mtu? Ndio, public figures wanasema hawana maisha binafsi lakini si kweli... Unapoanza kudodosa mtu kwa kutumia gazeti lako, na mwingine akitumia gazeti lake kudodosa mwingine na mwingine je, tutapona kweli...

  Wagombea wetu wakuu wameanza kampeni za kistaarabu na kiungwana sana, kuliko wakati wowote katika historia ya vyama vingi. Huyu Balile asitupeleke huko.. Au ndo anataka naye kutoka kwa uchaguzi wa mwaka huu kama wenzie waleeeeee waliotokea kwa uchaguzi wa 2005? Balile kama kweli una hako kashahada ka uzamili, unapaswa kujua kuna njia nyingi za kutokea...

  Unakumbuka makala yako ile ukiwa Tanzania Daima ukijikomboka kwa Waziri Membe? Jikumbushe

  Makala -Membe; fursa hii tusiipoteze

  Ile haikukutoa sasa umeanza na uchaguzi wa mwaka huu? Mimi sishabikii mtu au chama chochote, lakini ni vyema waandishi wakawasaidia wapiga kura kujua changamoto zao na aina ya wagombea wanaotakiwa katika maeneo yao? Kama alivyosema Kardinali Pengo, kuwa Mapadri wake wasisaidie wanasiasa wapumbavu, na mimi nasema, waandishi wapumbavu wasiwavuruge wananchi.

  Pili kusema kuwa utakutana na Dr Slaa Uraiani, pia unaonyesha kukosa upeo wa kufikiri kama kweli una hiyo shahada ya uzamili. Kitendo cha Dr slaa kuingia - aishinde au asishinde ni chachu kubwa na nzito katika uchaguzi wa mwaka huu. Hatungependa uchaguzi wa rubber stamp. unaona jasho wanalotoa wenzetu sasa... hiyo ndiyo demokrasia... na hapo ndipo dr slaa na chama chake walipoonyesha kuwa maslahi ya nchi yapo mbele ya maslahi binafsi daima. kwa watanzania na wanademokrasia hiyo ni zawadi ya pekee.... Any other issue ni personal life..... Tukiamua kupekuana hakuna atakayetembea tena barabarani. Usitupeleke huko... kwa maslahi yako binafsi.

  epuka kupandia ngazi isiyo yako....
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mwambie Balile wako wengi wanaomfahamu tangu kwao Nyanga Bukoba, akisoma Kishoju akifundisha Mugeza akisoma Nyegezi kwa msaada wa mafadha kwa kutembeza bakuri na kutokea mwananchi, Tanzania daima then Kikundi cha habari za Rostam aziz, si kwamba hatumfahamu.

  Twamuelewa na tena kwa undani. Tukieleza ya kwake chumbani ataikimbia nchi. Mengine tunyamaze tu maana yanayohusu ndoa yanamkabili kila mwanaume na hata JEYKEY yanamkabili. Hayo anayoandika ni non sense ambayo anaweza kuburuzwa mahakamani.
   
 3. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mpelekeni mahakamani ikapatikane haki!
   
 4. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huyo Balile ni aina ya watu ambao hata wakiambiwa wajilipue atajilipua.

  Kwa sisi tuliosoma psychology ukiangalia sura yake (kwenye picha, maana sijawahi kukutana naye uso kwa uso) utagundua ni mtu wa kujikomba sana na anayetekeleza maagizo bila kufikiri. Pia anaonyesha ni mtu mwenye chuki.

  Nashangaa kusikia eti huyu naye ana elimu ya chuo kikuu! Kama ni kweli basi ni miongoni mwa wale watu ambao wamepata elimu lakini hawajaelimika. Huyu huyu ndiye aliyeandika ile makala ya kipumbavu ya kusifia suti na viatu vya Lowassa wakati ule alipotimuliwa uwaziri mkuu kwa ufisadi, na kurejea Monduli kuwadanganya watu akijifanya eti ni shujaa aliyeachia uwaziri mkuu. Balile alikuwa kwenye msafara kule Monduli na kuandika habari ambayo itabaki katika kumbukumbu kama habari ya kipuuzi kabisa iliyowahi kuandikwa na gazeti la Mtanzania.

  Kwa wale mlio makini nawashari msipoteze pesa na muda wenu kununua na kulisoma hilo gazeti la Rostam kwani limejaa waandishi na wahariri vibaraka wanaotumiwa kama condom.
   
 5. N

  Ngareni3 Member

  #5
  Aug 25, 2010
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi yule mwingine yuleeeeeeee wa uchaguzi wa 2005 ambaye sasa ni mdomo wa jengo jeupe alitokea hapo hapo habari corporation au alitokea wapi? nadhani dogo naye pengine ndo strategy ya kutoka....
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,547
  Likes Received: 18,204
  Trophy Points: 280
  Naamini kilichoandikwa siyo kazi ya RA, bali naamini ni kazi binafsi ya mhariri kilaza kwa jina la Deodatus Balile, akitaka kuyaiga yaliofanywa na Salva na timu yake wakati wa kampeni ya 2005 dhidi ya Dr.Salim.

  Baada ya Salva kuyafanya aliyoyafanya, mambo yake yakawa safi, baada tuu ya mkulu kuingia magogoni, Salva huyo, akaula. Sasa huyu kilaza Balile anataka kuiga tembo ... kwa kujikomba komba kwa JK kwa staili ile ile akisubiri Salva apigwe ubalozini akiamini labda yeye ataitwa!.

  Kwenye fani ya habari, jamani, hizi njaa zetu wakati mwingine zitatuua!. Hapa kwa wanafani, mheshimiwa sana Balile, amejidhalilisha japo nakizi alichoandika sio majungu, wala hakutunga bali ni hard facts ila tatizo ni jinsi alivyoziwasilisha ikiwemo kutaka kulisha watu maneno.

  Credibility ya Magazeti ya Mtanzania, ilishashuka zamani wanachofanya sasa ni kuimalizia tuu, naomba mimi niwe wa kwanza kuitabiria Habari Corp kifo cha mende mara tuu baada ya uchaguzi kwa sababu wanamdhania RA ataendelea kubebwa ili na yeye awabebe, no way,
  kwa vile itakuwa ndio term ya mwisho kwa mborongaji, atahakikisha haborongi tena ili aache legacy, with nothing to loose, wasitegemee tena kama atawategemea wapambe wa style ya RA, atawatosa ili angalau wasizidi kumchafua.

  Kwa wale wenye mapenzi mema na Dr. Slaa, this is not a big deal, he is human, tit for tat za aina hii ni too low kwa mapambano ya kupigania maslahi ya taifa.

  Balile ya timu yenu, endelezeni kazi nzuri mnayoifanya, your days are numbered na malipo ni hapa hapa duniani!.
   
 7. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 929
  Likes Received: 696
  Trophy Points: 180
  Lakini pia ni vema, tukamshtua Balile kuwa Mke/kimada wake analalamika kuwa Balile anamlazimisha kila wakati kwenda kumtegeshea RA achombeze ili Balile afumanie na kudai fidia.

  Mama yule maskini analalamika kwa wanawake wenzake na kumshangaa mwenzake. Ameapa kuwa ni heri wafe maskini kuliko kutumiwa namna hii. Nadhani kinachofuata ni Balile kuvaa gauni ili hiyo aifanye mwenyewe! Njaa nyingine jamani.
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,547
  Likes Received: 18,204
  Trophy Points: 280
  Mchukia Fisadi, kuna kusoma na kuelimika. Kusoma ni kupitia vidato na kujipatia makaratasi, vyeti, shahada hata za uzamili na wengine mpaka Ph.D lakini bado wakawa ni vilaza na mbumbumbu tuu na hivi ndivyo mimi binafsi ninavyomtafsiri Balile.

  Mtu mwenye akili zake timamu, hawezi kujikomba kwa type ya Balile. Hivi hawezi kujifunza kwa kaka yake Mhingo?!. Jinsi alivyojituma kwenye kampeni ya JK mwaka 2005, wengi tunajua na alichoambulia pia tunakijua, angekuwa na yeye ni kilaza, ndio angejikomba.

  Kazi aliyoifanya Salva enzi zake inajulikana na malipo yake yameonekana, ila hiyo ni bahati ya Salva, Balile ukitaka kuiga kwa kudhania utaula kama alivyoula Salva, umepotea na sasa subiria tuu kuzimika.

  Angalizo, Hata hizo baadhi ya Masters za wanahabari, sio siri ni Masters za mashaka mashaka, enzi hizo unamaliza form 4 na Divisheni four yako, unaenda TSJ au Nyegezi unachukua Diploma ya Journalism kwa miaka miwili (Wakati huo hapo ndio mwisho kwa Tanzania, kulikuwa hakuna zaidi ya hapo), ukitoka unapelekwa vyuo vya ng'ambo kuchukua Masters, ukirudi hapa na masters yako, basi ndio unaitambia saana eti ni msomi, huku unaandika utumbo!.

  Waandishi wa type hii wako wengi tuu wenye vimasters uchwala na kuishia kujidhalilisha.

  Haya yakiendelea, tutaishauri NACTE kufanya marejeo, hivi vi masters baada tuu ya Diploma za miaka 2 nazo ni masters?!.
   
 9. N

  Nanu JF-Expert Member

  #9
  Aug 25, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nadhani Balile anajikomba komba tu. Hii inafuatiwa na ile taarifa ya Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam kuwa mapadri wasitumiwe. Hiyo ilikuwa na mantiki kuwa labda nguvu kubwa ya Dr. Slaa ipo kanisani wakati siyo kweli.

  Kila mtu anamfahamu Dr. Slaa na uchapaji kazi wake bila kuogopa chochote au kupendelea. Kama tuna umakini kama Watanzania basi CHADEMA mwaka huu italeta ushindani mkubwa kwenye uchaguzi na ndicho tunachohitaji. Tunahitaji mawazo mbadala, sera mbadala na utendaji mbadala. Hatutaki kuendelea kufanya kazi ile ile vile vile.
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Aug 25, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Pasco nakukubali kabisa unachosema.
  Ila angalia asije kusema unamuonea wivu kwa sababu yeye ana hiyo postgraduate degree inayoitwa masters na wewe una BA tu!. Lakini ukweli Balile ni kilaza si uongo. Tena ni mzushi wa viwango vya juu.
   
 11. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #11
  Aug 25, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mmmmmhh mmmmhhh kweli njaa ni siasa!!
   
 12. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #12
  Aug 25, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  BALILE=CONDOM (pamoja na elimu yake uchwara)
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  Aug 25, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hujamtendea haki pamoja na upuuzi wake alionao kumlinganisha na Kondamno.
   
Loading...